PreGE2025 CCM ilipaswa kulinda Demokrasia ya kuchagua na kuchaguana ndani ya chama badala ya hivi ilivyofanyika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Joined
Apr 8, 2023
Posts
43
Reaction score
29
Hizi ni salaam zangu kwa Katibu Mkuu wa CCM (ambaye kimsingi ndiye Mratibu Mkuu wa shughuli za chama. Pamoja na kwamba binafsi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa, ni muumini wa siasa za Tanzania kwa utanzania wangu na shabiki wa CCM kwa sababu kadha ambazo nitazieleza siku nyingine, leo niruhusu nakuomba nikuandikie maoni yangu ambayo ninadhani sitakuwa nimejitendea haki nisipoyasema. KWA CCM KUPITISHA MGOMBEA URAIS BILA KUMSHINDANISHA NA WENGINE, TUMEKWISHAPOKWA HAKI YETU YA KUCHAGUA HATA TUKISHIRIKI UCHAGUZI.

Hoja yangu inajengwa kwenye msingi kwamba kwa mujibu wa sheria na Katiba zote mbili yaani ile ya CCM na Katiba ya Jamhuri yetu, ingawa tunaye Rais halali kabisa (na hivyo tunawajibika kumtii), lakini si Rais aliyechaguliwa na Wananchi kuwa Rais wao. Ni Rais ambaye amechukua jukumu la kuingoza Tanzania kwa mujibu wa Katiba baada ya kufariki Rais aliyechaguliwa na Wananchi. Hata ndani ya chama, Rais wetu wa sasa "aliteuliwa" na mgombea kuwa "mgombea mwenza" na hivyo yeye binafsi hakuchukua fomu, kupiga kampeni na kuwaomba wanachama ama Wananchi kwa ujumla wao kuwa Rais wao. Huu ni uhalisi (Fact).

Sasa, bila kujali msingi wa hoja hapo juu, Rais huyu bado amefanya kazi nzuri na yenye kutukuka katika mengi aliyoyafanikisha chini ya uongozi wake, ni pamoja na kuhakikisha kwamba taifa limepita kwenye kipindi tete cha kisiasa baada ya kufa Kiongozi Mkuu wa taifa akiwa madarakani, jambo ambalo yeyote mwenye akili njema anafahamu lingekuwa limetokea nchi yoyote jirani yetu hapa Afrika Mashariki na hata Afrika nzima, tungeshuhudia mapigano na umwagaji damu, sisi tumevuka salama. Hii itabakia kuwa sehemu muhimu ya 'legacy' ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye vitabu vya historia kwa miaka mingi.

Soma Pia: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Hata hivyo, uamuzi wa CCM kupitisha jina la Rais Samia kama mgombea wake bila kupitia utaratibu wa kawaida wa kupigiwa kura kwa kushindanishwa na wagombea wengine kama ilivyotokea, siyo tu umevunja kanuni kadhaa za CCM, lakini umetengeneza precedence mbaya katika chama, kwamba wakati wowote kwa sababu zozote tunaweza tukaamua to manipulate utaratibu na hata sheria, kanuni, taratibu na hata Katiba ya CCM kufikia malengo tutakayo bila kujali ikiwa maoni ya wengi (Demokrasia) yamezingatiwa ama lah! Ni nini basi kitafanya baada ya 2030 tusikutane tena na kuamua kwamba tunaongeza mihula ya Urais na kadhalika na ikawa!!? Na je! Ikiwa hivyo utamaduni wa kuheshimu sheria na Katiba ndani na nje ya chama utakuwaje!!? Na mwisho tutatengeneza chama na taifa la namna gani!!?

Sawa, tuseme chama ni cha "wanachama" kama tusemavyo siku zote "CCM ina wenyewe...", lakini ikiwa siku moja kwa nasibu ama kwa sababu yoyote Mheshimiwa Samia atasimana mahala na kusema "Binafsi sikuwahi kugombea nafasi ya Urais na sikuomba kwa chama changu kupepea bendera ya chama kwenye uchaguzi, niliteuliwa tu...." atakuwa anadanganya!!? Wana CCM wana uhakika kwamba anataka kweli kuwa Rais wao na Rais wa taifa lao bila kushawishiwa na bila kushurutishwa kwa namna yoyote!? Kama ndiyo, kuna shida gani kuchukua njia iliyoelekezwa na taratibu za Chama kwenye kumpata mgombea wake kwa kupigiwa kura badala ya kuteuliwa!!?

