CCM jaribuni kutumia akili na busara kuelewa maoni ya upinzani. Kuhoji sio kupinga

CCM jaribuni kutumia akili na busara kuelewa maoni ya upinzani. Kuhoji sio kupinga

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Nimeshangaa kuona kwamba wengi wa wanachama wa CCM pamoja na viongizi wao wamekuwa wakiwashambulia watu wa upinzani kila wanapotoa maoni juu ya miradi kama SGR, ndege za ATC, mradi wa umeme wa SGR, flyover nk

Utakuta mtu anasema kwa nini unapanda ndege za ATC alizonunua Magufuli wakati mlipinga?

Huu ni upotoshaji wa makusudi au watu kuwa wavivu kutumia akili na busara zao SGR kwa mfano, mtu akiuliza mbona mradi huu unachelwa anajibiwa wewe ni mpinzani kwa nini unauulizia? Kuna watu hata walionyesha picha ya Zitto akishuka ndege ya ATC wakidai kwa nini anapanda ndege na yeye alikosoa ununuaji wa hizo ndege?

NI wazi kwamba wale wote, mashabiki na viongozi wa CCM, wenye mtazamo huu wana tatizo katika kufikiri. Ni sawa na mtu anapiga kelele kwamba usije kwenye harusi yangu kwa kuwa uliniambia nisiendekeze ngono kuna ukimwi!

NIngeshauri mashabiki wa CCM na viongozi wao wajaribu kutumia akili na busara katika kuelewa maoni yanayotolewa na viongozi wa upinzani juu ya maendeleo ya Tanzania. Viongozi wa upinzani wanaposhauri kwamba CCM msiendekeze ngono mnaweza kuambuizwa ukimwi, hawawakatazi CCM kuoa au kuolewa.

Na pale viongozi wa upinzani wanaposema taratibu zilikiukwa katika kutekeleza miradi kama ya kununua ndege au SGR, hawana maana hawapendi vitu hivi vijajengwa nchini au kwamba hawatavitumia. Wanachomaanisha ni kwamba vifanyike kwa utaratibu wa kisheria na ulioainishwa katika taratibu za manunuzi au miradi ya Serikali, kutia ndani Bunge kuhusishwa pale inapostahili.

Mtu mmoja kuwa anaamua juu ya miradi mikubwa peke yake kwa msisimko tu wa kisiasa bila kufuata utaratibu wa matumizi ya fedha za serikali kama kupeleka Bunge likaiizinishe matumizi ya fedha za miradi hiyo, huko ni sawa na kufanya ngono za uzembe - ni wazi watu wenye busara watakuonya kwamba usiendekeze ngono za namna hiyo kuna hatari ya UKIMWI.

Na wakikuambia hivyo utakuwa na akili ya mwendawazimu sana kuanza kupiga kelele kwamba umekatazwa kuoa au kuolewa kwa kuwa umeambiwa usiendekeze ngono, au kuwakataza waliokuonya wasije kwenye harusi yako kwa kuwa walisema usiendekeze ngono.

NIna uhakika Watanzania tuna akili na busara, basi tujitahidi kuzionyesha katika kauli zetu.
 
Hapana umeposha mkuu.
wapingaji wa maendeleo wanasema hivi"hawataki maendeleo ya vitu"kipaumbele chao ni maendeleo ya watu.
 
Kwako wewe Moderator wa thread hii

Title ya thread hii ilikuwa" CCM jaribuni kutumia akili na busara kuelewa maoni ya upinzani, wanaposema msiendekeze ngono kuna ukimwi hawawakatazi kuoa au kuolewa"

Mie sioni kwa nini Moderator uliamua kubadilisha, kwa sababu tungo tata iliyokuwa imetumika kwenye titke ina mambo ya msingi katika kuisaidia jamii kwa ujumla na kuweka mvuto maalum kwa wasomaji kuisoma thread.

Tatizo lenu hapo ni nini? Kwamba mashabiki wa CCM na viongozi wao hawapaswi kushauriwa kutoendekeza ngono? Mie ninashauri mrudishe title niliyokuwa nimeandika. Kama mnaona hayo hayapaswi kutamkwa kwa CCM ni kashfa kwao basi ifuteni thread yote maana binafsi naona mmeanza kuvuka mipaka ya ku-moderate

Tunailalamikia serikali kukandamiza uhuru wa maoni na vyombo vya habari pamoja na Jamii Forum, na nyie Moderatotrs wa JF mmeanza kufanya kwetu yale yale tunayoilalamikia serikali. Sasa hii kitu gani?
 
