CCM, gesi haiondoki Mtwara piga ua

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
16,950
Reaction score
13,527
Ccm habari hii iwakae sana akilini,na mkae mkijua ya kwamba suala la kuitoa gesi mtwara na kuihamishia sehemu zingne kutaathiri moja kwa moja maendeleo ya mkoa huo,,

kuna mpango ushaandaliwa wa kikwete kutaka kuipeleka gesi hii bagamoyo ili awalipe fadhila watu wa kwao pindi atapoondoka madarakani,,

suala hili halitavumilika hata kidogo,zipo juhudi za wanaharakati wa asasi zisizo za kiserikali zinafanywa kuupinga mpango hadi bungeni,,

gesi hii ingekua imegundulika arusha ccm ingethubutu kujenga bomba kuitoa arusha kuipeleka bagamoyo??ingethubutu??

Sasa kwa mtaji huu mmechokoza vita vingine,,ikibid hata msituni tutaingia,hata kujitenga tutajitenga,,


tuachieni gesi yetu tunufaike nayo,hatujakataa kugawa nishati kutokea mtwara kwenda sehemu zingne,tunachotaka ni uwepo wa gesi kanda ile ili kuwepo na ujenzi wa miundombinu,viwanda na kuongezeka kwa ajira za wananchi wa kanda ile

tutapigana sana katika hili
 

Attachments

  • GESI MTWARA.jpg
    20.5 KB · Views: 424
mkuu kwa hili nakupinga
gesi inapogunduliwa inakuwa ni kwa manufaa ya taifa zima na sio Mtwara pekee
mwekezaji anapopewa leseni ya kutafiti na kuchimba gesi na baadae mafuta anajenga pipelines
waliosoma hii wanasema anakuwa na plan for field development and na plan for installation
kutoka offshore kuja onshore,kisha wanaweka distribution,moja zitakuwa huko mtwara na zingine kuja dar kwa
ajili ya viwanda,kuzalisha umeme na matumizi mengineyo, huko ndiko kwenye market na matumizi
ingine wana wanachange form kuwa liquid ili isafirishwe nje.
walaji au watumiaji gesi mtwara ni wachache.
na ifahamike hiyo gesi hamwezi kuitumia majumbani bila kufanyiwa processing

Kuhusu kunufaika nayo ni suala la kiutawala serikali kuu kuamua na sio wananchi wa mtwara kuamua
Mlima Kilimanjaro au mbuga za wanyama haziwanufaishi watu wa Kilimanjaro pekee fedha zinaenda serikali kuu
labda mkitaka hivo mchague chadema wenye sera ya majimbo ndio mtanufaika kama katiba itaridhia majimbo.
Ukisoma policy mpya ya petroleum and gass ni kuwa mafuta na gesi ni mali ya watanzania wote na sio wana Mtwara
pekee.

Kwa hivo hakuna mwanamtwara mwenye haki ya kupinga hili.
wala msije mkaota.
 



sasa kwa mantiki hiyo kwanini waihamishe moja kwa moja kutoka sehemu ilipogundulika bila kuwashirikisha wananchi wa eneo hili husika??

Na kama wewe unasema gesi mtwara hawataimaliza wewe ulkua unatakaje waimalize watu wengne na sio wana mtwara,

kwani mtwara haihitaji viwanda?haihitaji miundombinu?haihitaji wakazi wa huku wapate ajira kutokana na miundombinu itayotokana na gesi hiyo??hatutaki yalitokea huko mwadui na sehemu zingne yajirudie,,na ndio maana tunataka ile rasimu ya sera ya gesi asili iliyoandaliwa na wizara ya nishati na madini iweke wzi zaid na sio kuficha ficha ukweli juu ya suala hili

upo uwezekano wa kuifanya gesi ikafanyiwa process zote huku huku mtwara then utaratibu mwingne bora zaid ukaangaliwa kwa baadae

wanaostahili kuona mabadiliko mi wenyewe wakazi wa huku kwanza
 
Mtwara kuna kiwanda gani mkuu?
shera iko wazi gesi na mafuta ni kwa manufaa ya wananchi wote na sio wa eneo moja tu.
nani atakuwa tayari kufanya processing Mtwara?

