CCM imedumaza uwezo wetu wa kufikiri, hadi wanaofikiri sawasawa wameanza kuchukiwa

CCM imedumaza uwezo wetu wa kufikiri, hadi wanaofikiri sawasawa wameanza kuchukiwa

Baada ya Mapinduzi (matukufu?) ya Zanzibar Mwaka 1964, chama cha ASP kikapiga marufuku vyama vingine vya siasa na kuharamisha viongozi wake. Ukiwa Zanzibar ilikuwa ama uwe ASP au uwe adui wa Mapinduzi. Kwa ivo kila mtu aliyetaka kufanya siasa Zanzibar ilibidi ajiunge na ASP ili afanye siasa na awe salama. Hapa kuna kumbukizi ya utata kwa watu kama Kina Kassim Hanga walikufaje na Salim Ahmed Salim ambaye ililazimika apewe Ubalozi wa Tanzania ili kumnusuru na hisia dhidi yake kwamba yeye ni Hizbu.

Tanganyika nako baada ya uchaguzi wa vyama vingi Mwaka 1965, TANU ilipiga marufuku vyama vingine vya siasa na kubakia peke yake. Hapo napo ndiyo kwenye ile misukosuko iliyowapata kina Abdalah Fundikira na baadhi ya wenzake. Kulikuwa kuna kundi kubwa sana ndani ya TANU ambalo lilikuwa halikubaliani na TANU lakini kwa kuwa vyama vingine vilikuwa vimepigwa marufuku, kundi hilo la watu ilibidi kuvumilia kubaki TANU.

TANU na ASP ziliunganisha nchi ya Tanganyika na Zanzibar lakini ilishindikana kuunganisha vyama vyao mpaka miaka 13 baadae walipoiunganisha ASP na TANU na kuzaliwa chama cha Mapinduzi-CCM. CCM ilirithi tabia ya TANU na ASP ya kutokutaka mawazo tofauti na wao. Na hapo ndipo walipoanzisha falsafa ya chama kushika hatamu.

Chama kushika hatamu ulikuwa ni mfumo kwa wananchi kutii bila ya kuuliza chochote dhidi ya mambo yote yanayotendwa na kuamuliwa na viongozi. Hali hiyo ndiyo imedumaza uwezo wetu watanzania kwenye kutumia akili zetu kujenga hoja.

Mtanzania anaweza kuwa na maneno meeengi lakini inakuwa taabu kwa msikilizaji au msomaji kujua msemaji anataka kusema nini. Kwa kweli watanzania wengi wamedumazwa uwezo wao wa kutumia akili zao kwenye kufikiri na kujenga hoja.

Kujenga hoja kunahitaji mantiki na mantiki haiwezi kujengwa na watu wasiotumia mbongo zao kufikiri kwa uhuru. Leo hii wanaofikiri kwa uhuru wameanza kuchukiwa kama ni maadui kwa kuwa eti ni kwa nini wao wanafikiri tofauti na viongozi, Ndipo ule msemo wa " Wewe unajua zaidi kuliko kiongozi" unapoibuka.

Tupo sehemu mbaya sana kama taifa. Hatuwezi kupiga hatua nzuri ya kimaendeleo kama hatutoruhusu mbongo zetu kufanya kazi kwa uhuru na kwa tafakuri jadidi. Matokeo yake mtu ana shahada tatu anafukuzwa ukuu wa Mkoa anaanza kutubu kama mwendawazimu mbele ya Kamera. Au ni sawa na Professa ambaye kwa hofu anamwita Rais "Mheshimiwa Mungu".
Kabisa!
 
Niambie chama mbadala baada ya CCM kuwa nje?

Jibu swali sio una QUOTE nusu nusu

Siku zote kwenye kutafuta majawabu lazima tuwe suluhisho, je chama kipi kitakuwa suluhisho? CUF ya Lipumba, ACT ya Zitto au CDM ya Mbowe?
Wewe ubovu wa CCM unauhamishia kwa vyama vingine kwamba vyenyewe ndiyo chanzo cha CCM kutobadilika. Kwa ivo CCM hawana mpango wa kubadilika??
 
Wewe ubovu wa CCM unahamishia kwa vyama vingine kwamba vyenyewe ndiyo chanzo cha CCM kutobadilika. Kwa ivo CCM hawana mpango wa kubadilika??
Sawa CCM imeshakuwa mbovu ilo lipo wazi.

