CCM ilihusika kifo cha Wangwe?

CCM ilihusika kifo cha Wangwe?

Sina mahusiano makubwa na siasa za CCM ila nimehakikishiwa kipande hiki kweli kimetokea. Cha ajabu ni kwamba maslahi ya Wananchi na kuliweka Taifa kwanza zinaitwa ni sera za Upinzani... Hapo mishipa ya akili imesimama, sijui niseme nini kuhusiana na CCM..

Ndio maana kila ninaposoma post za wateteaji ufisadi humu ndani kama anayejiita mkamap na wenzake, nazidi kupandishwa mori. Kelele na kejeli zao dhidi ya upinzani ndizo zinazidi kuchochea mwamko wa wananchi kutaka kutimua hili genge la wahuni (CCM) madarakani. Hivyo nawaomba waendeleze juhudi zao hizo za kubariki dhuluma kwa kuwa wanazidi kupalia mkaa wa moto hasira za wananchi. Kwa hilo nawapa pongezi Ladslaus na mkamap na wanaowaunga mkono.
 
Wewe ni dikteta wa fikra
Na dikteta wa namna hii ni mbaya kupindukia afadhali yule dikteta wa ki maumbo
 
Wewe ni dikteta wa fikra
Na dikteta wa namna hii ni mbaya kupindukia afadhali yule dikteta wa ki maumbo

Bado nakumbuka ulivyomtetea Mkapa bila kuyumba pamoja na hoja zote zilizotolewa humu ndani. Msimamo wako kweli ni wa kuigwa - maji ukiyavulia nguo bidi uyakoge. Kinachonitatanisha ni kukuelewa unasukmwa na nini, nani na kwa mantiki gani. Hizo zako ni mbinu kama za McCain dhidi ya Obama lakini yeye anasukumwa na ubaguzi, je wewe ?
 
Mimi nasukumwa na nia njema na wewe je? Hivi kile kimemo mlichofoji ITV kimefikia wapi?
 
Mkamap,
Huwezi sema chadema ama SLAA ama ZITTO ndio kaanzisha hii move nenda nyuma kidogo uone nani alisababisha IDD SIMBA kujiuzulu,nani alisababisha Mbilinyi kama sikosei waziri wa fedha kujiuzulu na kwa sababu zipi?
Mkuu CCM ile unayozungmzia sio hii ya leo na kama mambo haya yangetokea wakati ule, tusingesubiri kina Dr. Slaa na Zitto. Huwezi kuitumia CCM ya mwalimu kutolea mifano ya Uongozi ambapo asilimia kubwa ya wachezaji wamekaa bench!..Ni sawa na kufananisha Yanga ya kina Sunday Manara na hii ya leo..
Hata hivyo kina Idd Simba ulikuwa mchezo wa KULA ndani ya chama. Idd Simba alikuwa akijipanga kutafuta kura ndani na nje ya CCM ili kujiandaa na uchaguzi wa 2005. He did nothing wrong kiuchumi...
Mbinu ya sukari ilitumika kumwondoa kwani aliyeshiriki ktk mchezo mzima alikuwa mtu wa Rostam Aziz..kwa hiyo tunarudi nyuma tena kuwa hawa Mafisadi hawakuanza jana. Walianza ndani ya chama kiasi kwamba kina Dr. Slaa hawakuweza kuwaona hadi pale walipoanza kuonyesha makucha yao kitaifa..
 
ok mkuu maana naona umeshasema IDD

Harafu mkuu tatizo la wengi hamnielewi namaanisha nini hilo ni tatioz kubwa kwa sababu akili watu wameshazi fix nikiisema chadema basi mimi ni mtetezi wa mafisadi.

Elewa hapa ninachosema post na post ndiyo naongelea wale sijui akina kingunge ama mzee dekayaa walijipatia umarufuu bungeni kwa sababu ya kulipua mabomu ya wenzao bungeni umeipata point?
UMAARUFU!!! na si kwamba walifanya hivyo kwa ajili ya kutetea wananchi ni UMARUFU wa kisiasa ndio uliowasu(Tusi)(Tusi)(Tusi)(Tusi).