Kuna pia hoja kwamba kwanini tumeamua kwamba hatutaki kumshindanisha na watia nia wengine!!? Yeye anayo kazi yake mkononi mwake, anao uzoefu, amejifunza mengi katika kipindi cha miaka hii mitano ya kuwa Rais na ametengeneza maono yake ya jinsi ya kufanikisha ilani na ahadi za CCM kwa taifa, kwanini hatutaki kusikia na kuona kama kuna maoni bora zaidi, ama kama wana CCM kwa wingi wao wanaridhika!!? Yawezekana wasioridhika ni wengi na tunadhani kwamba akishindanishwa atapata ushindi kidogo au asipate kabisa!? Hofu yetu nini!!?

Katika wakati ambapo siasa za ushindani nchini ziko hoi bin taabani kwa vyama vingine vyote kukosa mwelekeo, CCM haioni umuhimu wa kulinda misingi ya Demokrasia kwa kuruhusu mchakato wa ndani badala ya hivi ambapo upinzani umedorora na sasa CCM haitaki kushindanisha fikra na maono ya wanachama wake kuibua maono na mipango kugombea badala ya mtu!!?

Nachelea pia kwamba maamuzi hayo ya chama, yanazipa mashiko na uhalali hoja za wapinzani kwamba hata Katiba ya nchi ilivyo sasa (hata bila mabadiliko) haiheshimiwi isipokuwa tunafanya na kuamua tutakavyo mradi tu tunafikia malengo ya wachache. Kama tunafanya maamuzi kwa ya kupata Rais kwa urahisi tu namna hii, tutaaminikaje kwamba tunaheshimu mguso wa mchakato mzima wa uchaguzi na hivyo uchaguzi kuweza kuitwa hasa Uchaguzi!!?

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sina maneno ya kuelezea vya kutosha ukweli kwamba sina jambo lolote kinyume na Mheshimiwa Samia binafsi, lakini nina hoja kwamba CCM ilipaswa kulinda Demokrasia ya kuchagua na kuchaguana ndani ya chama badala ya hivi ilivyofanyika, na kwamba haya ni maoni yangu binafsi. Kwa msingi huo, binafsi naona kama nimepokwa uhuru wangu wa kuchagua na hivyo ingawa kama Mtanzania mzalendo, mchambuzi na mtu walau mwenye kufikiri nitashiriki uchaguzi (hata kwa kusikia tu kuhusu uchaguzi) lakini sitapiga kura, kwa sababu uchaguzi ilipaswa kuanzia ndani ya chama na ndani ya chama haujafanyika kumefanyika uteuzi. Sote tunafahamu kwamba hakuna chama cha siasa kingine Tanzania chenye uwezo, mifumo na rasilimali watu kushika nchi na kuendesha Serikali kwa sasa nje ya CCM na hivyo uchaguzi ndani ya CCM ndiyo hasa "Uchaguzi Mkuu" na kama haujafanyika, basi ingawa tufanya uchaguzi, kimantiki hatutafanya "Uchaguzi Mkuu".

Wasalaam!
 
Akifa Samia kwa mfano Je na Nchimbi nae si atakuwa Rais kwa vipindi viwili kwa kujipitisha? Precedence sio kitu cha mchezo mchezo
 
Gentleman,
CCM wamefanya maamuzi yao kulingana na taratibu zao za kikatiba na kuamua namna ya kumpata mpeperusha bendera wa chama chao katika uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2025.

sasa wewe,
umepokwaje haki yako na CCM hali ya kua umedai wazi wazi kwamba wewe si muumini wa chama chochote cha siasa humu nchini?

unalenga kumpotosha nani gentleman? Sijapenda kabisa hii 🐒
 
CCM imevunja Katiba yake. Ila mlizoea kupora kura za wapinzani Leo mnaporana wenyewe kwa wenyewe!
 
huna haja ya kubabaika na mambo usiyoyajua na yasiyokuhusu hususani ya ndani ya vyama vya siasa,

na ikiwa una husika na una ushahidi, nenda mahakamani gentleman kuliko kumbwelambwela tu humu jukwaani na dhana potofu iliyo athiri fikra zako kwamba umeporwa kitu usichokua nacho kama vile mtoa hoja 🐒
 
Gentleman,
huna haja ya kubabaika na mambo usiyoyajua na yasiyokuhusu hususani ya ndani ya vyama vya siasa.
CCM imevunja Katiba yake. Tabia ya kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania iliwakolea leo mmevunja ya kwenye mnataka kuleta zogo.

