Mkuu,
Huyu Oscar Mukasa mimi namfahamu ingawa si sana. Anakaa Tabata Maflat ya NSSF na ni kijana mfupi mweusi. Anavaa miwani.
Nimjuavyo mimi na kwa muonekano, ni kijana wa kawaida ambaye huwezi kudai kuwa ana maisha ya juu. Ana maisha ya kawaida tu. Ndiyo maana Masanilo alipodai ana nyeti zake za ufisadi nilitaka kujua ni zipi. Bahati mbaya kaingia mitini hajibu maswali.
Amewahi kufanya kazi na Dr. Hassani Mshinda wa COSTECH kabla hajaamia hapo, na ni moja wa vijana ambaye yuko makini katika kazi yake.
Habari zake za kuingia katika siasa nilianza kumsikia toka wakati kulipokuwa na Kesi mahakama kuu ya uchaguzi wa jimbo la Bihalamulo. Alikuwa na nia ya kugombea na alidai wazee wengi wa kule kijijini walikuwa wanamuunga mkono kuliko wengine waliokuwa na azma ya kugombea.
Ngoja kesho, nitaongea naye nimsikie ni nini kilichojili na kisha tutahabarishana.