Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Baada ya kifo cha Magufuli aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na baadaye kutenguliwa na kuteuliwa kuwa Mbunge, CCM haina uongozi wa juu na hivi sasa inategemea Dola kuendeshwa katika shughuli zake za kila siku.
Jambo hili si la afya kwa mustakabali wa siasa za nchi na rasilimali za umma.
Kwa vyovyote vile rasilimali nyingi za umma zinatumiwa na CCM kinyume na sheria za nchi na hivyo kukosa sifa za kuwa chama cha siasa.
Wito kwa msajili wa vyama vya siasa kuwakumbusha CCM kujaza haraka iwezekanavyo nafasi za uongozi zilizo wazi ili kuepusha muingiliano wa kimaslahi baina ya Serikali na CCM.