Uchaguzi 2020 CCM inapaswa kuchukua hatua na kujibu hoja: Je, Maisha ya wananchi yameboreka kwa miaka mitano iliyopita?

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Wanabodi,

Ni dhahiri shahiri mikoa ya kusini ACT Wazalendo wanakitesa chama changu kwa hoja na makombora mazito ni kama wanatusambaratisha kabisa kwa kumtumia mbunge Bwege na mtu aitwaye Chaurembo

Mosi, hoja ya kuwa CCM ilipora korosho kinguvu na kutowalipa wakulima inatutesa sasa sana. CCM kuwaambia wananchi wakafuate pesa zao jeshini ni la aibu. Hii kauli inasemekana ilitolewa na wakuu wa wilaya na wakurugenzi huku wakifahamu wananchi wanaheshimu maeneo ya jeshi.

Utamuambiaje mkulima wa korosho afuate pesa Jeshini?

Pia hoja ya kuwa mashangazi watachakazwa imechukua sura mpya huko kusini. Pia kauli ya kuwa hata CCM ikipoteza majimbo yote kusini wataendelea na kazi imechukua sura mpya na kuwasha moto usiozimika kwa watu wa kusini

Hapa nashauri mambo mawili ili kukiokoa chama changu cha CCM

Mosi, tumtumie Mama Salma Kikwete kuomba radhi kwa kauli tata zilizotilewa hapo awali. Yeye watamuelewa kama Mama na mkazi wa huko.

Pili, tusijaribu kumtumia Waziri mkuu Majaliwa kuomba msamaha. Huyu huko Lindi anaitwa msaliti ingawa alikomaa kidogo wakati wa korosho, tutaharibu kabisa watu wana hasira sana.

Upande wa kaskazini mwa nchi CCM tunapigwa kwa hoja za ugumu wa maisha ya watu na Mamlaka ya mapato(TRA) kutumika kuwahujumu wafanyabiashara kwa kutumia Agency Notice. Hii hoja anaitumia Tundu Lissu na mpaka sasa inatutesa na kutuchakaza.

Watu ambao hawakujua sasa wanaamini Benk zetu sio salama sana kuweka pesa kwani zinaandikiwa barua na TRA kutoa pesa za wafanyabiashara hivyo kusababisha mzunguko wa pesa kuwa hovyo na maisha na ajira kuwa magumu na kutoweka.

Hapa nashauri Jambo moja tu,Hatuna haja ya kuongelea mambo ya reli, barabara kwenye mikoa kama Arusha, Mwanza au Shinyanga. Hawa watu wanahitaji habari za pesa na fedha tu sio porojo. Na wengi wana kubali maisha yamewatandika na wameyumba kipesa. Sera za kipesa kama Fiscal policy za kuongeza pesa kwenye mzunguko ndio za kuziongelea huko, CCM iseme itaongeza mzunguko wa pesa kupitia private sector partinership kwenye miradi na sio kutumia makampuni yake pekee ya kiserikali.

Tunazidi kuangalia hali ilivyo na tutatoa ushauri. Kuna mambo makubwa tumejifunza kwenye kampeni hizi na utofauti wa maslahi kikanda hasa kusini na kaskazini

Tulipokosea CCM tukubali makosa na kuwaomba wananchi msamaha. Nina hakika mambo mazuri mengi yamefanyika hata huko kusini na kaskazini, Mambo madogo ambayo yamewajaa wananchi moyoni ni kuomba msamaha na kusonga mbele.
 
..subiri mataga waje wakutukane.

..watakwambia wewe ulikuwa mpiga dili na mirija yako imekatwa ndio maana unalalamika maisha magumu.
Mkuu, Tumetofautiana uwezo wa kufikiri na Pia aina ya elimu tuliyopatiwa

Tunatofautiana aina ya malezi na misimamo ya waliotulea

Hao wanaoitwa mataga ndani ya chama changu cha ccm wengi ni choka mbaya haswa ni vijana wa elimu za kata na wazee wafia chama ambao hawaangalia mambo yanabadilika wao ni kupiga filimbi na matarumbeta kupata pesa mfukoni

Mambo mengi tunakishauri chama na yanafanyiwa kazi sana

Hao wanaoitwa mataga ndani ya chama hawana hoja wao wanajua kutukana ,mipasho na kuleta vichekesho na vituko

Kikubwa wapuuze wewe shauri chama kisonge mbele
 
..swali lako liliwahi kuulizwa miaka ya 80 wakati wa kampeni za Uraisi ktk nchi moja ya mabeberu.

..hebu angalia hapa jinsi huyu mgombea alivyohitimisha hoja zake akiomba kura za uraisi.

 
Inataka masikio ya kenge kuweza kukusikia.

Kwa ufupi bandiko lako litakuwa limewatia hasira sana wale misukule wa Lumumba - lb7. Hivi sasa watakuwa wanatweta wakisubiria maelekezo ya chakubanga.

Acha tusubiri kombora la kwanza. Tokea Lumumba au moja kwa moja tokea 'ikungu lya bashashi'.
 
Hiyo nitoe wazo kuwa tuiite ni Wanakulitafuta wanakulipata na wasipochafuka watajifunzaje, wakati ndio huu.
 
