GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Wanabodi,
Ni dhahiri shahiri mikoa ya kusini ACT Wazalendo wanakitesa chama changu kwa hoja na makombora mazito ni kama wanatusambaratisha kabisa kwa kumtumia mbunge Bwege na mtu aitwaye Chaurembo
Mosi, hoja ya kuwa CCM ilipora korosho kinguvu na kutowalipa wakulima inatutesa sasa sana. CCM kuwaambia wananchi wakafuate pesa zao jeshini ni la aibu. Hii kauli inasemekana ilitolewa na wakuu wa wilaya na wakurugenzi huku wakifahamu wananchi wanaheshimu maeneo ya jeshi.
Utamuambiaje mkulima wa korosho afuate pesa Jeshini?
Pia hoja ya kuwa mashangazi watachakazwa imechukua sura mpya huko kusini. Pia kauli ya kuwa hata CCM ikipoteza majimbo yote kusini wataendelea na kazi imechukua sura mpya na kuwasha moto usiozimika kwa watu wa kusini
Hapa nashauri mambo mawili ili kukiokoa chama changu cha CCM
Mosi, tumtumie Mama Salma Kikwete kuomba radhi kwa kauli tata zilizotilewa hapo awali. Yeye watamuelewa kama Mama na mkazi wa huko.
Pili, tusijaribu kumtumia Waziri mkuu Majaliwa kuomba msamaha. Huyu huko Lindi anaitwa msaliti ingawa alikomaa kidogo wakati wa korosho, tutaharibu kabisa watu wana hasira sana.
Upande wa kaskazini mwa nchi CCM tunapigwa kwa hoja za ugumu wa maisha ya watu na Mamlaka ya mapato(TRA) kutumika kuwahujumu wafanyabiashara kwa kutumia Agency Notice. Hii hoja anaitumia Tundu Lissu na mpaka sasa inatutesa na kutuchakaza.
Watu ambao hawakujua sasa wanaamini Benk zetu sio salama sana kuweka pesa kwani zinaandikiwa barua na TRA kutoa pesa za wafanyabiashara hivyo kusababisha mzunguko wa pesa kuwa hovyo na maisha na ajira kuwa magumu na kutoweka.
Hapa nashauri Jambo moja tu,Hatuna haja ya kuongelea mambo ya reli, barabara kwenye mikoa kama Arusha, Mwanza au Shinyanga. Hawa watu wanahitaji habari za pesa na fedha tu sio porojo. Na wengi wana kubali maisha yamewatandika na wameyumba kipesa. Sera za kipesa kama Fiscal policy za kuongeza pesa kwenye mzunguko ndio za kuziongelea huko, CCM iseme itaongeza mzunguko wa pesa kupitia private sector partinership kwenye miradi na sio kutumia makampuni yake pekee ya kiserikali.
Tunazidi kuangalia hali ilivyo na tutatoa ushauri. Kuna mambo makubwa tumejifunza kwenye kampeni hizi na utofauti wa maslahi kikanda hasa kusini na kaskazini
Tulipokosea CCM tukubali makosa na kuwaomba wananchi msamaha. Nina hakika mambo mazuri mengi yamefanyika hata huko kusini na kaskazini, Mambo madogo ambayo yamewajaa wananchi moyoni ni kuomba msamaha na kusonga mbele.