Uchaguzi 2020 CCM huwa hawaangalii Mgombea Bora bali wanaangalia mtu atakeyeweza kushinda jimbo

Uchaguzi 2020 CCM huwa hawaangalii Mgombea Bora bali wanaangalia mtu atakeyeweza kushinda jimbo

Wapo watu walitarajia kuwa Wagombea wa mwaka huu watakuwa wa aina yake lakini cha kushangaza wamechomoza wale wale akina Msukuma, Lusinde, N.k.

CCM huwa hawaangalii mgombea bora bali wanachotaka ni mtu ambaye anaweza kushinda na kubakiza kiti Chao Cha Ubunge, haijalishi ni kilaza au la.
Wengine wana matusi sana mpaka wanaogopwa
 
Huku Tunduma tunahoji kwanini wamesumbua wajumbe?
Swali zuri sana kwa wenye kuelewa siasa za ukanda huo kuanzia Mbeya hadi ufike mpakani Tunduma. Tusubiri muda swali lako litapata majibu.
 
Na kwa taarifa yenu hao watu hapo October watakataliwa na CCM wenyewe. Upinzani wataenda kumalizia nyundo tu!
Kwa kuwarudisha kwa nguvu watu kama Gekul, Katambi na Silinde, CCM tayari wana mpango mkakati kuhakikisha hao watu watatangazwa. CHADEMA wakibweteka tu na kudhani ballot box pekee ndio itaamua mshindi, watapigwa vibaya sana.

Kumbukeni uchaguzi wa marudio Kinondoni. Wasimamizi kwenye vyumba vya kujumuisha kura walikuwa na option 2: either kusaini matokeo hewa kwa kupewa hela au kukataa na watu wengine kusaini kwa niaba yao.
 
Vyama vyote vya siasa vinaangalia watu wanaokubalika kwa wapiga kura hayo ya ubora ni TBS.
 
Back
Top Bottom