PreGE2025 CCM Dodoma: Kauli ya Rais Samia dhidi ya Wanaharakati ilikuwa sahihi na ilipaswa kuwa Kali zaidi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, amesema matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, dhidi ya wanaharakati yalikuwa sahihi kwa kuwa, kama kiongozi, ni jukumu lake kuhakikisha tunu za taifa zinalindwa.

Jawadu ameyasema hayo leo, Alhamisi, Mei 22, 2025, jijini Dodoma, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kauli ya Rais Dkt. Samia aliyoitoa hivi karibuni dhidi ya wanaharakati wanaotoka nje ya nchi.

Amesema: "Kwa hiyo, matamshi ya Dkt. Samia dhidi ya

wanaharakati yalikuwa sahihi sana, na kwa kweli nadhani yalihitaji pia kuwa makali zaidi ya hapo, kwa sababu sisi tunafahamu kwa namna gani kupitia wanaharakati nchi mbalimbali duniani zimeanguka."

Aidha, ameongeza kuwa mashambulizi yanayotokea dhidi ya Rais Dkt. Samia yanathibitisha uwezo mkubwa alionao katika kusimamia misingi na maadili ya taifa.

Your browser is not able to display this video.
 
Kauli za wachumia tumbo hazina manufaa kwa taifa!
 
Chawa tu
 
Vilaza kama huyu hawezi kuelewa athari za kauli aliyotoa, Samia anatukanwa 24/7 na vitoto vidogo na Image ya nchi inazidi kuchafuka. Vibaka kama huyu ndiyo wanamponza Samia
 
Ile kauli ya Samia ilikua nyepesi sanaaa! Manyang’au sio yakuchekea!
 
ulitegemea mbweha kama huyu ataongea nini maana ana akili mbili tu ya kuvukia barabara na ya kujua njia ya chooni
 
Vilaza kama huyu hawezi kuelewa athari za kauli aliyotoa, Samia anatukanwa 24/7 na vitoto vidogo na Image ya nchi inazidi kuchafuka. Vibaka kama huyu ndiyo wanamponza Samia
Kwenye mtandao wa X anadhalilishwa hadi aibu, kuna clip imewekwa jamaa anagusa tumbo (mimba). Ni kama ile mwanaume anagusa tumbo la mjamzito mtoto anapocheza.
Aibu yote ya nini... Sio kila ushauri wa kuutekeleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…