Hakuna chama hapo,kilishajifia siku nyingi. Chama hakina ushawishi wa kawaida,chama kina jificha kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,chama kinabebwa na ma DC na ma RC,chama kinabebwa na ma ded.
Chama kinaogopa ukosoaji; hamna chama Cha siasa hapo
chama na serikali yake vinawaogopa wananchi wake. Chama hakiwezi kuruhusu serikali kupanga wala kusafisha miji kuogopa kukosa kura. Kwenye duka la vipodozi unaweza kuuza unga au pombe kama ukitaka.
Wanaomzunguuka Rais ndio chanzo cha kila kitu kisichofaa. Watu hawa wanamtisha, kumtia hofu na kumdanganya Rais kwa maslahi yao kuhusu kushindwa na kushinda uchaguzi. Watu hawa huwa hawapigi kampeni majukwaani wala kuyaelezea yale mazuri yaliyofanywa na serikali na sera mbovu za wapinzani, badala yake wanamtaka Rais abariki matumizi ya njia haramu kushinda uchaguzi kwa maslahi yao.
Watanzania sio maafala hata kidogo, ila hawaoni bado chama mbadala chenye viongozi mbadala. Watanzania hawana kero bado iliyofika shingoni kiasi cha kuitoa CCM kwa nguvu ya umma. Bado zipo sehemu za kuegesha bodaboda, kutandika chini biashara, kulima na kuvua.
Watanzania sio mafala bali wana maumivu ambayo yanafumilika bado. Kuna wakati watashindwa kuyavumilia na kila mtu atajishangaa mwenyewe na kushangaana.