CCM inakuwaje Askari wetu wa Uhifadhi wanakosa nguo na vifaa vya uhakika hadi kufikia kuvaa kama vikosi vya Waasi/ Askari wa DRC?

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Nimesikitishwa sana kuona uvaaji wa Askari wetu wa uhifadhi wanaofanya operesheni ya kuua fisi huko mkoani Simiyu.

Inakuwaje nchi iliyofikisha Watalii Milioni 5 mwaka huu ambao wameingiza fedha za kigeni za kutosha kushindwa kuwanunulia nguo na vifaa stahiki askari wetu wa Wanyamapori?

Inakuwaje Askari wetu wanavaa buti za wakulima kama askari waasi wa Congo au Askari wa Jeshi la Congo? Tuseme tumeshindwa hata kuwanunulia buti za kiaskari?

Imenisikitisha sana kuona wahifadhi wetu wakivaa kama Askari wa kikosi cha Wazalendo kule Congo.

Angalieni wenyewe hapo chini👇

Aibu naona mimi!


Hapa 👇chini angalieni wenzenu wa Kenya Wildlife Services wanavyovalishwa vizuri. Tujifunze!


 
Unazungumzia TANAPA au maliasiri au Tawa au wapi
 
Kwa sababu kama ni TANAPA wanatakiwa wapunguziwe MSHAHARA Namana hakuna Askari Mwenye ELIMU ya form iv anayepata pesa nzuri kama askari wa TANAPA Wenda umekulupuka form iv aliyepitia JKT au Chuo Cha pasias mkoan Mwanza akiajiliwa TANAPA ANAKULA BASIC SALARY YA 1570000 ML. HALAFU POSHO KWA SIKU DORIA 80000 WAKATI JWT ANAYEANZA MSHAHARA 600000 POSHO 360000 + 100000 YA VINYWAJI WAPI NA WAPI
 
Maliasiri na Tawa Wana 450000+ 300000 basi TANAPA 1570000 NARUDIA TANAPA 1570000 NA POSHO 80000 KWA SIKU UKIENDA PORINI DORIA WIKI MBILI 80000*14= UNAPATA NGAPI HIYO POSHO
 
Sasa hawa wakipewa dili zuri na m23 si wanajiunga fasta?
 
Huu uzi haungolei mishahara. Unaongelea Serikali kuwajali kimavazi na vifaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…