Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Muda sio mrefu madai ya wanaCCM yataibuka na kuwekwa wazi, ikiwa ni kilio na malalamiko juu ya uwezo wa Mwenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa, kwamba anashindwa kukiongoza chama, sababu za msingi hazikuwekwa wazi ni nini hasa kinachomfanya mwenyekiti huyo mpya ambaye hajamaliza hata mwaka mmoja kuonekana hatoshi, lakini wachambuzi wachache wa masuala hayo walidai ni ukiukwaji wa demokrasia, ukiukwaji wa utawala bora na kukiuka sheria na taratibu, kutokusikiliza ushauri na kuendesha nchi kwa hisia, mapenzi, chuki na matakwa binafsi bila kufuata utaratibu.
Kubwa zaidi; ndani ya chama hicho kuna ubadhilifu mkubwa wa fedha ambao mwenyekiti huyo ameshindwa kuushughulikia na kuudhibiti, kuna matumizi mabaya ya fedha ambayo yanazidi kukiondolea chama hicho sifa, kuna vyanzo vya mapato vya chama hicho ambavyo havijulikano, yaani hewa, lakini wadadisi wanavyosema kuwa inawezekana fedha hizo zinatoka serikalini na zinaingizwa kwenye chama hicho tayari kwa kuanza rasmi kazi za chama.. ambapo wachache hao wazalendo walidai kuwa chama hakipaswi kuihujumu mali ya umma kwani hata kama wananchi hawatakichagua tena, ni halali kwani ni kweli kimepoteza sifa, mvuto na nguvu kiliyokuwa nayo awali.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho ambao nilipata kuwadadisi kwa kufanya mazungumzo nao kwa njia ya VoiP, walinihakikishia kuwa chama hicho mpaka sasa hakina Dira, na waliyakumbuka maneno ya marehemu Horace Kolimba.
Malalamiko na manung'uniko hayo ni ya chini kwa chini yaliyodumu kwa muda mrefu sasa, yaliyopelekea maafisa kadhaa kwenye chama hicho kuondolewa nyadhifa zao na kuonywa vikali kutokuzungumza chochote, pia wengine kuamua kuachia nafasi zao bila taarifa rasmi..Lakini mwengi wamedai uwezo wake ni mdogo kushika madaraka makubwa mawili, yaani zile kofia mbili.
Taarifa kamili nitazileta kadiri nitakavyozipata kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya Chama hicho, chama cha mapinduzi CCM.