Tatizo hatuna sheria nzuri ya gesi,hatuna petroleum tax act,wala regulation zake
hela ambazo ziko uswizi ndio hizo watu wametoa fasta
fasta blocks kwa makampuni ya kutafiti na kuchimba gesi

hatujui serikali inachukua tax kiasi gani kwajili ya exploration na production of gas
wala wananchi hawajashirikishwa ili muwe na sauti na rasilimali yenu
watu wengine kutoka sehemu nyingine walishawaamulia kitambo

gesi mtaisikia tu inapita lakini mapato yake wanajua wao
hatuelewi kwanini wizara moja itoe vibali badala ya bunge kuidhinisha hilo ili kuepuka rushwa

hakuna chombo cha kumonitor nk
watu wanaofanya kazi kwenye blocks hizo TRA haiwajui,
mishahara yao haikatwi kodi,sisi hatuwafaidi kama taifa
ni wachache ndio waliobahatika kujiwekea fasta fasta uswizi
,kwa hivo mkuu safari bado ndefu sana
 
THE BIG SHOW! Suala si kuhamisha gesi mtwara, bali kuwa na mfumo wazi kuhakikisha jamii za mtwara zinapata first priority kuwekewa umeme/huduma hiyo ya gesi (japo nyumba nyingi kule ni nyasi na makuti....umaskini umekithiri) sijui namna gani wanaweza kulipia ankara za kila mwezi za TAANESCO! Pia, tunaweza hapa kuongelea Corporate social responsibility (CSR) na OPen Governance -kuhakiksha kunakuwepo uwazi katika makusanya ya kodi itokanayo na gesi na fungu fulani kuachiwa wananchi -(sio viongozi wao) waboreshe miundo mbinu maeneo yao
 



ni kweli mtwara hakuna viwanda,ila ni nani ataleTa viwanda sehemu ambazo hakuna nishati ya umeme??
Ni wazi kwa kupatikana kwa gesi hii sasa wawekezaji wangeona fursa ya kuja mtwara kuwekeza,labda nikuambie ya kwamba badala ya kuzubaa zubaa miaka chungu nzima ya kusafirisha korosho ghafi hii sasa ilikua ni nafasi ya kutumia viwanda vya kuprocess korosho hapa hapa nchini kwetu,hii ingeongeza ajira na vipato vya wananchi

pia kama unamfaham tajir mkubwa inawezekana akawa ni namba moja africa kutokana na takwimu za uhakika mnigeria anaitwa dangote kafungua viwanda na kuanza rasmi ujenz huo wa viwanda vya cement huku akiitarget gesi na bandari ya mtwara,hao na wengne wengi walianza kuja mtwara,leo wanaitoa gesi wanataka future ya kanda hii ielekee waPi??na kwa nin wamekurupuka bila kutoa elimu kwa wananchi??kuna nini hapo

vurugu lazima zitatokea kwa harakati zinazoendelea huku,kama huamin subiri
 



ni kweli mtwara ni mskini,lakin sio maskin kama unavodhani,ni serikali haijaipa kipaombele kanda hii,miaka nenda rudi,,tunamshukuru sana mkapa,bila yeye kuwa rais wa nchi hii,habari hii ya barabara ingeendelea kuwa ndoto kanda hii,atleast kaondoka na katuachia kitu cha kumkumbuka,,

watu wa mtwara sio maskini kias cha kushindwa kumudu gharama za umeme,ni propaganda za kuubeza mkoa huu,tandahimba ni wilaya ya pili katika halmashuri zinazoongoza kuingiza pato la taifa kwa kodi,na hii ni kutokana na zao la korosho,niambie serikali inathamini vipi mchango huu??

Sasa kwa kuwa wao wameamua kufunga vioo na kuwafanya watu wa huku ni mazuzu,messgi itapatikana kwenye suala la gesi,na kitaeleweka tuh
 
nasapato kwa sababu zifuatazo:-
1. Mtwara ni mkoa kama ulivyo Dar es Salaam na Ardhi ipo ya kujenga viwanda Serikali ifanye mtwara ndio kitovu cha viwanda.

2. Kama kuhamisha gesi ni rahisi basi na serikali nayo ifanye maamuzi ya haraka ya kuamia Dodoma.

3. Viwanda vikiwa kusini Mikoa yote ya kusini itakuwa kiuchumi na kuzalisha ajira nyingi zaidi.
 



just mkuu,,

thank you so much,,ni kwamba huu mwingne ni upumbavu wetu tuh wa watu wa mtwara kuiweka ccm madarakani,tunao mawaziri wawili hawa ghasia na mkuchika

hawa wanaingia moja kwa moja kwenye chombo cha maauzi ya serikali,badala ya kuutetea mkoa wao,wao wamekubali kuwa vibaraka wa kikwete na kuchumia tumbo,angekua ni waziri sitta,au magufuli au mwakyembe na gesi hii imegundulika makwao wasingeweza kuwa baridi kama walivokuwa hawa vihiyo ghasia na mkuchika,wanatia hasira sana kwa kweli
 
 
Hapa ndipo tunaona umuhimu wa devolved goverment. Sehemu zilizo baguliwa kimaendeleo ikiwemo Mtwara. zitafaidi rasilimali ya taifa. Hofu katiba mpya aka ccm sponsered katiba itapuuzilia mbali usawa mgawo wa mkate wa taifa.
 
