Pre GE2025 CCM inahitaji Mzee wa mafaili mwingine kama Mzee Mangula baada ya kujiuzulu kwa Komredi Kinana kuelekea 2025

Pre GE2025 CCM inahitaji Mzee wa mafaili mwingine kama Mzee Mangula baada ya kujiuzulu kwa Komredi Kinana kuelekea 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Huu ni mtazamo wangu binafsi wa mtu anayefaa kupokea kijiti Cha Komredi Kinana kama makamu mwenyekiti mpya wa CCM Taifa.

Kwanza, CCM inahitaji Mzee wa mafaili kama alivyokuwa Mzee Mangula. Kwa kuwa tunaelekea uchaguzi mkuu mtu mwenye sifa hiyo atakisaidia chama kuwafunga breki wanachama wanaoonekana kuenenda kinyume na taratibu za chama.

Pili, chama kinahitaji mtaalamu wa masuala ya chama na mwenye rekodi isiyo na shaka ya uwezo na uadilifu wake kwa chama.

Tatu, Chama kinahitaji mtu mwenye kuiishi vyema Imani na itikadi ya CCM kwa vitendo.

Nne, Chama kinahitaji mtaalamu mzuri wa propaganda za kisiasa na mwenye uwezo wa kutoa hoja na ufafanuzi.

Zaidi, Chama kinahitaji mtu mwenye karibu na misimamo thabiti kama ya Mzee Mangula kuelekea 2025.

PIA SOMA
- Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia
 
Hapa anaefaa ni Mizengo Pinda au Dr Mohamed Shein.
Msekwa au Warioba wangeweza se.a rekodi zao na misimamo imeyumba hapo kati.
Why not Anthony Mtaka (umri) , Kabudi, au Bashiru Ally? Itamsaidia Mwenyekiti kwenye kurudisha imani na kutuliza nyoyo zilizopata dhoruba baada ya kuondoka JPM.
Niliwahi kusema, bila ya Mwenyezi Mungu atakaewezesha kutumia karata ya JPM hamna mtu atatoboa 2025.
Miradi mkakati ilipuuzwa ili kuuwa legacy, unaona kilichotokea? Kaamua kuimaliza unaona wananchi walivyopokea?
 
Ahsante sana Ndugu Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutuletea Mzee Wassira , nahisi ni Mimi niliyemteua maana ana sifa zote nilizopendekeza
 
Back
Top Bottom