LGE2024 CCM Imeshinda kihalali na kuvuna kile ilichopanda, CHADEMA haikujipanga

LGE2024 CCM Imeshinda kihalali na kuvuna kile ilichopanda, CHADEMA haikujipanga

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Unapingana na akija jaji Warioba walioukataa uchaguzi wa 2020 ambao ni muendelezo wa chaguzi za baada ya hapo? Jiwe alikuwa mtu mbaya sana na wizi wa kura wa wazi bila aibu unaoendelea kwenye chaguzi uliasisiwa na jiwe. Hata wana ccm wale wanaokipenda chama na wanaofahamu siasa hawawezi kukubali upuuzi mnaouita uchaguzi. Chama kimetoka kwenye wizi wa kificho wameamua kuwa wezi wa kura bila aibu.

Huo uhalali ni kwa tafsiri ya ccm.
Kubalini ukweli kuwa hamkujipanga katika uchaguzi huu na kwamba mnapaswa kujipanga upya hapo mwakani.
 
Kubalini ukweli kuwa hamkujipanga katika uchaguzi huu na kwamba mnapaswa kujipanga upya hapo mwakani.
Wewe chawa usidhani kila anayekosoa upuuzi wa ccm ni chadema. Unapumbaza ufahamu wako wa kutofautisha jema na baya kwa sababu ya njaa zako tu. Wizi wa kura ccm ni wa muda mrefu ila umezidishwa na sababu ni wananchi wengi kuikataa ccm. Kama hujui hilo pole sana.
 
Wewe chawa usidhani kila anayekosoa upuuzi wa ccm ni chadema. Unapumbaza ufahamu wako wa kutofautisha jema na baya kwa sababu ya njaa zako tu. Wizi wa kura ccm ni wa muda mrefu ila umezidishwa na sababu ni wananchi wengi kuikataa ccm. Kama hujui hilo pole sana.
CCM tunapita kihalali na kwa haki.ndio maana unaona wananchi wakishangilia ushindi mitaani kote.
 
Tufute upinzani. Wa nini na chama tawala ndo pekee kinachohitajika?
Kama mnataka kufuta upinzani futeni maana hauna chochote çha maana. ufuteni tuu kàma chama tawala ndo pekee kinachohitajika.
 
Mimi sitokuja kupiga kura mpaka tupate chama cha upinzani chenye nia ya dhati ya kuwapambania watanzania.

Sio awa wa sasa hoja zao ni kuzusha taarifa mjini tweeter.
Watanzania wapi hawa au wengine? Kama mnategemea vyama vya upinzani ndio viwaletee mabadiliko basi mko nyuma sana na mtakuwa dissapointed, wananchi pambaneni wenyewe
 
Ndugu zangu Watanzania,

CCM imeendelea kuonyesha Umwamba wake katika siasa za Nchi hii na Bara zima la Afrika.imeendelea kuonyesha namna inavyokubalika ,kupendwa ,kuungwa mkono na namna ilivyo na ushawishi mkubwa hapa Nchini.

Imeonyesha namna ilivyobeba Matumaini ya mamilioni ya watanzania.imeonyesha Watanzania bado hawapo tayari kuongozwa na vyama vya upinzani wala kuviamini vyama vya upinzani. Imeonyesha watanzania bado hawaoni tumaini jipya kutoka vyama vya upinzani.

CCM Imeshinda uchaguzi huu kwa haki na kihalali kabisa .hii ni kwa kuwa CCM ilijiandaa vyema na uchaguzi huu,iliwekeza kwa watu ,ilikuwa karibu na watu,ilisikiliza sauti za watu,ilifanyia kazi na kutatua kero na changamoto za watu,ilijibu kwa wakati kero za watu, ilipeleka huduma karibu na watu,ilijisahihisha pale ilipokosea.

Lakini kubwa kuliko ni kuwa CCM iliteua viongozi na wagombea wanaokubalika kwa watu,wenye ushawishi kwa watu,waadilifu , wanyenyekevu,wasikivu, wachapakazi,wenye historia nzuri katika jamii na wenye ushirikiano mkubwa na wanajamii. CCM iliteua wagombea ambao walikuwa wanajua kero za maeneo yao na namna ya kumaliza kero hizo.

Wakati hayo yakifanyika upande wa pili vyama vya upinzani hususan CHADEMA ilikuwa inafanya kazi ya kuokoteza okoteza wagombea wasio na ushawishi wala uwezo wa kuongoza wala kukubalika kwa watu.iliteua wagombea wenye sifa mbaya kwa jamii ,wasio na upeo wala kufahamu vyema mahitaji ya watu.ndio maana walikuwa wanashindwa hata namna ya kujenga hoja za kueleweka majukwaani.

Lakini pia chama kwa ujumla kuanzia ngazi ya juu hakikuwa na maandalizi ya aina yoyote ile ya kushinda uchaguzi huu.hakukuwa na mipango na mikakati ya pamoja,hakukuwa na sera wala ajenda za pamoja,hakukuwa na muunganiko na ushirikiano wa viongozi.ni kama kila mtu alikuwa anapigana vita yake kutafuta ushindi wake binafsi. Ndio maana chama kimepoteza pambano pamoja na vita yenyewe.

