CCM haiwezi anguka kirahisi, ina kila namna ya kuwa-reward makada wake

CCM haiwezi anguka kirahisi, ina kila namna ya kuwa-reward makada wake

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Habari wakuu.

Baada ya kusoma kiarticle fulani, nimeona kitu hiki.

Tawala nyingi huanguka kutokea ndani. Si kitu rahisi watu kutoka nje kuangusha utawala ambao upo established. Mfano ni Rais wa Misri Mubarak, alianguka baada ya majenerali kuacha kumuunga mkono. Mambo yanayoweza sababisha watu wa karibu wenye ushawishi waache kukuunga mkono, moja ni kuona kuwa huna faida kwao tena. Au wakiona kuwa huko mbeleni hawatafaidika tena, hio ndiyo sababu baada ya jeshi kumuunga mkono Mugabe kwa miaka mingi, likaamua kumgeuka baada ya kuona kesho yao haijakaa poa.

Kwa hizi nchi za kidemokrasia, wanasiasa watakuunga mkono pale tu wanapoendelea kufaidika. Zaidi ya hapo utaangushwa kutokea ndani.

Sasa hii CCM, CCM wanasystem kubwa sana ya kuwanufaisha watu wao hadi wasione haja ya kuigeuka tokea ndani. Wanatumia nafasi za uwaziri, unaibu waziri, ukatibu mkuu, ubalozi, ukuu wa Wilaya, ukuu wa Mkoa, uDED, uRAS, UDAS na nyingine nyingi sana kuwareward watu wenye ushawishi. Mwanasiasa yeyote mwenye ushawishi ndani ya CCM ana uhakika wa kula. Na si rahisi mtu kuanza kuharibu anapokula.

Kiufupi CCM imejizatiti sana. Si rahisi kuangushwa labda litokee jambo ambalo lipo nje ya uwezo wao kama recession kali nk. Wote wanaoweza kuwa tishio kwa CCM wamekuwa 'taken care.'
 
Hayo yote kama Mungu ameamua hakuna cha kada wala mkereketwa. Rejea kwa dikteta Yahya Jammeh wa Gambia alikuwa madarakani miaka 22. Mwaka 2016 aliandaa uchaguzi tume ikiwa yake,jeshi lake,polisi yake,mahakama yake nk.

Tume hyohyo ilimtangaza mpinzani na mwenyekiti baada ya tangazo akakimbia nchi na kopi ya matokeo. Mahakama yake mwenyewe ikamgomea na majaji wakakimbia nchi.

Mwishowe jeshi na polisi nao wakamwacha. Alikimbia nchi mwenyewe. Kuna upepo ukikukataa wote wanakuacha.
 
Watu wenyewe wanaotaka kukiangusha ccm ndiyo hawa baada ya uchaguzi wanakimbilia
 
Back
Top Bottom