Uchaguzi 2020 CCM imechokwa na Watanzania tuache utani kabisa

Jamani tusichaguliwe Rais ambaye hata debate hawezi, haya ni maisha yetu na nchi ni yetu sote. Yaani sasa hivi kuna watu wanatuchagulia Rais kama wanavyoona wao na familia zao halafu wanatumia jeshi na polisi kunyanyasa. Tangu leo tukatae.

Tukichagua wenyewe tukiliwa tuliwe. Lakini vilevile tukimchangua wenyewe tunaweza kumwondoa madarakani. Kiongozi anayewekwa na Polisi na Jeshi huwezi kumondoa kwa kuwa hawezi kufanya kitu chema kwa wananchi, yeye hutegemea nguvu tu.
 

Labda wewe ndo hujajiandikisha! Hivi unajua kitambulisho cha kura ndio kilikuwa cha muhimu kabla ya cha Taifa, kila aliyestahili alikihitaji.
 
Ccm haiwezi kutoboa hata kwa dawa ...vijana kuanzia 18-30 ambao ndo idadi kubwa ya wapiga kura wote wako Chadema , sasa ccm wanatoboaje?...
Ukiona mtu anapinga sana Rais aliyepo na kazi nzuri anayofanya kuna jambo,either alikua ana vyeti feki ,mfanyakaz hewa,ndugu yake amekumbwa na kadhia hiyo,Mkopo bodi ya mikopo,na vitu kama hivyo.
 
Tumchague mtu ambaye anatumia mda mdogo kuelezea ukweli na tumkatae mtu ambaye anatumia nguvu nyingi kuelezea ukweli.
 
Sawa wanaweza wakawa wanaikubali chadema Ila unadhani vijana katika umri uliotajwa wana mwamko wa kupiga kura Kama wazee wa CCM
 
Umeongea ukweli mkubwa sana ndugu!!! Hivi naachaje kumchagua Lissu wakati ana Sera ya kumsomesha hata mwanangu ambaye nimemsomesha private?

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambae anarudisha makato ya mikopo ya bodi ya mikopo kutoka asilimia 15 ya magufuli hadi asilimia 6?

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambaye ametoa Sera ya kunijali mimi mlipa kodi na mfanyabiashara kwa kuniwekea mswada wa kunilinda mimi mlipa kodi ili TRA wasininyanyase?

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu ambaye hataniwekea mipaka kwenye masoko ya kuuza mazao yangu niliyoyalima kwa jasho kubwa?

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu mwenye Sera ya kurudisha katiba mpya ya warioba itakayoweka misingi ya utawala bora na kuondoa matumizi mabaya ya madaraka?
 
Kila mahali imekataliwa
 
16 September 2020

Tundu Lissu, Nyomi lake lahamia Mara, Polisi wasindikiza kwamzuka wa mdundo.!!

Wananchi wa mkoa wa Mara wakisindikiza wabunge wao na wimbo mtamu maarufu :Mdogo mdogo tupo bungeni, mdogo tupo bungeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…