Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
CCM imeendelea kuonyesha Umwamba wake katika siasa za Nchi hii na Bara zima la Afrika.imeendelea kuonyesha namna inavyokubalika ,kupendwa ,kuungwa mkono na namna ilivyo na ushawishi mkubwa hapa Nchini.
Imeonyesha namna ilivyobeba Matumaini ya mamilioni ya watanzania.imeonyesha Watanzania bado hawapo tayari kuongozwa na vyama vya upinzani wala kuviamini vyama vya upinzani. Imeonyesha watanzania bado hawaoni tumaini jipya kutoka vyama vya upinzani.
CCM Imeshinda uchaguzi huu kwa haki na kihalali kabisa .hii ni kwa kuwa CCM ilijiandaa vyema na uchaguzi huu,iliwekeza kwa watu ,ilikuwa karibu na watu,ilisikiliza sauti za watu,ilifanyia kazi na kutatua kero na changamoto za watu,ilijibu kwa wakati kero za watu, ilipeleka huduma karibu na watu,ilijisahihisha pale ilipokosea.
Lakini kubwa kuliko ni kuwa CCM iliteua viongozi na wagombea wanaokubalika kwa watu,wenye ushawishi kwa watu,waadilifu , wanyenyekevu,wasikivu, wachapakazi,wenye historia nzuri katika jamii na wenye ushirikiano mkubwa na wanajamii. CCM iliteua wagombea ambao walikuwa wanajua kero za maeneo yao na namna ya kumaliza kero hizo.
Wakati hayo yakifanyika upande wa pili vyama vya upinzani hususan CHADEMA ilikuwa inafanya kazi ya kuokoteza okoteza wagombea wasio na ushawishi wala uwezo wa kuongoza wala kukubalika kwa watu.iliteua wagombea wenye sifa mbaya kwa jamii ,wasio na upeo wala kufahamu vyema mahitaji ya watu.ndio maana walikuwa wanashindwa hata namna ya kujenga hoja za kueleweka majukwaani.
Lakini pia chama kwa ujumla kuanzia ngazi ya juu hakikuwa na maandalizi ya aina yoyote ile ya kushinda uchaguzi huu.hakukuwa na mipango na mikakati ya pamoja,hakukuwa na sera wala ajenda za pamoja,hakukuwa na muunganiko na ushirikiano wa viongozi.ni kama kila mtu alikuwa anapigana vita yake kutafuta ushindi wake binafsi. Ndio maana chama kimepoteza pambano pamoja na vita yenyewe.
Angalia Mbowe Mwenyewe alikuwa amejificha nyumbani kwake huko siku zote na kuja kuibukia siku za mwisho kwa kupita maeneo machache tu.huku Lissu naye alikuwa akipuyanga tu kivyake bila ajenda wala sera za kueleweka wala hoja zenye kugusa Maisha ya watu.chadema ya sasa ilikuwa ni tofauti sana na ile CHADEMA ya 2014 chini ya Dkt Slaa pamoja na Mbowe Mwenyewe ambao walifanya kazi ya kuzunguka Nchi Nzima kupiga mikutano ya nguvu na yenye kila aina ya hoja zenye kugusa Maisha ya watu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.