CCM haitathubutu kuipinga Rasimu

CCM haitathubutu kuipinga Rasimu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
CCM imeitisha Kikao cha Dharura cha Kamati Kuu kitakachofanyika mjini Dodoma. Lengo hasa la kikao hicho ni kuipitia na kuichambua Rasimu ya Katiba mpya iliyowasilishwa kwa watanzania na Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba.



Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana amenukuliwa na vyombo vya habari leo akisema kuwa CCM haikubaliani na mambo yote yaliyomo kwenye Rasimu.Baadaye leo,Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akasema kuwa maneno ya Kinana ni 'ya mtaani' na msimamo wa chama utatolewa baada ya kikao husika.



Nape,akihojiwa na BBC, akadai kuwa CCM wanajiandaa pia kuunda Mabaraza ya Katiba kama Taasisi. Amini nawaambia,CCM haitaipinga Rasimu hii.Kiukweli,Tume ya Warioba imedhibitiwa na CCM. Imeandaliwa na kuwasilishwa na watiifu wengi wa CCM wakiongozwa na Jaji Warioba. Itajadiliwa na kupitishwa chini ya CCM. Kwasasa na ilikofikia ,CCM haitaipinga.



Chama changu kimezoea mchezo wa kuvuta hisia za watanzania. Hufanya hivi hasa kwenye Uteuzi wa Mgombea wa Urais na wale wa Ubunge.Wanapenda kuteka bongo za wananchi ili wafuatiliwe na kusikilizwa watakachojadili huko Dodoma. Wanapenda 'kuwa hewani sana'.Hakuna zaidi. Hakuna jipya. CCM haitathubutu kuipinga Rasimu ya Warioba. Wanataka 'attention' tu!



Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Nakubaliana na wewe mkuu,nadhani kitengo cha propaganda kinafanya kazi yake.
 
Hilo linafahamika Mkuu , taarifa za Upekuzi zinaonyesha kwamba ccm waliiona rasimu hata kabla haijasomwa hadharani !
 
mkuu uccheze kabisa na CCM, hii rasimu kama umeisoma vizuri ni mwiba mchungu kwa wanasiasa wengi sana... acha wakae.. ila kina warioba wamefanya kazi yao!!!
 
Ushauri kwa CCM: Wajitahidi hii katiba iwe fair kwa vyama vya upinzani, maana wakati hii katiba itakapoanza kutumika effectively, CCM itakuwa chama cha upinzani. Wakijifanya kuipindisha ili ikibebe chama tawala, wajue wanaijengea CDM mteremko baada ya uchaguzi ujao...
 
Badala ya kuijadili tanganyika itafufukaje wao wanaeka chama mbele.
 
Siyaamini maccm msiwape trust mpaka karata ya mwisho. Wanaweza fanya chochote maana tatizo lao kubwa wengi ni wachumia matumbo yao na sio ss wananchi wa kawaida. ....
 
Back
Top Bottom