CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

CCM imemlipia faini ya Tsh. Milioni 30 mwanachama wake Dkt. Vincent Mashinji. Atoka gerezani

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2019
Posts
1,521
Reaction score
4,381
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam kimemlipia faini ya Shilingi Milioni 30 mwanachama mpya wa chama hicho Vincent Mashinji aliyekutwa na hatia kwenye makosa kadhaa kwenye Hukumu iliyotolewa jana ya kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia hatua hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Humphrey Polepole, amesema kiasi hicho cha fedha kimechangwa na wanachama wa chama hicho ili kumtoa kada huyo aliyelala gereza la Segerea baada ya zoezi la kulipa adhabu hiyo jana kushindikana kwasababu ya muda.

Polepole.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akionesha risiti ya malipo leo Jumatano Machi 11, 2020 alipofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kulipa faini ya milioni 30 ya mwanachama wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji.



UPDATE: Dkt. Mashinji atoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 30

mashinjii.jpg

Dkt. Mashinji akiwa ndani ya gari baada ya kutoka gerezani

Akizungumza baada ya kutoka jela, Dk Mashinji amesema, “ sikutegemea wana CCM watanilipia faini, sikutegemea wangelifanya jambo hili kwa uzito kama huu maana hadi jana familia yangu ilikuwa inaendelea kutafuta fedha ili kunitoa.”

“Ila leo wana CCM Mkoa wa Dar es Salaam wamejiunga kwa pamoja na kunilipia faini, nashukuru nipo chama dume kwa ajili ya kutoa mchango wangu kwa Taifa.”
 
Ndio maana watu wanahamia ccm si kwakujaliwa huko [emoji23][emoji23]


Sent using Jamii Forums mobile app
Huko bado kiini macho, a.k.a utakatishaji unaendelea. Haiingii akilini wabunge wote haokukosa hizo fedha. Nyumbu wa Ufipa wanaendelea kutumika tu bila kujijua. Hata hivyo hiyo faini mabeberu watailipa. Hapa tunadanganywa tu kuwa wananchi wanachanga.
 
Back
Top Bottom