Hapana umeposha mkuu.
wapingaji wa maendeleo wanasema hivi"hawataki maendeleo ya vitu"kipaumbele chao ni maendeleo ya watu.
Kusema hatutaki maendeleo ya vitu haina maana hawataki vitu, ndio maana nikasema mtu akikuambia usiendekeze ngono hana maana usioe au kuolewa
 
Hata hizo ndege watu wanapanda maana fast jet ilihujumiwa. Ikumbukwe nauli ya fast jet ilikuwa chini ya hizi za ATCL. Iwapo fast jet ingeachwa ishindane bado watu wangepakia ndege watakazo.
Jinga nyie fast jet ilikuwa inaendeshwa kihuni hata tozo zingine hailipi sasa hapo ilikuwa inahujum nchi wewe ndio unaona sifa?
Mpaka sasa hivi wanadaiwa hawajalipa
Walipe madeni wasepe.
 
Jinga nyie fast jet ilikuwa inaendeshwa kihuni hata tozo zingine hailipi sasa hapo ilikuwa inahujum nchi wewe ndio unaona sifa?
Mpaka sasa hivi wanadaiwa hawajalipa
Walipe madeni wasepe.
Aaah Mkuu, ukinikumbusha Fastjet hata machozi yananitoka. Niliwapandisha wazazi wangu ndege na hawakutemea wala mie sikutegemea wangepanda ndege maishani mwao. Wakaja watu na Bombadia zao wakaikomesha FastJet, halafu wanataka tuwaimbie nyimbo za sifa!
 
Jinga nyie fast jet ilikuwa inaendeshwa kihuni hata tozo zingine hailipi sasa hapo ilikuwa inahujum nchi wewe ndio unaona sifa?
Mpaka sasa hivi wanadaiwa hawajalipa
Walipe madeni wasepe.

Bora fast jet, nenda kwenye msafara kwa kampeni za ccm uone magari na raslimali nyingine za umma zinavyotumika kwa faida ya ccm kinyume na sheria, kisha uje hapa uwanyooshee kidole fast jet.
 
Magufuli aliwahi kusema "mimi ukinishauri ndio umeharibu kabisaaaa maana hatafanya kile unachomshauri"

Magufuli aliahidi kuufuta na kuua upinzani kwa Mabavu ya police na vyombo vyake,
Yeye hajui kwamba upinzani unajengwa mioyoni mwa watu.

"Aliwahi kuwaambia wakurugenzi/ NEC.
Nimekupa kazi.
Nakupa mshahara.
Nakupa posho.
Nakupa gari nzuri.
Nakupa nyumba nzuri alafu umtangaze mpinzani kashinda iiii...."

Hakuna binadamu timamu kabisa asiyekuwa mpinzani othewise ni Roboti
 
Kwani una dhani hawana akili? Au macho?? Wame weka hivyo vitu rehani wana tumia makalio kufikiri kwa muda..
 
Hivi sasa haishangazi tena kuona Wanachama wa CCM na viongozi wao wanashambulia wapinzani kila wanapotoa maoni yao kuhusu miradi kama SGR, Stiegler's Gorge au kununua madege ya ATCL kwa sababu wenzetu kwa ujumla wao hawako sawa upstairs. SGR ilikuwa ifike Morogoro siku nyingi tu tamko la mwisho likiwa ingekamilika mwezi Novemba, 2019 ni mwaka sasa haijulikani imefika wapi wala hawasemi tena chochote kuhusu reli hiyo.

Stiegler's Gorge bado wanafanya maandalizi ikiwa ni pamoja na kujenga mchepuko kubadilisha mkondo wa maji ya mto ili kuwezesha kuanza kujenga ukuta wa bwawa kwenye mto Rufiji. Miradi hii miwili sasa hivi kinachosemwa ni asilimia ya kazi iliyofikiwa na trilioni ya fedha zilizotumika takwimu ambazo hazina maana yoyote wala wananchi hawataki kusikia bali wanataka tu huduma zitakazotolewa na miradi hiyo.