Twende kwenye suluhisho mkuu.
 
Hayo matakataka yote kwisha kazi. Aggrey Mwanri, Kabudi, Kangi Lugora na Sheikh Alhad walijidhalilisha sana kwa kumfananisha Magufuli na mungu
Ilikua mihemuko tu,wanajisahau Sana,wanasahau Sauli alipigwa chango la tumbo baada ya watu wake kumwambia sauti yako Kama ya MUNGU,walifikia kusema edo angefia madarakani [emoji24][emoji24][emoji24]
 
CCM inatakiwa usiongozwe na akili. Muhimu ujue kua mnafiki na mchumia tumbo
Fuatilia watu ulosoma nao shule wale mambumbumbu walokuwa wanapata maksi 5 kushuka chini ndio huwa wapo ccm na ndio wanatetea chama, yan imekuja kuonekana kwamba kugombea kitu chochote ukiwa sisiem ni rahis kushinda sababu wataiba kura sasa hapo ndio utajua we are recruiting wezi, vilaza na majitu yenye tamaa... Tulishasema haya watu wakawa hawaelewi... Sijui raia wameanza kuelewa... Huwa najiuliza sana why watu makengemaji, matahira, hawajui kujenga hoja wala kutengeneza hata a single line sentence wote wapo ccm NAKASIRIKAGA SANA ona hii list ya matahira
1.wema sepetu
2. Wolper
3.stiv nyerere
4.ray kigosi
5.mwinjaku(huyu choko kabisa)
6. Sufian juma(choko lingine)
7.juma lokole
8.nabii tito choko mzoefu.
Yako mengi nachoka kuandika na usije ukashangaa siku moja yamekuwa viongozi alafu yameolewa na wanaume wenzao, hii nchi inaenda wapii?
 
Niambie chama mbadala baada ya CCM kuwa nje?

Jibu swali sio una QUOTE nusu nusu

Siku zote kwenye kutafuta majawabu lazima tuwe suluhisho, je chama kipi kitakuwa suluhisho? CUF ya Lipumba, ACT ya Zitto au CDM ya Mbowe?
Hakuna chama mbadala wa ccm wakati huu!! They have rendered themselves irrelevant!
 
Sawa CCM imeshakuwa mbovu ilo lipo wazi.

Twende kwenye suluhisho mkuu.
Suluhisho linaweza likawa la namna hii. Ukiwa na gari moja, na watoto wa wanne. Mmoja wa watoto hao akiwa amekua dereva wa gari hilo tangu ulinunue, na amekua akiliendesha VIBAYA. Na kila ukiangalia watoto walio baki, unaona pia hawafai kuliendesha gari hilo. Nafikiri unaweza fanya hivi;
  • Kwakuwa watoto wote wanamafunzo ya udereve, ACHISHA udereva huyo dereva aliopo.
  • Mpe udereva mtoto anayefuatia. Pima ufanisi wake. What do you have to loose, watoto wote si ni ovyo?!
  • Usipopenda ufanisi wake, Weka mtoto mwingine awe dereva. Pima ufanisi wake. Kwa wakati huu utakua umeanza kuona picha halisi ya watoto wako kwa vitendo. Huyu naye akianza kuharibu mambo, kabla ujafikia mtoto wa mwisho, Anza utaratibu wa kutafuta dereva nje ya familia. Ili sasa ujue utafanya nini baada ya wa mtoto wa mwisho kushindwa.
 
Africa kumekuwa na Cancer kubwa sana ya kukosa uadilifu katika uongozi. Chimbuko la yote haya linaanzia katika familia na mfumo wa Jamii ambao mafanikio ya mtu yanapimwa Kwa kile anachomiliki bila kujali kimepatikana Kwa njia za uadilifu au namna gani. Sumu hii inatutafuna. Watu wanakimbilia CCM Kwa sababu ukiwa huko ni rahisi kupata FURSA, CONNECTION na PROTECTION Kwa misingi ya kulinda chama. Mambo ya hovyo yanafanyika lakini yanawekwa undercover ili kulinda chama, na hapa kwenye kulinda chama ndio kunafanya ukosefu wa uadilifu utamalaki na unasababisha uozo usambae kakika ngazi zote za maisha lakini hii yote ni ripple effect inayoanzia juu.
 
Back
Top Bottom