Maisha kuboreka au kuharibika ni uamuzi binafsi wa mtu mwenyewe. Kama msemo usemavyo: unaweza kumpeleka punda mtoni ila huwezi kumlazimisha kunywa maji.

Swali lingekua, serikali imeweka miundombinu thabiti ya mtu kujikwamua? Hapo jibu ni Ndiyo.
 
Kama hayajaboreka Lisu amgekuwa anafanya kampeni kwa ndege ya kukodi ya pesa alizochangiwa na wanachadema?

Si amgekuwa anatembea kwa miguu kufanya kampeni
 
Kama hayajaboreka Lisu amgekuwa anafanya kampeni kwa ndege ya kukodi ya pesa alizochangiwa na wanachadema?
Si amgekuwa anatembea kwa miguu kufanya kampeni
Haha hivi ndivyo umejibu hoja za mleta mada?!🤔

And you think you're among of those who can give constructive ideas for the party's nomination towards the coming election?!
Kweli mataga bure kabisa!
 
Maisha kuboreka au kuharibika ni uamuzi binafsi wa mtu mwenyewe. Kama msemo usemavyo.. unaweza kumpeleka punda mtoni ila huwezi kumlazimisha kunywa maji.

Swali lingekua, serikali imeweka miundombinu thabiti ya mtu kujikwamua? Hapo jibu ni Ndiyo.
Mfumo wa tozo la TRA umewatoa wengi kwenye biashara hasa watu wa kipato cha wastani.
 
Mfumo wa tozo la TRA umewatoa wengi kwenye biashara hasa watu wa kipato cha wastani.
Tegemea kura za hasira kutoka kwa;
Wafanyabiashara walioathirika na tozo za kodi zisizokuwa na kichwa wala miguu
Walioathiriwa na issue ya vyeti feki
Walioathiriwa na bomoabomoa kimara mpaka mbezi kwa double standards alozozionesha mgombea wa CCM kwa watu wa Mwanza waliopaswa nao wabomolewe kupisha upauzi wa barabara. Hapa alionesha ukabira na upendeleo wa wazi kabisa
Wazee wastaafu waliokosa pensions zao mpaka sasa
Wanafunzi wa vyuo vikuu walioathiriwa na mfumo ulioingiliwa wa mikopo ya elimu ya juu awamu hii
Wakulima wa mazao kama korosho, mbaazi na pamba n.k
Kizazi kipya (vijana) wanaoona mambo yanavyoenda nchini
Wasio na ajira baada ya kumaliza elimu ya juu
Watumishi wa umma maana mpaka wanapewa barua za kuhudhuria mikutano ya CCM na wasipoenda watakiona
Wanaccm walioathiriwa kwa sera na mipango na maamuzi mbalimbali yaliyofanyika ndani ya chama.

Wanaochukizwa na kauli za umimi (ninafanya/nitafanya baada ya kauli za serikali inafanya/itafanya) kebehi, ubabe, zisizo na utu wala hekima mbele ya halaiki sometimes na ulevi wa madaraka wa mgombea wa chama tawala
Wimbi kubwa la maaskari wa vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ambao wako tayari kuishi kwa utaratibu na kanuni za viapo vyao (kisirisiri)

Kama chama kina think tank wa ukweli cha kwanza wangekuwa na mikakati ya kuwarejesha au kuwaweka sawa hawa na si kila siku sera za SGR, kuongeza ndege na barabara nchi nzima as if awamu zilizopita walikuwa hawafanyi kitu.
Kinachotegemea ni bao la mkono; Tume + vyombo vya dola

Wananchi wengi hawako tayari kwa huo ujinga sasa, wanataka maamuzi yao yaheshimiwe na vuguvugu hili litaanzia visiwani kusambaa mpaka bara.
Na hapo ndipo Tanzania nzima itakapoimba nyimbo moja na kuitafuta amani ya kweli
 
Tutashinda tu kwa mbinu za kisasa zaidi,Hatutaiba kura bali tutashinda kwa shikwambi
 
Tutashinda tu kwa mbinu za kisasa zaidi,Hatutaiba kura bali tutashinda kwa shikwambi
Cha msingi iwe njia ya wazi ambayo watanzania wataridhika. Hofu yangu ni pale maridhio yasipokuwepo. Wote tunaipenda nchi yetu kwa mustakabali wetu na wa vizazi vyetu vya baadae.
 
Tangu nchi iumbwe mtza anaishi maisha magumu kuliko tawala zote kwa nyerere yalikuwa magumu lkn haifikii hii wengi wamesahau hata kunywa chai tu kitambo wanabahatisha mlo mmoja tu, familia zinasambaratika baba hana pesa ajira hakuna biashara hazitoki nyumbani pesa inatakiwa ili kumudu maisha kelele zinazid familia inasambaratika yote sababu tu ya MTU mmoja kuharibu uchumi kavimbiwa kodi zetu kaamua kuwatesa watz.

Mungu ni upendo kuwapenda watu kanisani wanafata nn kumdhihaki Mungu. Watu wamebambikwa kesi kwa sababu ya elf20 wapo ndani miaka eti ushahidi ujakamilika familia zao zimesambaratika.

Watz mkirudia kosa mmekwishaa mtalimia kucha safari hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…