Madege ya Magufuli yamenunuliwa na kodi za wananchi wote ikiwa ni pamoja na wa Upinzani kwa hiyo Wana haki ya kusafiri na ATCL, Shirika la Umma lakini hiyo haiwafanyi wasihoji kama kuna kitu hakiko sawa. Kuna makosa mengi yalifanywa kwenye ununuzi wa madege lakini kosa kubwa kabisa ni kuwa yalinunuliwa na Rais mwenyewe ambaye hadi sasa hajatambua lilikuwa kosa kujihusisha na ununuzi huo ndo maana hajatumbuliwa yeyote. Bahati mbaya sana Chama chake ambacho kingeweza kumkemea au kuanzisha mchakato wa kumwajibisha lakini kimekuwa msitari wa mbele kuunga mkono juhudi za kununua zaidi. Kosa lingine kubwa ni kulikuwa na haja gani kununua madege miaka kadhaa iliyopita kwa matumizi miaka kadhaa ijayo?

Awamu ya Tano inataja miradi mingi sana iliyotekelezwa lakini hawaonyeshi iko wapi na Ina hali gani walianza na nchi ya viwanda ikiwa ni pamoja na viwanda 4000 vya cherehani 4 vya Mwijage lakini tungali tunavaa mitumba, wakaja na viwanda 100 kila Mkoa kwangu sijaona hata kimoja. Bomba la mafuta toka Uganda mpaka Tanga lilikuwa liwe limekamilika lakini juzijuzi Rais Museveni akaja kuongeza nguvu kwenye kampeni ya mwenzake na kuahidi Bomba litaabza kujengwa ingawa Kampuni ya Total tawi la Tanzania ambayo ilikuwa ijenge hilo Bomba imeanza kufunga virago.
 
Wanajua wanachokifanya na madhara yake makubwa. Hawajali maslahi ya nchi wala wananchi. Ndio maana hoja zikishindwa kujibiwa zinakuja kauli za "pambana na Hali yako"; "serikali haiwezi kukuletea pesa au ugali mezani kwako"; "Mbowe na Lissu hawawezi kukusaidia kitu"; n.k.

Hiyo miradi imefanywa "top secret"; haikaguliwi na inatetewa kisiasa. Taaluma zimewekwa kando. Kwa kifupi, hazina inakaushwa kuiweka hiyo miradi hai hadi siku janja nyingine itakapopatikana kuwaweka sawa wananchi wanaochukuliwa kama mazuzu. Hakuna mwanataaluma asiyeelewa kuwa kwa jinsi ATCL "inavyofufuliwa" itakula pesa ya serikali mpaka mwisho wa uhai wake - yaani mwaka itakapouzwa au kuvunjwa. SAA sasa hivi imebakia na option ya kukabidhiwa kwa mwendeshaji yoyote mwenye uwezo atakayekuwa tayari kuiendesha hata bila kulipa kitu. Naona ET wameshatoa ofa.
 
Kazi tunayo nchi hii badala ya kwenda mbele tusije tutajikuta tunarudi nyuma kwa kasi sana nakuanza kutafuta aliyetuloga. Tuombee hii miradi isije ikawa white elephant. Kwa sasa hivi sijui kweli kwamba hizi ndege huko mbele zitanufaisha taifa au zitaendelea kula kodi zetu maana uendeshaji wa ndege ni gharama kubwa.
 
Hata hizo ndege watu wanapanda maana fast jet ilihujumiwa. Ikumbukwe nauli ya fast jet ilikuwa chini ya hizi za ATCL. Iwapo fast jet ingeachwa ishindane bado watu wangepakia ndege watakazo.
Monopoly has never been the best practices in managing businesses competitively.
 
Hata hizo ndege watu wanapanda maana fast jet ilihujumiwa. Ikumbukwe nauli ya fast jet ilikuwa chini ya hizi za ATCL. Iwapo fast jet ingeachwa ishindane bado watu wangepakia ndege watakazo.
Nyuma ya fastjet unafahamu kulikuwa na nini? Kwa nini ndege yao moja imekamatwa mpaka sasa? Acha kupinga pinga na ushabiki.
 
Hata hizo ndege watu wanapanda maana fast jet ilihujumiwa. Ikumbukwe nauli ya fast jet ilikuwa chini ya hizi za ATCL. Iwapo fast jet ingeachwa ishindane bado watu wangepakia ndege watakazo.
Jiwe hapendi ushindani kabisa, ukiangalia kilichowatokea fastjet utaelewa kwanini hata fomu ya Uraisi fisiume ilikuwa moja.
 
Back
Top Bottom