CCM hawana Ubavu wa kumfukuza Polepole kwa sababu ya Madudu ya Ndugai Bungeni

CCM hawana Ubavu wa kumfukuza Polepole kwa sababu ya Madudu ya Ndugai Bungeni

Ndugai na wana CCM wengine walishindwa kuona impact ya kuwacha bungeni Akina Harima Mdee na wenzake kwamba ikitokea mwana CCM akatakiwa kuvuliwa chama Na apoteze ubunge hawez kuvuliwa Kwa sababu kuna wale COVID 19??
COVID 19 imeng'ania kama ruba😄.Je kinyonga atashindwa kung'ania zaidi?
 
Akina Polepole na akina Gwajima wanajiamini sana..

Wanajua CCM hawana Ubavu wa kuwavua Uanachama kwa sababu hatua hiyo itamexpose Ndugai na kumtaka awavue Ubunge..

Itakuwa ni fedheha kubwa sana kwa Faru J kuwafukuza Ubunge akina Gwajiboy kwani atahojiwa wale Covid-19 wanafanya nini Bungeni hata baada ya kufukuzwa Chadema?

Ataulizwa akina Cecil Mwambe walirudije Bungeni baada ya kufukuzwa Chadema?

Mihimili hii miwili, Bunge chini ya Ndugai na Mahakama chini ya Ibrahim Juma kwa hakika IMENAJISIKA sana, kama ilivyo pia kwa Jeshi la Polisi

Kurudi kwa heshima ya taasisi hizo ni hadi wakuu wake hawa wenye uwezo mdogo waondolewe, hivyo tu

Polepole, Gwajima na wabunge wengine wowote wale hakika wako salama sana na mimi nawasihi wakaze kamba ili kama ni kutoka CCM watoke na mtu, Kama si Faru J basi Bi.Tozo mwenyewe
Haya majamaa hayafai .
 
Back
Top Bottom