uozo wote wa kudumaza maendeleo ya mtwara umeletwa na serikali ya ccm.Kibaya zaidi kila mara wanakuja mtwara kutengeneza majukwaa ya kueneza utapeli wao, kugawa kofia na tshirt za kijani NA mnawashangilia na kukejeli CDM. Hamuwahoji hata uwiano wa rasilimali zilizopo mtwara na mustakbali wa maendeleo ya mikoa hiyo ya kusini.Mnakesha mitandaoni mkimsapoti NAPE aliyeshindwa kuwaletea maendeleo akiwa mkuu wa wilaya huko kusini.Watu wa kusini Mnaiponda chadema ambayo kumbe imejaa sera za ukombozi wenu.Mmeshachelewa kulilia raisilimali za kusini, GESI ndiyo hiyoooooo inasepa, CCM watarudi tena kusini kujenga majukwaa ya kuomba kura.
 
Loh! Kuna watu humu wana akili zenye kukatisha tamaa. Kwani hiyo gesi ni taa kusema unaiondoa Mtwara na kuipeleka ikaangaze Bagamoyo?

Kwani madini yaliyopo Arusha yanatumika kuiendeleza Arusha peke yake? Akili za wapi hizi jamani!

Umeme mnaotumia mtwara miaka yote unatoka hapo mtwara? Cement mnayotumiwa ilikuwa inachimbwa hapo hapo Mtwara?
 
 



wewe tumia akili,huwezi kuyafananisha madini na gesi hata siku moja,,

tena kaa chini ufikiri mara mbili mbili usije kichwa kichwa hapa,mbona zanzibar mmeshindwa kuyachukua mafuta kule na kuitoa hoja ya mafuta na gesi kwenye suala la muungano??

Unahamisha gesi kuitoa mahala inapozalishwa kiholela unataka wenyewe wa mkoa husika wakae kimya??hawajashirikshwa,hawajui hatma ya zao hilo,unataka wasihoji??

Hakuna aliekataa kushare faida za gesi hiyo,tunapinga kuondolewa kwa gesi hiyo kwa hoja nyepesi nyepesi ya kwamba ni nyingi na haitaisha tukiitumia pekeetu,,sasa plan yao iishe au plan yao ni kuiwekea mipango stahiki??
Maendeleo ya sehemu husika hutokana na rasilimali za eneo hilo,unataka kuniambia mtwara inanufaika vipi na patola madini la huko kwenu arusha pamoja na watalii wanaokuja pande hizo??kama inanufaika basi ni kwa uchache sana,huko hampati ajira kutokana na madini??hampati ajira kutokana na utalii??

Unataka watu wa huku wajivunie vipi kwa gesi hii??
Huna akili kbs
 



kwa hapa ilipofikia hili suala ccm litawagharim tuh,

hadi bunge lijalo ujumbe wa wananchi utawafikia kwa namna yyte ile.,,haitakua rahisi kama wanavodhania
 
Wewe Lokisa nadhani haujamwelewa vizuri mtoa mada na pia una matatizo ya kupambanua hoja. Mtoa mada ameandika vizuri kuwa hakatai gesi kusambazwa nchini kwa matumizi anuwai. Alichodai ambacho ndiyo mantiki ya hoja ni kuwa kwanini kiwanda cha kuprocess hiyo gas kijengwe Pwani badala ya Mtwara? Je,kwa fikra zako viwanda pamoja na miundo mbinu mingine havistahili kujengwa Mtwara siyo? Wanachotaka watu wa Lindi na Mtwara ni kujengwa kwa kiwanda cha kuprocess gas huko huko Mtwara/Lindi ili kufungua fursa ya uwekezaji na ajira kwa watu wa mikoa hii. Au nikulize swali dogo au jepesi,"Je,kiwanda cha kuprocess gas kikijengwa Mtwara kutaifanya gas hiyo kutokuwa mali ya taifa/umma? Na je, kwa kiwanda kujengwa pwani ndiyo udhihirisho wa mali ya taifa?" Ni vema rasilimali za taifa hili zikanufaisha wananchi wote siyo sehemu fulani za nchi kama ilivyo sasa.
 
hapa ndipo tunaona umuhimu wa devolved goverment. Sehemu zilizo baguliwa kimaendeleo ikiwemo mtwara. Zitafaidi rasilimali ya taifa. Hofu katiba mpya aka ccm sponsered katiba itapuuzilia mbali usawa mgawo wa mkate wa taifa.


watu washaamka sasa,,pia washachoka kwa utumwa wao

wasubiri 2015
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…