Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimetoa ufafanuzi kuhusu madai yanayomkabili aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mbureni, Faraja Maliaki, ambaye hivi karibuni ilisambaa video kwenye mitandao kijamii inayoonesha baadhi ya wanachama wa CCM kurudisha zawadi alizowapa wakidai kuwa ni rushwa ili aweze kupita kwenye mchakato wa kura za maoni
Akizungumza hivi karibuni kwa njia ya simu na Global TV, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipuran Ramsey, amesema kwa sasa chama kinafanya uchunguzi kubaini kama tukio hilo ni la kweli. Amesema endapo itathibitika kuwa diwani huyo alijihusisha na vitendo hivyo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake
“Mimi nimeona mitandaoni na chama kinaendelea kuchukua hatua kwanza katika kuhakikisha je jambo hilo ni la kweli? Ni kwei Diwani huyo alipeleka hivyo vitu? Kwa hiyo vikao vinaendelea na wanachama wale kama ni jambo la kweli na tunajua ni wanachama wetu kwakweli walitimiza ahadi namba 4 kwamba rushwa ni adui wa haki. Kama kweli amefanya hivyo vikao vitaamua”
Source: Global Online TV