kulagha nenga
JF-Expert Member
- Jan 1, 2026
- 690
- 1,375
Wadau habari zenu,
Mimi sio mwanasiasa LAKINI naipenda nchi yangu na viongozi wake , nawapenda pia viongozi au wanasiasa wa upinzani ambao wana misimamo sio njaanjaa na ni wazalendo wanaowajibika kwa wananchi. Sio uzalendo wa kinafiki wa kuwasifia viongozi wakuu hata kama hawafanyi vizuri eti ili TU upate chochote au mambo yako yanyooke
Niende kwenye mada sasa,
Kiukweli CCM imepoteza sifa yake ya asili ya kuwa chama cha kutetea maslahi ya wakulima na wafanyakazi.
Kwasasa CCM inaonekana kutumiwa na kundi fulani la la viongozi au wafanyabishara kwa maslahi yao binafsi sio ya nchi na wananchi.
Wananchi wengi wanalalamka juu ya :-
Chaguzi zisizo na matokeo ya ukweli. Wanaopitishwa na kutangazwa sio chaguo la wananchi. Siku hizi watu wengi hawashiriki uchaguzi kwasababu wanaamini sauti zao hazita sikilizwa
Hakuna sauti ya kukemea maovu kama vile rushwa ubadhirifu ufisadi, utekaji au kuuwawa kwa watu, kukabali makosa na kuwachukulia hatua wahusika
Polisi kuvunja sheria mfano kuwashikilia watu Kwa muda mrefu bila kuwepeleka mahakamani mpaka jaji mkuu analalamika. Yaani ofisi ya mashitaka inaweza kukupa shitaka la ugaidi hata kama kosa lako ni kuiba kijiko inaongeza chuki kwa chama na serikali
Hakuna jitihada za wazi zinazoonesha kuwa serikali
inapambana na rushwa na ufisadi unaozidi kutamalaki.
Hakuna uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwenye ofisi au Taasisi za selikali/za umma .licha ya malalamiko ya wananchi.
.
Suluhisho.
lazima wakubali kuachana nabaadhi ya viongozi mizigo na mafisadi. Wanafiki wanaosifia mchana usiku wanakunanga
Kuteua safu ya viongozi vijana, wasafi kimaadili wasio waoga kukemea na kusema ukweli. Wasiokuwa chawa
Kukiimalisha kitengo cha uenezi na propganda ili kiweze kujibu hoja za wapinzani na kueleza nini serikali inafanya
Jeshi la polisi lisitumike kama chombo cha kusaidia CCM wananchi wengi wanamtazamo hasi na chombo hicho
Kudhibiti rushwa na ufisadi kwakuchukua hatua sahihi
Vyombo vya kusimamia sheria polisi na mahakama vifanye kazi kwa mujibu wa Sheria na sio maagizo na maelekezo
Kusikiliza kero za wananchi na kizitafutia ufumbuzi .
Hayo ni baadhi ya maswala ambayo naamini yakifanyiwa kazi yatarudisha imani ya wananchi Kwa serikali na Chama