Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimewaonya viongozi wa chama wanaotumia vibaya mali za chama huku kikisisitiza kuwa hakitavumilia uzembe na ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulani Ramsey, wakati akizungumzia maandalizi ya ziara ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, inayotarajiwa kufanyika mkoani Arusha kuanzia Juni 4 hadi 6 mwaka huu.
Ramsey amesema chama kimebaini baadhi ya viongozi waliopewa pikipiki kwa ajili ya shughuli za maendeleo na uhamasishaji wa shughuli za chama wamekuwa wakibadilisha muonekano wa vyombo hivyo kwa kuweka makava mapya au kufanya mabadiliko yasiyoruhusiwa kinyume na taratibu zilizowekwa. Amesema viongozi watakaobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kunyang’anywa vyombo hivyo vya usafiri, huku akisisitiza kuwa mali za chama zinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Wakati huo huo, Ramsey amesema maandalizi ya ziara ya Kenani Kihongosi yamekamilika ambapo ataanza ziara yake Wilaya ya Karatu kabla ya kuendelea Arumeru na baadaye Arusha Mjini. Amesema ziara hiyo inalenga kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya viongozi wa chama na serikali katika ngazi mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki na kushirikishwa katika masuala ya maendeleo.