Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 253
- 360
👉Kwa Nia njema Nina Machache kuhusu maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama changu Cha Mapinduzi (CCM), niseme tu kwamba CCM inahitaji kufanya 'Reform' yaani Mageuzi au Mabadiliko ili kutengeneza ari na mwamko mpya wa Chama na kuleta mvuto kwa wanachama wake pamoja na watu wengine wasio wanachama wa CCM.
👉Reform hizi lazima ziendane na mabadiliko ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na Kiitikadi, yanayohitaji umakini mkubwa na uwazi.
👉Kwanza ni muhimu Uongozi wa Chama uwe shirikishi, yaani viongozi wapya ngazi zote wanapoingia kukiongoza Chama lazima watokane na msukumo wa wanachama na sio msukumo wa wajumbe walioko ukumbini na wala wasitokane na NDIYO ya wajumbe wanapokuwa ukumbini.
👉Ukiwa mjumbe ndani ya ukumbi inahitaji ujasiri sana kusema HAPANA kwa kiongozi aliyependekezwa na viongozi wako walio juu yako.
👉 Kuepusha hilo ni vema viongozi watokane na msukumo au maoni ya wanachama ambao ni nje ya wajumbe. Kazi ya wajumbe ukumbini itakuwa ni kuthibitisha tu kile kilichoamuliwa na wanachama huko nje.
👉Utaratibu huu unaweza kuratibiwa kwa kuunda Kamati za ngazi zote za kuratibu upatikanaji wa kiongozi anayekubalika zaidi Katika eneo husika kuanzia shina, tawi, kijiji, kata, Jimbo, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.
👉Hii itasaidia sana kuleta mvuto kwenye Chama pale ambapo kiongozi wa Chama anapokubalika na wanachama na wasio wanachama.
👉Pia viongozi wa Chama wawe ni wale wanaoendana na mabadiliko ya Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Kiitikadi, kwanini nasema hivi?
👉Kwasababu unaweza ukawekwa kukiongoza Chama huku umeshikilia itikadi ambazo hazikidhi haja ya Jamii iliyopo kwa wakati huo.
👉Kwa mfano, kwa sasa watu wengi wanaamini kukosekana kwa Maendeleo kunatokana na uzembe wa utendaji kazi kwa baadhi ya watu wa serikalini, Matumizi mabaya ya fedha za Umma kwa watu wasio waadilifu pamoja na kukithiri kwa rushwa.
👉Sasa hapa kama kiongozi wa Chama huwezi kuwaambia watu, endeleeni kukiamini Chama kwasababu sisi ni wazalendo.
👉Badala yake atahitajika kiongozi mwenye uthubu wa kupambana hadharani na watendaji wazembe na wasio waadilifu kwa kuwawajibisha bila kuwaonea aibu wala kuwaogopa lengo likiwa ni kulinda heshima ya Chama.
👉Kufanya Reform Kuna gharama zake, Kuna kuchukiana, Kuna kusemana, kukaripiana na kutokusifiana hovyo, lakini moja ya ahadi ya mwanachama wa CCM ni kwamba "Nitasema Kweli Daima Fitna Kwangu Mwiko".
👉Hii itakuwa njia ya kuleta mabadiliko ya kweli, kuamsha ari mpya, na kuvutia wanachama wapya ambao wanahitaji chama kinachoongozwa na maadili ya kweli na maendeleo.
👉Mwisho, CCM kujivunia na kutamba na Ukongwe isimaanishe kuwa ni Chama Kidumavu Kisichobadilika Bali imaanishe kuheshimu misingi iliyotufikisha hapa tulipo na misingi hiyo iwe chachu ya kutengeneza mustakabali wa Chama kwa kufanya 'Reforms'. Tofauti na hapo we are slowly digging our own grave for the future burial.