Na ukiangalia LIWAYA ya chadema u aproach hilo tatizo logically utagunduwa tu wanachotafuta ni UMAARUFU kisiasa umenipata? Na ndio maana anayeleta mizengwe ktk kuusaka umaarufu wao hawakawii kumwiita FISADI ama ANATUMIWA na MAFISADI.

Tumeona wanaotumiwa na mafisadi akina Kabouru,chacha,mtikila,mrema,mbatia,mziray na wengine wengiiiiiiiiiiiiiiiiiiii humu jf.

ALAMSKI
 
ni nani alimuua chacha wangwe? kama kuna mkono wa mtu/watu hili halitajificha juu ya ardhi na mbingu! kwa kuwa imeandikwa kuwa damu ya abel nduguye itakulilia kila siku, na kamwe nitakuweka alama ili mtu asikuue!
 
hizi ni cheche,baada ya muda utakuwa moto,watu wengine hawajiulizi wala kutafakari haya maneno yalio wakilishwa na mkuu hapa jamvini matokeo yake wanaanza kutoa vimaneno.
Nilivyosoma hapa nikaona kuwa hii move ndo imeanza we go,tutafika maana mambo ya laptop nayo kwangu ni mapya.
kama hauna lakuchangia jikalie kimya kuliko kumkatisha tamaa mwandishi wetu.
 
ni nani alimuua chacha wangwe? kama kuna mkono wa mtu/watu hili halitajificha juu ya ardhi na mbingu! kwa kuwa imeandikwa kuwa damu ya abel nduguye itakulilia kila siku, na kamwe nitakuweka alama ili mtu asikuue!
Najitambulisha tena kuwa mimi sio mwanachama wa chama chochote bali mwananchi wa kawaida.
Marehemu Chacha Wangwe alifariki kwa ajali ya gari jamani. Naomba muamini hivyo. Ile ni kazi ya Mungu.
Tatizo ni kuwa kwa vile alikuwa ni mmoja wa wabunge changamoto, wafuasi wake bado wanaweweseka na mzimu wake hivyo kuendelea kumtafuta mchawi.
Hili la kuihusisha CCM ama Chadema na kifo cha Wangwe,ni lengo la kupanda mbegu ya chuki kwa kuwaaminisha watu damu imeshamwagika hivyo wawe tayari kumwaga damu kwa ajili ya kile wanachoamini.
Wanaojua kusoma dalili za nyakati katika medani za siasa tayari wameshasoma mwelekeo wa kitakachotokea 2010 kinaonekana wazi hakuna sababu ya kuendelea kuchafuana kwa kisingizio cha kifo cha Wangwe wala siamini laptop yake iko kwa Makamba. Makamba na laptop wapi na wapi?!.
Tujadili siasa sio kupanda mbegu za chuki. Nyerere angekuwepo angesema "Huu ni upuuzi mtupu!.
Namalizia kwa kusema 'japo siasa ni mchezo mchafu lakini sio kihivyo!'.
 
Bado nakumbuka ulivyomtetea Mkapa bila kuyumba pamoja na hoja zote zilizotolewa humu ndani. Msimamo wako kweli ni wa kuigwa - maji ukiyavulia nguo bidi uyakoge. Kinachonitatanisha ni kukuelewa unasukmwa na nini, nani na kwa mantiki gani. Hizo zako ni mbinu kama za McCain dhidi ya Obama lakini yeye anasukumwa na ubaguzi, je wewe ?

Huwezi juwa jamaa alipa fadhira aliyotendewa hata kama jamaa ana makosa vp lazima amtetee ndiye aliye mwezesha kuwepo mjini ni mkubwa wake.....
 
