CCM, Angelina Mabula na Stanslaus Mabula, hizo nyumba zilizouzwa na Jiji la Mwanza zinaenda kuwa ajenda ya kwanza ya wapinzani. Mtatikiswa!

CCM, Angelina Mabula na Stanslaus Mabula, hizo nyumba zilizouzwa na Jiji la Mwanza zinaenda kuwa ajenda ya kwanza ya wapinzani. Mtatikiswa!

Rais Samia amefungulia mikutano ya hadhara, na katika majiji ambayo Chadema wanajiwinda kuyadhibiti ni Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam. Wanatafuta ajenda nzito za kutikisa na kuwashika wananchi.

Arusha walifanya tukio, Sasa hivi wote wananyea debe, angalau wanaarusha wanaelewa hatua zimechukuliwa.

Kwa Jiji la Mwanza, Mkurugenzi wa Jiji na maafisa ardhi nao hawajachelewa kuwapa wapinzani ajenda.

Kuna habari kwamba Jiji la mwanza limeuza nyumba zake katikati ya Jiji kwa bei ya kutupa, bila kufuata taratibu.

Maeneo hayo yameuzwa wakati machinga mjini hawana maeneo ya biashara, wameenda kutupwa igoma nyamongolo huko ambako hakuna wateja, na kiloleli, na bila kuzingatia maelekezo ya Rais ya ubia kati ya sekta binafsi na Serikali, kiasi kwamba wangeongea na taasisi yoyote ile au mtu binafsi, akawekeza, wakawa wanakula faida, na eneo likabali lao.

Ni kwamba, wanamwanza wameibiwa.

Stanslaus Mabula, wewe ndio mbunge wa Nyamagana, bila shaka unalijua Jimbo linakuwaga la moto, hasa ukizingatia "sponsor kafa".

Angelina Mabula, wewe ndio Waziri wa hiyo ardhi ya serikali iliyouzwa, na uhamishaji miliki usingefanyika bila kupitia Ofisi za ardhi. Na sijui kwa nini kama mamlaka ya serikali inapotaka kuuza ardhi isitakiwe kupata Kibali Cha Waziri wa Ardhi au Waziri Mkuu! Au Rais! Uwepo udhibiti.

Mna kazi moja tu, kuirudisha ardhi hiyo, hatutaki Rais aanze kupata shida kupata kura za Mwanza wakati alishanyoosha mapito yake kwa miradi mikubwa ya maendeleo.

Ni hapohapo mwanza machinga aliyekuwa anauza ndizi, Jiji lilimwaga ndizi zake na kumpiga, Leo Jiji Lina ardhi hapohapo katikati ya mji linaiuza!

Njia moja tu, kurejesha hizo nyumba, na Kila Afisa aliyehusika apelekwe mahakamani, wanamwanza wataridhika wakiwaona wahusika wanapanda kizimbani, na kupelekwa gereza la Butimba.
Wala usipate shida hakuna lolote litakalofanyika kwani sio Mwanza tu ni kawaida ya Mawaziri wa Ardhi wa Tanzania kudhulumu ardhi za watu bilakuona aibu hata ndege za Tanzania hazitatuka ulaya kwani waliodhuliwa na hao Mawaziri ni wengi na wako nchi mbalimbali na kesi zinafunguliwakila siku ulaya dhidi ya hiyo nchi ya kidhalimu
 
Takukuru itafanya nini wakati order imetoka kwa anayewalipa mshahara😂😂😂😂😂😂😂
Takukuru wa Tanzania ndio wezi wenyewe usipoteze mda wako kwenda Takukuru kuwajulisha chochote nasikia wanaomba pesa ulaya eti waboreshe taasisi yao itabidi tujulishe serikali za ulaya kuwa Takukuru ndio matapeli na hawafai kupewa msaada kutoka kodi zetu huku ulaya
 
Angelina ana husika nini viwanja vimekaa miaka 20 adi vinaota vichuguu, sheria ya ardhi inasemaje kwa viwanja visivyoendelezwa.
Kuna viwanja vingapi ambavyo vimekaa miaka nenda rudi nahakuna mtu anagusa??Tena unawezakuwa jirani na viwanjaambavyo hawathubutu kugusa alafu cha kwako wanakuletea uhanithi. Hiyo imejaa majambazi wa ardhi na mali za watu lakini wananchi ni wapole hawajui haki zao wanadanganywakila siku
 
Sheria inasemaukifyeka na kuweka ukutaumedhaendeleza ujinga utaisha lini Tanzania??
Wala sio ukuta wa matofali kweli kuna shida sana Tanzania katika kudhulumu mali za watu hasa ardhi na utakuta Watanzania wengi wanasamehe na kumuachia mungu inabidi wawe kama Wayahudi jino kwa jino jicho kwa jicho mpaka wote tumalizane na vizazi vyao ndio watuelewa mtu akikudhulumu ardhi usimsamehe lipa kisasi ndio watashika adabu na kuogopa kuiba mali za watu
 
Na ndiyo maana hoja ya majimbo inatakiwa, viongozi wachaguliwe na wananchi ili waweze kuwajibishwa haraka.

Hili la kungojea mamlaka za uteuzi zilizopo Dodoma na Dar es Salaam kuamua masuala ya ardhi iliyopo jijini Mwanza inaleta jeuri kwa wateuliwa.

Lakini kama mkuu wa wilaya au mkoa / jimbo angekuwa amechaguliwa na wananchi na viongozi wengine wakaomba ajira ktk jimbo basi kutimuliwa ingekuwa rahisi bila kusubiri mamlaka za uteuzi za waziri au rais ambaye hajui hata kiwanja hicho kipo wapi na kina umuhimu gani kwa mfano jiji la Mwanza.
 
Back
Top Bottom