PostGE2025 CCM imeshaanza kujiteulia wasuluhishi na wapatanishi wa mauaji ya Oktoba 2025

PostGE2025 CCM imeshaanza kujiteulia wasuluhishi na wapatanishi wa mauaji ya Oktoba 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nani atakubali TAKATAKA zao? Wasione wanaweza kila kitu

Hatutakuwa na maneno matupu kwanza
1. Msulihishi atoke nje ya Bara la Afrika maana hawa wotewni madikteta hakuna mwafrika atakuja awe upande wa wananchi ,
2. Tundu lissu na kesi Nyingine zoote zifutwe
3. Vyama vya siasa hewa vilivyopewa Pesa na CCM kufanya siasa uchwara vifilisiwe na watubu,
4. Tume huru ya Uchaguzi iundwe, ihusishe, kila wanachama, na ipitiwe na mahakimu au mawakili
5. Katiba mpya
6. Bunge livunjwe na uchaguzi mkuu urudiwe
Hayo yote hayatekelezeki. Labda watekeleze CDM na TEC. Otherwise maisha yaendelee hivi hivi mpaka 2030
 
Vyombo vya habari Namibia ikiwepo Shirika la Utangazaji Namibia (NBC) vimeripoti taarifa ya Naibu Jaji Mkuu wa Namibia kuombwa na Tanzania kujiunga katika Tume ya Uchunguzi Tanzania

Naibu Jaji Mkuu wa Namibia Petrus Damaseb ameteuliwa kuhudumu katika tume ya Rais ya uchunguzi Tanzania, itakayochunguza ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa 2025 nchini Tanzania.

Ofisi ya Mhimili wa Mahakama nchini Namibia ilitangaza siku ya Jumatano kuwa Jaji Mkuu Peter Shivute alimteua Jaji Damaseb kufuatia ombi kutoka kwa Serikali ya Tanzania kwa Namibia.

Ombi la Serikali ya Tanzania kwa Serikali ya Namibia lilikuwa ni kutoa jaji anayehudumu au aliyestaafu wa Mahakama Kuu ya Namibia ili kuhudumu kwenye tume hiyo ya uchunguzi.

Tume hiyo imeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchunguza vyanzo vikuu vya vurugu zilizofuata baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa 29 Oktoba 2025,

Ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio hayo ya siku na baada ya uchaguzi zinaonyesha angalau vifo 518 vilirekodiwa, huku takriban watu 2,400 wakijeruhiwa wakati wa machafuko hayo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya NBC Digital News na The Namibian inaeleza kwamba, Wajumbe wa tume hiyo ya uchunguzi wataapishwa tarehe itakayotangazwa na Serikali ya Tanzania.

The mosquito going to investigate malaria?

Nini maoni yako?
Hii ni zaidi ya kilichofanyika oct 29 na baada!
 
Back
Top Bottom