CCM imeharibu Elimu yetu. Utumiaje kiingereza miaka 10 kujifunzia halafu usijue kiingereza?

Hapo ndipo unajua umuhimu wa shule za English Medium

Yeye alisoma za kawaida za kayumba
Miaka ya Magufuli akiwa primary na secondary elimu ya shule za kitaifa ilikuwa bora kama au zaidi ya private.
Lakini pia Magufuli O level kasoma seminary mpaka alipofukuzwa kwa kosa la uzinzi form 2
 
Dr. Magufuli, Dk. Ndalichako wamesoma kwa Kiingereza kwa zaidi ya miaka 16 na wanetoka kappa.
Hao
Sio hao karibuni kaibuka na waziri Jenista Mhagama naye kingereza hakipandi

Shida yao kubwa ni elimu ya masingi walisoma wote shule za kayumba swahili medium hivyo kingereza mgogoro

Solution wazazi pelekeni watoto English Medium mbapoambiwa elimu ya Msingi muwe mnaelewa

Msingi hata wa nyumba huhitajika kuwa imara kuliko unapoanza kujenga matofali juu

Kingereza shule ya msingi mhimu mno kujenga mtoto matofali ya huko juu .Sasa unataka mtu aweze kingereza akiwa juu wakati huku chini kwenye msingi kubovu

Dawa ni English medium shule zote za Serikali ziwe English medium kiswahili.kibaki kama mojawapo ya masomo na lugha ya nyumbani tu kama ilivyo Kenya .Shuleni kingereza ,nyumbani kiswahili kama wakenya watoto watakuwa wako vizuri tu

Mbona watoto wote wanaosoma shule za msingi za English Medium mbons kingeteza wako vizuri sana ma kiswahili wako vizuri
 
Miaka ya Magufuli akiwa primary na secondary elimu ya shule za kitaifa ilikuwa bora kama au zaidi ya private.
Lakini pia Magufuli O level kasoma seminary mpaka alipofukuzwa kwa kosa la uzinzi form 2
Primary alisoma kiswahili medium shida ni hapo
 
Kujua Kiingereza kunataka mazoezi ya kukitumia.

Tanzania watu wanaongea Kiingereza nje ya hizo shule?
Hapana.

Halafu hoja yangu Hawa wasiojua kiingereza (Jaji Mkuu alisema mawakili wengi hawajui kiingereza) Wana weledi kwenye taaluma zao?

Inakuwaje tutumie miaka kumi kufundishia wasomi wetu maarifa kwa lugha wasiyoimudu?

Halafu jee wakijifunza kwa kiingereza wanapokuja kwenye jamii huku mitaani hutumia Kiingereza kuwasiliana na jamii?

Hitimisho. Lugha ni nyenzo ya kupatia maarifa ingawa lugha yenyewe siyo maarifa. Sasa jee Kuna ulazima wa kutumia Kiingereza kutafutia maarifa?
 
Hili nalo nilakujiuliza wakati majibu yako wazi.

Unajifunza usiyoyajua kwa lugha usiyoijua, hapo hakuna miujiza ni kukariri tu. Sasa unategemea mtu aliye kariri akashindane kimataifa?

Suruhisho ni,
Tuwafunze watu wetu kwa lugha wanayoielewa, hii itawasaidia kujua wanachojifunza ila wajifunze kingereza kama lugha kama wanavyojifunza watu huko mitaani na wanakuwa na uwezo wa kuizungumza lugha ya kingereza kuliko wahitimu wa vyuo.

Usitegemee kwa mazingira haya ambayo watu hawazungumzi kiswahili fasaha eti wakawe wazungumzaji wa kingereza fasaha huo ni uongo labda itokee miujiza.
Suruhisho ni nini?
 
Hapana.

Halafu hoja yangu Hawa wasiojua kiingereza (Jaji Mkuu alisema mawakili wengi hawajui kiingereza) Wana weledi kwenye taaluma zao?