Angalia Mbowe Mwenyewe alikuwa amejificha nyumbani kwake huko siku zote na kuja kuibukia siku za mwisho kwa kupita maeneo machache tu.huku Lissu naye alikuwa akipuyanga tu kivyake bila ajenda wala sera za kueleweka wala hoja zenye kugusa Maisha ya watu.chadema ya sasa ilikuwa ni tofauti sana na ile CHADEMA ya 2014 chini ya Dkt Slaa pamoja na Mbowe Mwenyewe ambao walifanya kazi ya kuzunguka Nchi Nzima kupiga mikutano ya nguvu na yenye kila aina ya hoja zenye kugusa Maisha ya watu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ukiona chama kinakaa madarakani kwa chaguzin za kihayawani, ujue chama hicho kiko nje ya wakati.
 
Binafsi huwa nawashangaa upinzani hii nchi na Imani yao ya kutoboa.
Serikali iliyopo madarakani ndio mzimamizi wa mchakato mzima wa uchaguzi Sasa inawezekanaje ikajipiga mama kupitia mchakato huo?
 
CCM tunapita kihalali na kwa haki.ndio maana unaona wananchi wakishangilia ushindi mitaani kote.
Ipi mantiki yako? Cdm na ccm ni watu na wote ni wananchi au ni uongo? Ccm wakishangilia ni wananchi pia na Cdm walioyakataa matokeo ni wananchi pia na hiyo ndio mantiki. Hakuna kitu kinachoitwa wananchi katika ujumla wao wakiwa na mitazamo inayofanana. Kinachopingwa ni dhuluma ya wazi kabisa ambayo kila mfuatiliaji wa siasa ameona kupitia video mbalimbali mitandaoni.

Mambo kama hayo ndio unachangia umaskini wako na kizazi chako lakini kwa kuwa huna vision huwezi kuyaona hayo. Ccm ni wezi wa kura kama unakataa na huku nafsi yako ikiujua ukweli basi wewe ni mfuasi wa ibilisi. Kwenye mambo ya haki za watu hupaswi kuwa mpumbavu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

CCM imeendelea kuonyesha Umwamba wake katika siasa za Nchi hii na Bara zima la Afrika.imeendelea kuonyesha namna inavyokubalika ,kupendwa ,kuungwa mkono na namna ilivyo na ushawishi mkubwa hapa Nchini.



Lucas Hebel Mwashambwa, Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mr Lucas Mimi nipo neutral sio CCM wala sio mpinzani.
Kwa Hali niliyoiona hamna chochote Cha kujivunia maana mlicheza faulo tangu wakati wa kupitisha majina kwa kuwakata isivyo halali wapinzani wenu karibu nchi nzima so ushindani haukuwepo kwavile mlikuwa mkiogopa kushindwa iwapo haki ingefanyika mngeanguka vibaya sana au ingekuwa 50/50.
Mathalani Hapa mtaani kwetu vituo vilikuwa vyeupee watu wengi hawakupiga kura sababu waliowataka sio waliopitishwa kugombea
 
Mr Lucas Mimi nipo neutral sio CCM wala sio mpinzani.
Kwa Hali niliyoiona hamna chochote Cha kujivunia maana mlicheza faulo tangu wakati wa kupitisha majina maana mliwakata visivyo halali wapinzani wenu karibu nchi nzima so ushindani haukuwepo kwavile mlikuwa mkiogopa kushindwa maana haki ingefanyika mngeanguka vibaya sana au ingekuwa 50/50.
Hapa mtaani kwetu vituo vilikuwa vyeupee watu wengi hawakupiga kura sababu waliowataka sio waliopitishwa kugombea
Hivi unafahamu ya kuwa maeneo mengi sana CHADEMA ilikuwa haina wagombea baada ya kukosa wagombea? Unajua ilifika wakati ikawa inawaomba watu wagombea ambao ukiwaangalia walikuwa hawakubaliki kabisa.dosari huwa zinakuwepo na ni kawaida katika uchaguzi.lakini ukweli ni kuwa upinzani haukujipanga na umepoteza kabisa ushawishi.embu niambie Mbowe alianza lini kupiga kampeni za uchaguzi huu?
 
Mimi sitaki kukupinga wala kukukubalia kwamba ccm inaongoza kwa kukubalika ila mimi ni muumini wa ushindani wa halali kwa hiyo nakerwa sana na matukio kama lile la iringa kuzuia kugongwa muhuri kwenye barua za mawakala wa chadema, kule Dodoma kukutwa masanduku ambayo yamepigwa kura tayari mara kuna watu wamepiga kura lakini hawapo kwenye daftari Matukio kama yale yanatia kinyaaa.

Maana kama mnkubalika acheni ushindani wa halali ili mtu anayeshindwa ashindwe kwa halali
Fact
 
Back
Top Bottom