Naam zingatia mada tajwa hapo juu,
Salaam,
Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Sisi wataalamu wa hizi kazi tunafahamu kwamba, ili chama cha siasa kiweze kuendelea na kibaki kuongoza dola ni jambo moja tu itabidi lifanyike, nalo ni huduma za kijamii ambazo serikali itakuwa imepeleka kwa wananchi katika kipindi cha baada na kabla ya uchaguzi.
Nipende kutumia fursa hii kukujuza ndugu mwananchi kuwa, hakuna chama duniani, hata kingetumia vyopa, vifaru na nyuklia kubaki madarakani huku kikiwa hakitoi huduma vyema kwa wananchi wake halafu kikaendelea kuwepo. Hakipo, na kikiwepo basi hakiwezi kuwa na maisha marefu.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Chama Cha Mapinduzi kingekuwa hakileti huduma za kijamii mtaani basi kingetolewa madarakani na wananchi wenyewe (sio kwa kutangazwa kushindwa uchaguzi na tume) tangu mwaka 1995 tulipoanza mbio za vyama vingi.
Hivyo ni kusema kwamba, uhai na mdundo wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi unaouona leo ni matokeo ya huduma za kijamii ambazo chama hicho kimeziwasilisha kwa wananchi.
Yeyote yule, hatoweza kuwashawishi wananchi kukipiga chini Chama Cha Mapinduzi eti kwa kasoro tu ambazo chama chochote cha siasa kingeshika dola kingekuwa nazo. Ikiwa chama hicho kina kasoro, na haziwezi kukosa, tutazifanyia kazi ruwayda ruwayda yaani taratiibu taratiibu.
Ujenzi wa taifa na chama hautosimama hadi dunia itakaposimama, changamoto mpya zitaendelea kuwepo hadi dunia itakaposimama, linapobainika tatizo ama changamoto ya kimaendeleo hiyo itaongezwa tu kwenye list ya mambo yanayohitaji Suluhu na haiwezi kutambulika kama a
disqualifying factor kwa Chama Cha Mapinduzi. never, ever, forever.
Ni uongo kudhania kwamba, pale inapotokea changamoto eti Chama Cha Mapinduzi hawapendi kutekeleza jambo fulani au ndio wasababishi, ili tatizo lipate Suluhu ni lazima liwepo kwanza, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kulihudumia taifa hili mpaka kiyama kitakaposimama, na hakitashinda uchaguzi kwa kutegemea tume, polisi wala Katiba ila ni huduma za kiraia zinazowafikia wananchi.
Kwa Bahati mbaya nimekosa muda wa kuambatanisha data za tafiti za kisomi zinazofungamana na andiko langu, hata hivyo niwaombe wale wenye angalau orodha ya miradi iliyotekelezwa na Chama tangu 2020 waipaste hapa ili tujue tulipo na tunapoelekea.
[email protected]