Uchaguzi 2020 CCM imeonesha demokrasia kuhesabu kura kwa uwazi, tume ya uchaguzi ifanye hivyo

Kwani ni lini kura hazikuhesabiwa kituoni? Tume yetu ni huru Sana, ndio maana kura huwa zinahesabiwa na kubandikwa vituoni mara tu baada yakumaliza zoezi lakupiga kura Tena kwauwazi kwaushiriki wa vyama vyote na waangalizi wengine.
Hizo zingine ni hofu yakushindwa
 
Kuhesabu sio issue. Hivi Walionyesha live pia kura zilivyopigwa? Term ya pili ya JK kura zilipiwa kimikoa na kila Mkoa uliambiwa kama itatokea kura ya Hapana, watapaswa kuwajua na kuwataja hao “wakorofi”. Huu ni uburuzwaji
 
Ukitulia na kutafakari vizuri,unagundua kuwa CCM wanafanya siasa kweli kweli na CHADEMA wanafanya harakati,harakati zinaweza kuwa sehemu ya siasa ila si wakati wote. Ccm wamehesabu kura hadharani ilawakiwa wamejipanga na wako oncontrol. Uchaguzi wa 2015 wasingeweza kufanya vile.
Mimi binafsi nawasifu ccm wanavyofanya siasa
 
Kwa namna mchakato mzima wa kuwapata wagombea ulivyoendeshwa ndani ya CCM, hapakuwa na haja hata ya kwenda kupoteza muda wa kupiga kura! Hii ni sababu wagombea urais wa pande zote mbili tayari walishatengenezewa mazingira na walishajulikana hata kabla ya kupiga kura! Kwa upande wa Zenji ilishajulikana DK Mwinyi ndiye alikuwa chaguo la wenye nguvu na mamlaka, hivyo tayari mchezo ulishamalizwa mapema kabisa! Kwa upande wa bara kwanza wale wote waliokuwa na nia ya kutaka kuja kushindana na Magu, walishafukuzwa toka ndani ya chama na zaidi yote hata formu ya mgombea iliandaliwa moja tu, hivyo kilichokwenda kufanyika kuthibitishwa na wala si kuchagua tena maana kila kitu kilishachongwa tangu mwanzo! Alafu utasikia vyombo vya habari vikisema kashinda kwa kishindo! Najiuliza alishindana na nani????...
 
kuhesabu kura mia sio sawa kuhesabu kura milioni. Wacha wahesabu kikawaida wamalize haraka watoe jibu tu.
Nigeria walihesabu kuea hadharani, zikahkikiwa hadgarani. Wapiga kura ni wengi, zaudi ya mara 6 ya Watanzania. Na bafo majibu yalitoka haraka.

Majibu ya kura huwa yanacheleweshwa na uchakachuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanye hivyo yaani unaandika jina lako halafu karatasi haikunjwi kila mmoja anaweza kusoma ulichoandika hiyo ndiyo demokrasia unayo itaka?
 
Bonge ka point!
Na wala kilio cha tume huru kisingelikuwa na maana yoyote.

Baada ya kura kupigwa, wagombea na wawakilishi wao wanajitoma ndani kushiriki kuhesabu kwa kupokea matokeo yao moja kwa moja, pasingekuwa na majungu wala lawama.
 
demokrasia ni kura ya siri, siyo wazi kama ilivyofanyika!
Kura ya siri! Kwani kura haikupigwa kwa siri?
Kura ilipigwa kwa siri, ila namna ya kuhesabu ndiyo inayoongelewa hapa ili kuondoa utata na majungu yasiyokuwa na ulazima wowote.
 
Kujecharize matokeo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]!
 
Kura ya siri! Kwani kura haikupigwa kwa siri?
Kura ilipigwa kwa siri, ila namna ya kuhesabu ndiyo inayoongelewa hapa ili kuondoa utata na majungu yasiyokuwa na ulazima wowote.
karatasi hazikukunjwa.
kila aliyepiga NDIYO/SIYO kamera zilikuwa zinamdeku tu kwa ajili ya figisu baadaye!
 
Ndo maana kila chama kinakuwa na wakala wake wa kuhesabu kura na matokeo yanatangazwa na kubandikwa na mawakala wanasaini.huo ni uwazi wa hali ya juu.
 
uwazi si kwenye kupiga kura.... ndiyo maana kwenye uchaguzi mkuu mtu hutengewa chamber yake peke yake ya faragha!

Uwazi kama ule unahitajika kwenye kuhesabu kura zilizopigwa kwa siri.
 
Demokrasia ni kkumchagua mgombea wao wa Urais pale Kisiwandui
 
Thubutu! Umeona taratibu za maadili zilizotungwa na msajiri wa vyama? Zinasisitiza usiri wa hali ya juu.
 
Tena uwazi wa aina hiyo ni wa kuigwa , maana upigaji kura kila mtu anakuona , kutumbukiza kura sandukuni bila kukunjwa na sanduku unaloweka kura linajulikana wapigaji kura wake wote
 
Hata kura huwa zinahesabiwa kwa uwazi mbele ya wasimamizi na mawakala. Wasimamizi huwa hawafaamiani na mawakala wanatoka vyama mbalimbali swala la uwazi huwa ni kubwa mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…