Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Yaani napita mitaani kila kona na hata kwenye maofisini hasa ofisi za umma katika watu 10 ninaowakuta 1 au 2 ndio wanapotezea CCM.Mitandao yote ya kijamii tukianzia humu JF, FB,Tweeter,Watsaap na mitandao miingine ya kijamii ukikuta wapo members 100 Basi utakuta 5 au 10 ndio wanaokitete CCM,Sasa CCM iko na nani?
Mnasema hiki chama kina maisha marefu kweli?
Chama kimebaki na Pole pamoja na Dkt. Bashiru ambao hata wakisema CCM oyeee yaani wanona aibu, hawafanyi na salamu hizi kwa sababu hawajazaliwa wala kulelewa katika itikadi zake. Mtu kama Nape au Makamba akisema CCM oyee utaona inatoka moyoni kabisa.
CCM kimebaki na vijana wachache wa UVCCM ambao wapo kimaslahi zaidi na wengine wapo humu, hawa ukikutana na mmoja mmoja pembezoni wanaongea mengine kabisa.
Watu wengi ni dhahiri sasa wamechoshwa na hiki chama kulingana na matendo yake. Hawana hamu nacho ndio maana wanaokishabikia ni wachache wanaonufaika na mfumo.