Mwenye ushahidi proved beyond doubt kuhusu kifo cha Chacha Wangwe na alete hapa. Naona watu tunachangia tu kila mtu na mawazo yake na ambayo hayana proof yoyote. Kama tulivyoanika siri za mafisadi hapa, mihela yao na vitega uchumi hasa vile vya EPA basi na proof ya kifo cha Chacha Wangwe ipostie hapa. Badili hata anonymity yako upost hapa ili tuchangie.

Na yule aliyechangia eti kulikuwa na fax a day before the tragedy then aipost hapa ili kukata mzizi wa fitina.

Vinginevyo tunabaki ku attack vyama, watu etc. Tuwe na uchangiaji yakinifu. Nawasilisha wakuu.
 
Wewe ni dikteta wa fikra
Na dikteta wa namna hii ni mbaya kupindukia afadhali yule dikteta wa ki maumbo

Mtu kukemea, kuchuki, kuongelea usifadi na wanaokula pesa zetu na wanaosapoti sio dikteta unless sijui maana ya udikteta
 
Hivi si imeshadaiwa hadharani kuwa waliomuua Chacha ni Chadema? Polisi hawajasikia? Wamefanya nini? Pia inadaiwa hapa kuwa CCM ina mkonio kwenye kifo cha wangwe, Polisi wanafanya nini?
Walichofanya Polisi ni kufanya uchunguzi baada ya kifo cha wangwe na kufungua kesi. Aliyeshtakiwa ni nani, Deus Mallya, si Chadema wala CCM.
Kwa mujibu wa kesi iliyopo polisi, kifo cha Chacha weangwe kilisababishwa na mwendo kasi wa gari lililokuwa linaendeshwa na Desu Mallya.
Mpaka hapo wachunguzi wa Polisi watakapotuletea taarifa nyingine, hivi sasa habari ndiyo hiyo.
 
"MAKAMBA AKIBANWA ATAELEZA ALIKOIPATA MKOBA NA LAPTOP YA MAREHEMU CHACHA WANGWE ILIYOPOTEA SIKU YA TUKIO"
Ina maana huyu jamaa alikutwa nayo kweli ama.
Saa ingine kuka kijijini ni mbaya sana. Nisameheni siko updated sana.
 
1-Hivi nani alikuwa mtu wa mwisho kuzungumza na Wangwe pale Dodoma?
2-Hivi baada ya Chadema kumvua Umakamu, kifo cha Wangwe kilikua na athari gani kwa Chadema?
3-Je, CCM hawana "majasusi" wa kujua kwamba watu wanapogombana mmoja akivamiwa na majambazi, mtuhumiwa wa kwanza ni waliyegombana naye?
4-Hivi CCM walijiandaa ama hawakujiandaa katika kuhakikisha kifo cha Wangwe kinatumika kukibomoa Chadema?
5-Je, si ni kweli Chadema walishitukizwa katika propaganda kabla ya kuzinduka na kuanza kujipanga na kushinda uchaguz?

Kimsingi kukiwapo uchunguzi huru wahusika watatakiwa kutoa maelezo ya kwa mfano ilikuwaje CCM wakawa wamejiandaa na propaganda za kifo cha Wangwe hata kabla ya kifo chake, wachunguzi huru wanapaswa kuanza kuangalia mawasiliano na vikao vya mikakati.

Hapo watapata picha nani alijua kifo cha wangwe hata kabla ya kutokea na hapo wanaweza kujitetea kwamba waliambiwa na "Sheikh Yahaya" na hivyo kesi inafungwa na kuendelea na ile ya Deus Mallya kuendesha gari vibaya, vinginevyo mambo mazito yataibuka.
 
Halisi need no to say more!
 
Sishangai wanaotetea ufisadi/mafisadi maana kula yao inatokana na UFISADI.
Mafisadi wote muarobaini wenu unachemka jikoni so its a matter of time tu.
 
Back
Top Bottom