CCM, Halotel na DP World wana lao

CCM, Halotel na DP World wana lao

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Nimekuwa nikipokea SMS za CCM kupitia line ya Halotel Kama inavyoonekana hapo chini.

Pia soma: Kumbe Halotel ni CCM?

Screenshot_20230723-083329.png
 
Hawa watu ni wendawazimu...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Samia ameyumba sana. Aachane na matapeli wanaomdanganya kuwa watanganyika ni wajinga na hawajui lolote. Hata ukiwauza utumwani wataendelea na ushabiki kama wa simba na yanga.

Ataamka siku atajikuta
Na wanakula bando hao kenge siyo mchezo aisee
Samia ameyumba sana. Aachane na matapeli wanaomdanganya kuwa watanganyika ni wajinga na hawajui lolote. Hata ukiwauza utumwani wataendelea na ushabiki kama wa simba na yanga.

Ataamka siku atajikuta uhamishoni.
Uvivu wa Maprofesa wetu wa sheria umesababisha haya.
Kwani katiba ilioruhusu Zanzibar kuwa na serikali yake kamili, huku Tanganyika ikiwa haina serikali nyingine yake yenyewe, kwanini katiba hio sasa ikaruhusu Mzanzibari kurithi Urais wa serikali hii badala ya siku zote kuishia umakamu wa Rais kwa ajili tu ya kulinda maslaha ya Zanzibar ndani ya Muungano?

Ikitokea kama kifo cha Rais wa Tanzania basi kipengele kingesema aliekuwa Waziri Mkuu au Jaji Mkuu, Speaker wa Bunge ashike Urais hadi Uchaguzi mkuu ujao. Mzenji akibaki nafasi yake kivulini ya umakamu ili alinde maslaha ya nchi yao Zenji.

Uvivu huu sasa ndio unaumiza forever, haya mambo yatapelekea vita na nchi za kiarabu. Na tutavwamiwa kinguvvu. Nipo paleee nanywa kahawa mie
 
Na waliotaka kujitenga na Tanganyika na waliokuwa na chuki dhidi ya Tanganyika yupo huyo huyo, kama alivyokuwa bosi wake na Mentor wake mkuu Amana Karume.
Yaani huyooooooo, ndio huyo uliemfikiri na wewe!. Sema hamumjui tu
Mmeingia cha kike Tanganyika
 
Kumbe tumefika huku tayari?
Mithili ya kampeni za uchaguzi ?

Kuna kila sababu ya kuamini hii issue kuna la ziada nyuma yake.
Dola milioni 350 za rushwa zilizotolewa na DP zinafanya kazi. Zitawagusa watu binafsi, taasisi mbalimbali hadi makampuni.
 
Mbinu na Mikakati iliyozeeka toka kwa chama Kizee chenye wajinga wengi wanadhani kila m2 ni Km wao.
 
Dola milioni 350 za rushwa zilizotolewa na DP zinafanya kazi. Zitawagusa watu binafsi, taasisi mbalimbali hadi makampuni.
Na ifike hapo ili tujue maana halisi ya unafiki wa baadhi ya watu tunaowaheshimu.
 
Back
Top Bottom