LGE2024 CCM Imeshinda kihalali na kuvuna kile ilichopanda, CHADEMA haikujipanga

LGE2024 CCM Imeshinda kihalali na kuvuna kile ilichopanda, CHADEMA haikujipanga

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ukiona chama kinakaa madarakani kwa chaguzin za kihayawani, ujue chama hicho kiko nje ya wakati.
CCM inapendwa, kuaminika na kukubalika sana na ndio maana inaendelea kusalia madarakani kwa kupigiwa kura katika kila uchaguzi
 
Binafsi huwa nawashangaa upinzani hii nchi na Imani yao ya kutoboa.
Serikali iliyopo madarakani ndio mzimamizi wa mchakato mzima wa uchaguzi Sasa inawezekanaje ikajipiga mama kupitia mchakato huo?
Wapinzani wa Tz na wao ni kama hawana msaada kwa wananchi. Suala la uchaguzi lilipaswa kukataliwa kabisa hadi pale kutakapokuwa na tume huru. Kingine walipaswa kuhakikisha wanafungua kesi nyingi sana zitakazolazimisha kuwepo kwa chaguzi huru. Utaratibu mzima wa uchaguzi unatoa mianya kwa ccm kufanya hujuma na hayo yalitakiwa yakapingwe mahakamani kwa ushahidi na kama wangefanyiwa hujuma kwenye kesi wangerudi kwa wananchi na kuwaeleza hali halisi kisha wananchi wataamua wenyewe lakini chama kinapita mule mule ccm inakotaka kipite na baadae wanalalamika wizi wa kura.

Ccm ni wezi wa kura na kama CDM itaendelea kushiriki chaguzi kwa kuamini kuwa wanaweza kushinda basi huo ni ujuha. Miaka zaidi ya 30 ya CDM bado wanalalamika wanaibiwa kura kila chaguzi bila kuchukua hatua yoyote ni upumbavu sana. Ni bora wajiondoe kwenye siasa wabaki ccm na vibaraka wao.
 
Wananchi hawana habari na CHADEMA maana wanajua ni wababaishaji sana.
 
Hivi unafahamu ya kuwa maeneo mengi sana CHADEMA ilikuwa haina wagombea baada ya kukosa wagombea? Unajua ilifika wakati ikawa inawaomba watu wagombea ambao ukiwaangalia walikuwa hawakubaliki kabisa.dosari huwa zinakuwepo na ni kawaida katika uchaguzi.lakini ukweli ni kuwa upinzani haukujipanga na umepoteza kabisa ushawishi.embu niambie Mbowe alianza lini kupiga kampeni za uchaguzi huu?
Mimi shahidi hapa mtaani vilikitokeza vyama vingi vilivyo simamisha wagombea mbali ya hiyo Chadema na CCM ila wote hao wa vyama vingine walihenguliwa visivyo halali na kuachwa wa CCM pekee sa jiulize haki Ipo wapi?
Watu wenye elimu zao za vidato waliogombea uenyekiti wa mtaa na ujumbe eti form zao Zina kasoro na Darasa la saba CCM ndio hawana kasoro
 
CCM inapendwa, kuaminika na kukubalika sana na ndio maana inaendelea kusalia madarakani kwa kupigiwa kura katika kila uchaguzi
Sio kwa huu ukhanithi tunaouna kwenye hizi chaguzi. Fahamuni kizazi kimebadilika, ukiona unatumia mbinu chafu kubaki madarakani uje kizazi sio chako tena.
 
Sio kwa huu ukhanithi tunaouna kwenye hizi chaguzi. Fahamuni kizazi kimebadilika, ukiona unatumia mbinu chafu kubaki madarakani uje kizazi sio chako tena.
Mbinu inayotumia CCM kushinda kwa kishindo ni kuwa na wagombea wanaokubalika vyema na wenye sera na ajenda zenye kugusa Maisha ya watu.
 
Mbinu inayotumia CCM kushinda kwa kishindo ni kuwa na wagombea wanaokubalika vyema na wenye sera na ajenda zenye kugusa Maisha ya watu.
Wagombea wanaokubalika, hiyo kuengua wapinzani inatokea wapi? Ukiona chama kinaogopa chaguzi za haki, ujue chama hicho kimepoteza ushawishi kwa umma.
 
CCM Imeshinda kihalali na kuvuna kile ilichopanda, CHADEMA haikujipanga.
Je ni nini matokeo ya ccm kushinda kihalali?
 
Mimi sitaki kukupinga wala kukukubalia kwamba ccm inaongoza kwa kukubalika ila mimi ni muumini wa ushindani wa halali kwa hiyo nakerwa sana na matukio kama lile la iringa kuzuia kugongwa muhuri kwenye barua za mawakala wa chadema, kule Dodoma kukutwa masanduku ambayo yamepigwa kura tayari mara kuna watu wamepiga kura lakini hawapo kwenye daftari Matukio kama yale yanatia kinyaaa.

Maana kama mnkubalika acheni ushindani wa halali ili mtu anayeshindwa ashindwe kwa halali
Hili Mzee wa kupiga kura kwa wizi Lukas Mwashambwa anakimbia kujibu!
 
Ushindi iliyopata CCM ni ushindi wa watanzania wote wapenda maendeleo,amani,utulivu, mshikamano na ustawi wa Taifa letu.
NO HAPANA.

NI WIZI NA UDANGANYIFU KATIKA KURA. TUNAWAPATA VIONGOZI WALIONGIA MADARAKANI BILA RIDHAA YA WANANCHI.
IFIKE MAHALI KURA YA KIA MLALA HOI IHESHIMIKE.
CCM INA RASILIMALI FEDHA NYINGI SANA NA INATAKIWA KUTUMIA HOJA KUSHAWAHISHI WAPIGA KURA NA KUVIPA VYAMA VINGINE FURSA KWA MUJIBU WA KATIBA.

TUNATENGENEZA BOMU ZAIDI YA UKOLONI AMBALO LITAKUJA KULIPUKA TU
 
CCM inapita kwa kupendwa na watanzania kunakotokana na ubora wa sera na ajenda zake pamoja na utekelezaji mzuri wa ilani yake ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom