CCM fanyieni kazi kero hizi mbili za Muungano

Mkataba wa muungano wa 1964 suala la Ardhi halikua la muungano ni nani Aliengiiza Ardhi ya tanganyika kuwa ya muungano ? Na kwa nini Alifanya hivo?
 
Umepaniki sana.

Kinachotakiwa ni Usawa. Kama Muungano unamambo ya Muungano yabaki ya Muungano, yasio ya Muungano yabaki kuwa sio ya Muungano. Ibaki hivi.
Unayajua mambo yaliyo ya Muungano na yasiyo ya Muungano? Mkishika Dola ongezeni mnayoona yanafaa. Mtu anatoa hoja kwa kuwa kaisikia kwa fulani, ila haelewi hasa nini anachoongelea.

Muungani hauwezi kuwa sawa hata mapato hayawezi kuwa sawa, kwa sababu sehemu ya pili ya muungano ni ndogo kwa eneo na kwa idadi ya watu pia. Hivi mnatumia akili au ushabiki.
 
Ni hatari sana.

Na hii itawafanya CCM wapitie kipindi kigumu sana hata kwenye uchaguzi wa mitaa maana ndiko ardhi inauzwa.
Kwenye uchaguzi wanategemea Magufuli style, hivyo hawajali lolote ni lazima walinde huo muungano wa matambiko.
 
Ila hao wachache wanaweza kupata wabunge wengi!
 
Ukizielewa hoja inatosha.

Kwani waliungana ili wake wapate faida?
Haki haipimwi kwa wingi ama idadi.
Kama watu wao wanakuja huku na kununua ardhi, kwanini na sisi tusinunue ardhi? Kuna visiwa vingi tu a sio Zanzibar peke ake ila tunanunua ardhi na kukaa. Iweje wao wawe na hoja mfu?
Kwetu waje watawale, kwao kwenda kutawala haiwezekani? Shida Iko wapi?
 
Tanganyika siyo jina ila ni ardhi, ipo tangu zama hizo na wenye ardhi yao (Watanganyika) wanazaliwa kila leo.
 
Uchawa ukizidi unakuwa ujinga.
 
WAONDOE KIKOKOTOO,MENGINE BAADAE
 
Wewe ulitaka nini ikashindikana au na wewe umekaa nyumbani unaangalia clip za wanasiasa na kuitikia
 
Ila hao wachache wanaweza kupata wabunge wengi!
sijaona jibu la hoja, nini kimekosekana au kushindikana au na wewe unadandia hoja za wanasiasa.

Hebu tutumie akili ya kawaida tu ya kuzaliwa.
 
Sasa Unguja au Pemba kuna Ardhi ya kugawana?
Siyo swala la ardhi ya kugawana, ni swala la kuwepo na kizuizi bayana kikibagua watu.
Mimi nikikubaliana na rafiki yangu toka Zanzibar anipe kipande cha ardhi nami nimgawie kipande huku kwetu, mimi sitakubaliwa, kwa sababu tu natokea bara, siyo kwa sababu hakuna ardhi. Sijui kama umenielewa.
Udogo wa ardhi siyo hoja hata mara moja, ni kubaguliwa watu dhahiri kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…