Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, amesema matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, dhidi ya wanaharakati yalikuwa sahihi kwa kuwa, kama kiongozi, ni jukumu lake kuhakikisha tunu za taifa zinalindwa.
Jawadu ameyasema hayo leo, Alhamisi, Mei 22, 2025, jijini Dodoma, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kauli ya Rais Dkt. Samia aliyoitoa hivi karibuni dhidi ya wanaharakati wanaotoka nje ya nchi.
Amesema: "Kwa hiyo, matamshi ya Dkt. Samia dhidi ya
wanaharakati yalikuwa sahihi sana, na kwa kweli nadhani yalihitaji pia kuwa makali zaidi ya hapo, kwa sababu sisi tunafahamu kwa namna gani kupitia wanaharakati nchi mbalimbali duniani zimeanguka."
Aidha, ameongeza kuwa mashambulizi yanayotokea dhidi ya Rais Dkt. Samia yanathibitisha uwezo mkubwa alionao katika kusimamia misingi na maadili ya taifa.