Inakuwaje tutumie miaka kumi kufundishia wasomi wetu maarifa kwa lugha wasiyoimudu?

Halafu jee wakijifunza kwa kiingereza wanapokuja kwenye jamii huku mitaani hutumia Kiingereza kuwasiliana na jamii?

Hitimisho. Lugha ni nyenzo ya kupatia maarifa ingawa lugha yenyewe siyo maarifa. Sasa jee Kuna ulazima wa kutumia Kiingereza kutafutia maarifa?
Kama unataka kuingia kwenye uchumi wa dunia Kiingereza hakiepukiki.

Kama unataka kujifungia Chanika na nduguzo hata Kizaramo unaweza kutumia.
 
Lugha yoyote kama hukuanza nayo utotoni lazima ikuzingue kiasi chake. Kiingereza kiwe lugha kuu ya kufundishia kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Kuanza kujifunza kiingereza form one ni ujinga.
 
Suruhisho ni nini?
Na suluhisho ni kuwa kama jamii tunawezaje kuwa na wasomi wenye Elimu na siyo wasomi waliofaulu mitihani pekee.

Tunakuwa na wasomi lakini linapokuja suala la kupambania maslahi ya nchi nje ya Tanzania eti tunakodisha wasomi toka nchi nyingine.
 
Kama unataka kuingia kwenye uchumi wa dunia Kiingereza hakiepukiki.

Kama unataka kujifungia Chanika na nduguzo hata Kizaramo unaweza kutumia.
Sawa. Na Mimi nakubaliana nawe. Lakini kwenye kitabu nilichoweka hapo juu " Language Crisis in Tanzania..." Waandishi wana hoja kubwa Sana.

Wanauliza Kila msomi wetu atahitaji kuwa na weledi wa kiingereza? Hoja yao jee ni watanzania wasomi wangapi watakutana na mazingira ya kuwalazimisha kutumia Kiingereza kuwasiliana.

Na kwenye kitabu hicho wameweka tafiti mbali mbali kuonesha kuwa si kweli kuwa ni lazima wasomi wetu wote wajue kiingereza ili wapate maarifa na kuyatumia maarifa hayo kwa jamii.
 
Katika ulimwengu unaojichanganya kimataifa ukijifungia ndani ushapotea.
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.
Yaan mwalimu ana 4 ya mwshoni, aje anifundishe nijue unge vizuri kabsaaa🙄
 
Katika ulimwengu unaojichanganya kimataifa ukijifungia ndani ushapotea.
Yes. Hii hoja ya kujifungia ndani ni ya kinadharia zaidi. Wachina wanaipelekesha Dunia kiteknolojia na kiuchumi. Jee unadhani ni asilimia ngapi ya wasomi wachina wanaotumia kiingereza kujifunzia na kuwasiliana?

Kwa takwimu ni kama wachina milioni 10-25 ndiyo wanaotumia kiingereza kuwasiliana kati ya wachina bilioni Moja na milioni mia nne, sawa na asilimia kama tatu na kidogo.

Kuna nini kitatokea kama Kiingereza iwe somo la lugha inayotiliwa mkazo halafu kiswahili ikawa ndiyo lugha ya kufundishia?

Hakuna mahali nimeoneaha shaka ama kusema watu wasijifunze kiingereza.
 
Kanuni moja muhimu kabisa ya kulinganisha ni kulinganisha vinavyolinganishika.

Vinavyofanana.

Ndiyo maana hata kwenye ndondi watu wanapiganishwa kwa uzito ubaofanana.

Wachina wana civilization ya maelfu ya miaka iliyoanza kutengeneza bunduki kabla ya wazungu.

Lugha wa Kichina ina historia ndefu kuliko Kilatini cha kale na Kigiriki cha kale.

Usilinganishe Tanzania na China.
 
Usilinganishe Tanzania na China.
Nakubaliana na hoja yako. Kweli tusilinganishe visivyolingana.

