CCM ikiendelea kupuuza misingi ya uongozi ya Hayati Dkt. Magufuli, ni dhahiri watakosa kura 2025

CCM ikiendelea kupuuza misingi ya uongozi ya Hayati Dkt. Magufuli, ni dhahiri watakosa kura 2025

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Nawaonya CCM kwa mara ya kwanza kwamba, kupuuza na kutupilia mbali mtindo wa kuendesha nchi kwa alivyokuja nao hayati JPM, 2025 lazima iwagharimu

Ninao uhakika juu ya hili, endapo CCM Kitaendelea kupuuza yote mema, na misimamo thabiti ya namna alivyokuwa nayo kiongozi wa awamu iliyopita hayati JPM kwa kuitupilia mbali, 2025 siyo mbali, Historia itaenda kuandikwa upya na kwa mara ya kwanza, Tanzania itakuwa mikononi mwa msiowapenda!

Bibafs, kwa chama chochote kitakachokuja na slogani ya Magufulification kitapata kura yangu, na nitakuwa wa kwanza kufanya kampeni ili kumng'oa CCM, naamini stakuwa peke yangu, ni wimbi kubwa la Watanzania watakaounga mkono chama hiko

Ndiyo, Hayati JPM anayo makosa mengi, ila pia anayo mazuri mengi

Machache kati ya mengi mazuri aliyokuwa nayo,

# Hakupendelea nchi yetu iwe ombaomba

#Hakupendelea nchi yetu tujione wanyonge na kujiita sisi ni masikini, hakupenda kabisa tujivunie umasikini, kokote alikotembea alisema kwa ujasiri kuwa Tanzania sio masikini

# Alitupilia mbali na kukataa katakata miradi yote ya kinyonyaji kama mradi wa Nandari ya Bagamoyo

#Alielewa madhara ya kama kiongozi mkuu kukubali kuwa sasa tumeelemewa na Korona na tunahitaji misaada zaidi ya Msaada kutoka Kwa Mungu Hili nakili kuwa linaupinzani mkubwa kwa sababu kuna wanasayansi hudhani Mungu na sayansi ni kama vita vya tembo na nyasi licha ya hivyo huwa inaeleweka siku zote kuwa Mungu ni zaidi ya sayansi

#Aliwakemea wote wenye kutaka kuleta fyokofyoko bila kujali umaarufu wao, na ndiyo maana hatukushuhudia ujingaujinga wa shirika la Tanesko kukatakata umeme kama ilivyo sasa, misingi hii inapaswa isimamiwe kwa nguvu zote ili tutoke

Jambo lingine la kusisimua, JPM aliamini hasa ukiwa kiongozi unayesimama kwa ajili ya kutetea rasilimali za nchi, kifo huwa ni rafiki mkuu wa mtu huyo, Yeye hakujali
.
Tumpate wapi mtu kama huyu asiyeogopa chochote kwa ajili ya wengi?

Naam..! kwa maana hii, huu ndio unapaswa kuwa msingi wa nchi yetu, anayestahili haki apewe na mwenye kuvunja sheria bila kujali anacheyo gani naye awajibike

Uingozi, sio kumfurahisha kila mtu pia sio kumfedhehesha kila mtu
 
Mimi sijawahi kuwa CCM lakini ni muumini wa mapenzi mema kwa nchi yangu yeyote ataye kuwa tayari kuipiginia nchi yangu kama Magufuli huyo amebeba kura yangu pamoja na jamii yangu yote.

Except Lissu huyu anafaa kufungiwa jiwe la kusagia na kutupwa.
 
Kwahiyo unatakaje?

Wasitishe shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani ili CCM pekee waendelee kufanya siasa kama ilivyokuwa wakati wa Magufuli?
Wabambikie kesi viongozi wa upinzani?

Watafute ushindi kwa hila na mabavu dhidi ya upinzani kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019?
Watumie dola kubakia madarakani?

Zama zimebadirika mkuu.

Vumilia tu, maana hakuna namna.
 
Mimi sijawahi kuwa CCM lakini ni muumini wa mapenzi mema kwa nchi yangu yeyote ataye kuwa tayari kuipiginia nchi yangu kama Magufuli huyo amebeba kura yangu pamoja na jamii yangu yote.
Except Lisu huyu anafaa kufungiwa jiwe la kusagia na kutupwa
Mungu alivyowaajabu akamponya mshonwa risasi, halafu aliyekuaakilindwa kwa ulinzi usiomithirika ndio akatangulia mbele.