CCM imevunja Katiba yake!
 
sasa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeingiaje CCM gentleman?

halafu kulikoni CCM inafanya mambo yake chadema na vyama vingine huweweseka?🤣

Kumbe waTanzania wa vyama vyote vya siasa nchini hufahamu wazi kwamba uchaguzi ndani ya CCM ukikamilika, basi uchaguzi mkuu ni kukamilisha takwa na ratiba za kikatiba tu, right?🤣
 
Gentleman,
CCM wamefanya maamuzi yao kulingana na taratibu zao za kikatiba na kuamua namna ya kumpata mpeperusha bendera wa chama chao katika uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2025.

sasa wewe,
umepokwaje haki yako na CCM hali ya kua umedai wazi wazi kwamba wewe si muumini wa chama chochote cha siasa humu nchini?

unalenga kumpotosha nani gentleman? Sijapenda kabisa hii 🐒
Umesomaje nilichoandika!!? Unafahamu tofauti ya kuwa Mwanachama, Shabiki na Muumini!!?

Kupotosha ni kufanyaje walau kwa tafsiri yako!!? Hujapenda!!? Kusema kweli sitarajii ninachoandikwa kupendwa na kila anayesoma na hivyo wewe ni sehemu ya ambao hawajapenda, nilitarajia wawepo wasiopenda
 
Pamoja na kwamba binafsi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa, ni muumini wa siasa za Tanzania kwa utanzania wangu na shabiki wa CCM kwa sababu kadha ambazo nitazieleza siku nyingine, leo niruhusu nakuomba nikuandikie maoni yangu ambayo ninadhani sitakuwa nimejitendea haki nisipoyasema
Nimeishia hapa. Najua huko mbele ni utoporo tu
 
Umesomaje nilichoandika!!? Unafahamu tofauti ya kuwa Mwanachama, Shabiki na Muumini!!?

Kupotosha ni kufanyaje walau kwa tafsiri yako!!? Hujapenda!!? Kusema kweli sitarajii ninachoandikwa kupendwa na kila anayesoma na hivyo wewe ni sehemu ya ambao hawajapenda, nilitarajia wawepo wasiopenda
sijapenda kabisa upotoshaji gentleman, na kwakweli siwezi kuvumi jambo kama hilo,

yaani udai kwamba hufungamani na chama chochote cha siasa, halafu hapo hapo useme CCM imepora haki yako, hiyo si sawa ni upotoshaji gentleman 🐒
 
Kama sisiemu hawataki vyama vingine vifanye siasa basi kwakuwa wapo wengi wapeleke bill bungeni ya kufuta vyama vya upinzani wajibakize wao tu ili tuokoe fedha zinazoenda kutumika kwenye UCHAFUZI.
 
Kwa hiyo ulitaka apitishwe kwenye chujio la ushindani ili akwame Kama machicha ya Nazi sio.
 
sijapenda kabisa upotoshaji gentleman, na kwakweli siwezi kuvumi jambo kama hilo,

yaani udai kwamba hufungamani na chama chochote cha siasa, halafu hapo hapo useme CCM imepora haki yako, hiyo si sawa ni upotoshaji gentleman 🐒
Mradi sijatukana na wewe hujatukana, naheshimu maoni yako. Kwamba umependa au hujapenda, pia huo ni uchaguzi wako kama ambavyo nimechagua kutojali ikiwa umependa au hujapenda mawazo yangu.
 
mawazo ni mazuri mno gentleman,
changamoto iliyopo ni element za upotoshaji,

ni wazi,
tone ya uandishi wako inatambulisha mrengo wa chama cha siasa ulipo

but kiujumla,
andiko lako ni zuri lenye pure political contents 🐒
 
Sema chama kimejaa chawa na waimba pambio, viongozi wao hata wawafanyie nini wao watashangilia.

Mgombea Urais na Umakamo Urais wa CCM ni BATILI!
kwani gentleman,
unadhani mihemko na makasiriko ya wasio wana CCM dhidi ya CCM yana athari zozote kisiasa kijamii au kiuchumi ?

ni useless and completely nonsense ndio maana chama kipo bize kujiandaa na ushindi wa kishindo October mwaka huu 2025🐒
 
Back
Top Bottom