Kwa mfano Kenya wanachama cha waalimu kinaitwa Kenya National Teachers Union (KNUT) na Tanzania tuna Chama cha waalimu Tanzania (CWT)
Hivi ni vyama viwili vya kitaaluma vya aina moja. Lakini ukiangalia uwekezaji unaofanywa na KNUT ni mkubwa kuliko ule wa CWT.

Nguvu ya KNUT kwenye kusimamia maslahi ya waalimu Kenya ni kubwa kuliko nguvu ya CWT kwenye kusimamia maslahi ya waalimu Tanzania.

Jee ni kwa kuwa Kenya wanatumia kiingereza kujifunzia ndiyo maana KNUT Ina nguvu sana kuliko CWT?

Pia hoja yangu inatilia shaka kama mtu anatumia lugha kwa miaka kumi kujifunzia, halafu haimudu lugha hiyo, ni kweli anayo maarifa inayosemwa anayo?
 
Kwahio kwa logic yako sababu watu wanaweza kuongea kiswahili tangia wazaliwe hata wakipewa paper ya kiswahili watapa A ?

Au kujua na kutokujua tunakupima vipi ?
 
Nakubaliana na hoja yako. Kweli tusilinganishe visivyolingana.

Kwa mfano Kenya wanachama cha waalimu kinaitwa Kenya National Teachers Union (KNUT) na Tanzania tuna Chama cha waalimu Tanzania (CWT)
Hivi ni vyama viwili vya kitaaluma vya aina moja. Lakini ukiangalia uwekezaji unaofanywa na KNUT ni mkubwa kuliko ule wa CWT.

Nguvu ya KNUT kwenye kusimamia maslahi ya waalimu Kenya ni kubwa kuliko nguvu ya CWT kwenye kusimamia maslahi ya waalimu Tanzania.

Jee ni kwa kuwa Kenya wanatumia kiingereza kujifunzia ndiyo maana KNUT Ina nguvu sana kuliko CWT?

Pia hoja yangu inatilia shaka kama mtu anatumia lugha kwa miaka kumi kujifunzia, halafu haimudu lugha hiyo, ni kweli anayo maarifa inayosemwa anayo?
Kenya is more outwardly looking than Tanzania. English is a big part of that.

Elimu na uchumi no vitu vinavyiendana. Huwezi kuwa na elinu bira kama huna uchumi mzuri na huwezi juwa na uchumi mzuri kama huna elimu bora.

Unaelewa kuwa hata kwenye kazi za kufundisha Kiswahili kimataifa, walimu wa Kenya wanawashinda walimu wa Tanzania?

Unaelewa kuwa Kiingereza kimechangia sana hapo, hata kwenye Kenya kutushinda kwenye kufundisha Kiswahili?

Tanzania hata unaposema wanatumia lugha miaka kumi kujifunzia hawatumii lugha hiyo, wanabumbabumba tu.
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.
YAWEZEKANA HATA KISWAHILI WAKAWA WANAFELI.LUGHA AMBAYO HUJAFUNDISHWA NA MAMA MZAZI SIYO MCHEZO MCHEZO
 
Wachache sana. Watanzania hawana uthubutu huo
Hivi ukimuona Rais au kiongozi yeyote mkubwa akiwa ziarani nje ya nchi, km Marekani, akikutana na umma wa Watanzania waishio huko (diaspora), umeshawahi kujiuliza ni nani hao au walifikaje huko?

Bila shaka kwa mawazo yako unaamini wote, ukitoa watumishi wa ubalozi, ni wazamiaji na wabeba box (msamiati wa JF). Na kwako mtu maarufu unayemtambua ni Mange Kimambi pekee.

Wake up! Kushuka kwa elimu Tanzania kunawanyima fursa nyingi duniani vijana wa ki-Tanzania. Propaganda hazisaidii kitu. Ni muhimu kupigania elimu irejeshwe kwenye viwango stahiki.

Ni AIBU kwa nchi kuwa na shule zinazojinasibu eti “English Medium School”! Ni aina ya fulani ya ushamba.
 
Back
Top Bottom