Tanzania ni yetu sote! Tupendane.
 
.... yeyote ataye kuwa tayari kuipiginia nchi yangu kama Magufuli huyo amebeba kura yangu.....except Lisu huyu anafaa kufungiwa jiwe la kusagia na kutupwa

tuwekee hapa makosa matano ya lissu aliyokukosea kiasi cha kutaka mwana wa mwenzio afungiwe jiwe la kusagia na kutupwa.

kama unamumia sana na utawala wa mama, nenda chato kalinde legacy kwenye kaburi la yule mshenzi labda kidogo itakupa faraja. vinginevyo kubali tu kuwa nyakati zimebadilika.
 
Bibafs, kwa chama chochote kitakachokuja na slogani ya Magufulification kitapata kura yangu
Mpo wangapi kwani?

Hivi Mngekuwa wengi mhusika angelazimika kushinda kwa wizi wa kura, kura za mabegi zilizopigwa tayari, gilba, utapeli, ulaghai, hila, utekaji, nk??!!!

Amini usiamini, Kwenye kampeni ukija na hiyo "slogan" utaangukia pua mapema asubuhi😊
 
Mpo wangapi kwani?
Hivi Mngekuwa wengi mhusika angelazimika kushinda kwa wizi wa kura, kura za mabegi zilizopigwa tayari, gilba, utapeli, hila, utekaji, nk??!!!

Amini usiamini, Kwenye kampeni ukija na hiyo "slogan" utaangukia pua mapema asubuhi😊
Kwa ushahidi upi? kama siyo kubwabwaja tu hapa
 
Mimi sijawahi kuwa CCM lakini ni muumini wa mapenzi mema kwa nchi yangu yeyote ataye kuwa tayari kuipiginia nchi yangu kama Magufuli huyo amebeba kura yangu pamoja na jamii yangu yote.
Except Lisu huyu anafaa kufungiwa jiwe la kusagia na kutupwa

Sentensi yako ya mwisho inaelezea roho yako kiuhalisia na hayo mapenzi kwa nchi unayoyataja ni hadaa! Mwenye upendo kamwe hawezi kumwombea mauti mtu asiyempenda.

Lissu ameipigania nchi hii na kuadhibiwa kwa maumivu kuliko wewe muumini wa maneno tu! Je kila unayemuona ni tofauti utamfungia jiwe na kumtupa? Unathibitisha kuwa Lissu ni mmoja wa survivors wa tabia yenu - kumbe kuna wengine mmewafanya hivi??!!
 
Nawaonya CCM kwa mara ya kwanza kwamba, kupuuza na kutupilia mbali mtindo wa kuendesha nchi kwa alivyokuja nao hayati JPM, 2025 lazima iwagharimu

Ninao uhakika juu ya hili, endapo CCM Kitaendelea kupuuza yote mema, na misimamo thabiti ya namna alivyokuwa nayo kiongozi wa awamu iliyopita hayati JPM kwa kuitupilia mbali, 2025 siyo mbali, Historia itaenda kuandikwa upya na kwa mara ya kwanza, Tanzania itakuwa mikononi mwa msiowapenda!

Bibafs, kwa chama chochote kitakachokuja na slogani ya Magufulification kitapata kura yangu, na nitakuwa wa kwanza kufanya kampeni ili kumng'oa CCM, naamini stakuwa peke yangu, ni wimbi kubwa la Watanzania watakaounga mkono chama hiko
Tutakuwa taifa la ajabu kuamini kwamba wewe ndo mwenye mawazo sahihi kuliko wengine. Yaani tuamini bila wewe na huyo mungu wako nchi haitaendelea? Ni miezi 3 tangu ameondoka duniani, umeona upungufu wowote wa kutokuwepo kwake? Nyie mmepoteza nafasi alizowapa kwa upendeleo, kwa hiyo mnajaribu kutisha watu ili waone bila kundi lenu nchi haiendi.
Bashiru,
Makonda,
Mnyeti,
Dotto,
Nk
Hawako kwenye system, lakini umeona system imecolapse?
Acheni majungu wakati si rafiki kwenu. Aidha mjirudi twende pamoja, au nendeni peke yenu mpotee daima.
 
Back
Top Bottom