Kura zitaendelea kununuliwa na wagombea kwa kutumia mawakala wao. Hapa wamewaongezea gharama wagombea wao. Njia nzuri ya kuwapata wagombea safi pamoja na kura hizi za wanachama ni kwafahamu kwa undani wagombea wetu na mema na mabaya yao yakawekwa hadharani. Vinginevyo tuendelee kutumia umasikini wa wapiga kura wetu kushinda kwa kishindo.
Mkuu WildCard, unapofanya uamuzi wa kuleta demokrasia, sio kwamba suala la rushwa litaondoka kabisa, lakini ni mojawapo ya mbinu ya kulipunguza. Kuongeza wigo wa wapiga kura ni jambo zuri, kuliko watu wachache waliokuwa wanatoa maamuzi ya wanachama kibao. Kununua kundi dogo ni rahisi kuliko watu kibao.
Unapozungumzia njia nzuri ya kuwapata wagombea kwa kujua mema na mabaya yao, ni wazo zuri. Lakini hata chaguzi zilizopita kuna watu walijulikana mabaya yao na wakapitishwa kugombea, huenda sababu ya rushwa. Hivyo kuongeza wapiga kura kwa hizi hatua za mwanzo ni wazo jema kabisa.
Kwa hili nawapa CCM hongera kubwa sana. Ila jitahidini basi mkiwekana sawa ndani ya CCM mtupe na tume ya uchaguzi huru, ndio uchaguzi utanoga.