Oneni maigizo ya CCM yalivyobuma japo wao wanavyoyapanga wanakua wanahisi "Wametumia Akili kwelikweli”.
Suala la Uenyekiti wa CHADEMA na Mgombea Urais Kupitia CHADEMA , maandalizi yalianza kwenye uchaguzi wa Ndani wa CHADEMA , hapa wakadhani wameshinda.
Lissu akagombea Uenyekiti, CCM wakatumia Kila mbinu Kumwangusha, Huku Pesa za Abdul zikisadikika kutumika, TUNDU LISSU AKASHINDA na akaanza Kampeni za NORENE .
CCM Wakaona alaaa, wakaanza nao Mikutano ya kujibu mashambulizi ,mara Virusi vya Ebola , M-Pox , bado LISSU AKAZIDI KUCHANJA MBUGA.
CCM Imemkamata LISSU wakampa Kesi ya UHAINI... Huku Nje kuanzia Mitandaoni Mtaani , nje ya Nchi ,na Dunia Kwa ujumla, wasomi wanasema "UHAINI SI MANENO , NI MIPANGO NA MATENDO".
CCM wakaja na Igizo la KUSAINISHA VYAMA 12/4 , akili zao zikadhan ni mtego, tuwaone kweli kama Hawatokuja, walidhani CHADEMA inatania na NORENE , Katibu Mkuu Mnyika akasema Hatoshiriki na Hajamtuma MTU ( hapa bila KM kusema, CCM ingeleta MTU wao wakasema alotumwa ).
KAILIMA WA CCM , alipoona CHADEMA wamerukà mtego, akaja na Hoja ya "Ambaye Hajasaini ,Hatoshiriki uchaguzi "
Kipigo kimemgeukia KAILIMA, haamini ,UJUAJI wake Mdogo wa Sheria na Katiba ya Nchi, wasomi wanamchachafya, kuanzia Tundu Lissu mpaka Wasomi Mmoja Mmoja mpaka Wananchi wa kawaida, tuliosoma Katiba tunasema "
Hamna kifungu kwenye katiba kinachosema chama kisiposaini kanuni za madili, hakitashiriki uchaguzi, hilo tisa, kumi katiba haitaji muda maalumu wa chama au vyama visainishww lini, wakati gan na baada ya muda gan havitasainishwa "
CCM Kila Igizo analokuja nalo, anapigwa KO.
Wenye Hekima, Busara na Akili, huko CCM mpo??