Uchaguzi 2020 CCM asili tunampa Lissu kura zetu

Uchaguzi 2020 CCM asili tunampa Lissu kura zetu

Yaani wewe sijawahi kuona ukipinga hoja kwa vitendo au kwa point zenye mashiko..... Huyo ni mwana CCM mwenzako,

Mimi sina chama ila ninapoona hoja zako kwenye haya majukwaa huwa nafikiria sana na kujiuliza, wanaokulipa wanakulipa shilling ngapi

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
Halafu ananiachaga hoi,ana vicoment vyepesi mnoo na vya kitoto sana yan.
 
Mkuu unajua kabisa kuwa wewe sio CCM na bado tu ukaandika uzi kutudanganya.
 
Jana nilikuwa naongea na mzee wangu ambae ni CCM kindakindaki toka TANU lakini kwa sasa ana changamoto ya macho haoni ila ameniambia kura yake ni kwa Tundu Lissu! na amenishangaza hata haya mambo yanayoendelea na kampeni za Lissu zote anafuatilia.
 
Kuna wana ccm zaid ya hamsini ninaowafahamu watampa kura Lisu
CCM ipi unayoisema?
CCM haipo tena ,imeshatekwa na mtu mmoja,yeye ndiye kila kitu.
Kama huami ,Makamu mwenyekiti kwani ni nani?
Na yuko wapi?
 
Tunaonekana kijani, lakini mioyoni tuna jambo let. ......
1603594271119.png
 
Kuna wana ccm zaid ya hamsini ninaowafahamu watampa kura Lisu
Mm kwa ofisi yetu kulikuwa na wagombea 3 ,toka wanyimwe salary wakimchukia jamaa mazima na wanasema wazi watampa TL kura ,maccm yana Hali mbaya Sana saizi mbinu wanayotaka kuitumia kuhalalisha wizi ni kusema eti tayari Wana kura za wanachama wao mln.17 huo ni uhuni wakati kiukweli zaidi ya robo au nusu ya maccm wanampigia Tundu
 
Zamani zile walikuwa ni wazee waliokuwa wanachama wa ccm, hivi sasa wazee wa enzi zile wengi wao wameshafariki na miji yao imerithiwa na vijana.
Hii haiwezi kuwa ni moja wapo ya sababu zenu za kuhalalisha wizi wa kura.
Haya yalikuwa maoni yangu lakini pia na heshimu maoni yako
 
Kura kwa Lissu wana CCM wenzangu
Wewe mwanaCCM gani utakayempa kura Lissu? Kama wewe ni fisadi, huna uzalendo, mla rushwa, asiyependa maendeleo, anayependa ushoga, ..... NDIYO UTAMPA KURA huyu kibaraka wa Wazungu. Ujue kuwa mwenzako Lissu analianzisha hapa na kwamba tayari ana tiketi ya kukimbia nchi mara tuu baada ya uchaguzi maana anajua fika kuwa ATASHINDWA. Hata mshirika mwenzake Membe anajua Lissu hafai kuwa Rais. HATUDANGANYIKI. SISI WATANZANIA WA VYAMA VYOTE KURA ZETU KWA MAGUFULI.
 
Wewe ni chama cha Mbowe, unaona hata aibu kukisema hapa jukwaani. Lissu hawezi kuwa Rais wa Watanzania milele.
 
Kubaki nyuma ya ulimwengu wa kiliberali sawa lakini nimetoka Paris wiki 2 zimepita wetu wanataka JPM akawafanyizie kazi wakulima wa ngano na wafugaji. Yellow vest wanamhitaji kuliko mnavyodhani. Nyie jifurahisheni lakini mjiandae kisaikolojia
Labda kama Lengo langu ilikuwa ni kutueleza kuwa ulikuwa Paris Ila kimsingi hakuna point yoyote uliyoelezea hapo.
 
Mimi ni baadhi ya wahanga wa kamati kuu. Ingawa tulishinda kwenye kura za maoni matokeo yake najina yetu yalikatwa. Nilikuwa wa kwanza lakini baadae niliondolewa. Nilipohoji niliambiwa ntapigwa money laundering. Nikaufyata. Ila kwa kweli tuna jambo let tarehe 28 Oktoba.

Tuko wengi. Rafiki yangu ni katibu wa CCM mkoa, naye ana lake jambo 28 October. Yeye alimchangia Lissu laki 5 na mgombea ubunge laki moja. Tunaonekana kijani, lakini mioyoni tuna jambo let. Wana CCM wenzangu, CCM asili, fanyeni kweli tarehe 28 October.

Tugawane mbao na hawa CCM mpya. Kura kwa Lissu
There You are.... WanaCCM wengi tutampa kura Lisu.... Tumetukanwa sana na hawa wakina Bashiru na Pole Pole
 
Back
Top Bottom