CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar

CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar

Haya . . . Kanyaga twende . . . .

Source: UPL-Homepage


Oscar Mukasa: Kijana anayedhamiria kutumia

NA EPSON LUHWAGO

KUNA msemo unenao kuwa mjenga nchi ni mwananchi. Msemo huo ambao umezoeleka miongoni mwa watu una busara ya namna ya kipekee na una maana kwamba aendeleo yatatokana na wananchi wenyewe katika jamii husika kwa kutumia nyenzo na rasilimali zilizopo wakiwemo watu. Ni msemo ambao umekuwa ukitoa changamoto ya aina yake kwa Watanzania kutaka kutumia juhudi, maarifa na uwezo wao katika kuleta maendeleo ya jamii na taifa kwa jumla.


Kutokana na ukweli huo, kuna Watanzania lukuki wanaosoma ndani na nje ya nchi ama kwa gharama zao au za serikali ili pindi wanapomaliza watumie elimu yao katika maendeleo ya taifa. Pamoja na ukweli huo, ni Watanzania wachache ambao wamekuwa na mtazamo chanya katika kushiriki kwao kutoa mchango wao kuendeleza jamii zao ili kuondokana na umasikini unaowakabili.


Oscar Mukasa, ameamua kuvunja ukimya na kuwa mfano kwa vijana wengine wasomi wa Tanzania katika kushiriki kwa vitendo kutumia elimu na maarifa yake kuisaidia jamii katika maendeleo. Akizungumza na mwandishi wa makala hii ofisini kwake Mikocheni, Dar es Salaam, juzi, Mukasa alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na kuamini kuwa yeye ni sehemu ya jamii, hivyo anahusika moja kwa moja kuibadilisha na kuwa na maendeleo endelevu.


"Matatizo ya nyumba hayamalizwi bila juhudi binafsi za wenye nyumba. Kadhalika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, haziwezi kutoka kwenye kundi la dunia ya tatu wala kuondokana na umasikini, ujinga na maradhi, isipokuwa kwa juhudi za watanzania wenyewe, kwa nafasi zao, taaluma zao, na dhamira zao njema," alisema.


Mukasa, mwenye umri wa miaka 38 na mtaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika afya na utabibu, alisema hiyo ndiyo inayomgusa zaidi katika kujitoa kwake kushiriki katika mapambano dhidi ya matatizo yanayoikabili jamii.


Alisema kwa muda mrefu amekuwa akiwaza nini hasa suluhisho la kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi wengi hasa wa vijijini huku Watanzania wengi waliosoma wakiyapa kisogo matatizo hayo.


Mukasa, mwenye shahada ya uzamili katika teknolojia ya habari na mawasiliano, alitoa mfano wa sehemu anakotoka, wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kwamba wananchi wanaishi katika hali ngumu licha ya kuwa na rasilimali lukuki.


"Inaumiza kuona miaka nenda miaka rudi, jamii iliyotulea inagubikwa na matatizo mengi mno. Nadhani wakati umefika sasa wa kushiriki kuyatatua kwani ni sehemu ya jamii ile," alisema.


Mukasa, ambaye hivi karibuni anatarajia kuhitimu shahada ya uzamivu (PhD) nchini Uswisi, aliongeza: "Sisi kama vijana taaluma na nafasi zetu zitakuwa na maana zaidi kama zinatoa mchango moja kwa moja katika kutatua matatizo ya jamii tunazotoka."
Alisema wapo vijana wengi wasomi fani mbalimbali kama vile afya, elimu na uhandisi hivyo wanatakiwa kupata fursa kushiriki katika kuiletea jamii maisha bora, kwa kutumia taaluma zao.


Kwa mujibu wa Mukasa, matatizo ya maji, upungufu wa walimu katika shule za sekondari na msingi, na upungufu wa watumishi wa afya ni baadhi ya mambo yanayohitaji msukumo wa kutosha ili kuyapatia ufumbuzi.


"Panapokuwa na ubunifu ufumbuzi wa masuala haya unawezekana kwa kiasi kikubwa sana. Kinachohitajika ni kuhakikisha unakuwepo uwakilishi mzuri katika vyombo vya maamuzi," alisema.


Anaamini kwamba elimu, ambayo kwa dunia ya sasa ni silaha muhimu katika kuongoza mpambano dhidi ya umasikini, hivyo Watanzania wasomi hawana budi kuitumia ipasavyo katika kushughulikia matatizo hayo.


Kuhusu njia atakazotumia kutimiza malengo yake ya kupambana na umasikini kwa maeneo ya Tanzania yaliyonyuma, alisema jambo kubwa ni elimu yake na uzoefu alio nao.


"Nina uzoefu wa kuandika na kusimamia miradi ya maendeleo katika nyanja za afya. Ni suala la kutumia ujuzi na uzoefu huo kwa kupanua wigo wa fikra," alisisitiza.


Alisema hivi sasa anashirikiana na rafiki zake wa Italia, Canada na Singapore kuandika miradi maalumu katika nyanja tofauti, hivyo lengo lake kuelekeza nguvu hizo katika maeneo yanayohitaji miradi hiyo, Biharamulo ikiwemo.


"Tayari tumekuwa na mazungumzo na wafadhili mbalimbali ambao wameonesha nia ya dhati kufadhili miradi hii. Tutakapokuwa tayari hivi karibuni nitaiweka hadharani ili umma uelewe," aliongeza.


Katika kuhakikisha azma hiyo inafanikiwa, mpango shirikishi baina yake na wananchi wa wilaya ya Biharamulo utakuwa dira kuu ya mafanikio.


Kwa mujibu wa Mukasa, wilaya hiyo ina vijana wengi waliosoma hivyo kinachohitajika ni kuwakusanya pamoja na kutumia elimu na taaluma zao katika kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hao.


ALIKOTOKA


Mukasa aliyezaliwa Julai 1970, ni mtoto wa tano kati ya 10 katika familia ya Mzee William Mukasa na Mama Apolonia Mukasa. Alizaliwa katika kijiji cha Rukaragata kilichopo takriban kilometa tatu kutoka mji Biharamulo, barabara ya kwenda wilayani Ngara.
Baba yake ni mtumishi wa umma mstaafu ambaye amewahi kuwa Ofisa Afya wa wilaya ya Biharamulo kati ya mwaka 1977 na mwaka 1987 kabla ya kuwa Ofisa Afya wa mkoa wa Kagera kati ya mwaka 1987 na 1992 alipostaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya hapo, aliwahi kuwa mtumishi wa umma sehemu mbalimbali nchini.


Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Biharamulo kuanzia mwaka 1978 mpaka 1984 na baada ya hapo alichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Nyakato iliyopo nje kidogo ya mji wa Bukoba.

Mwaka 1989 alichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondari ya Pugu, Dar es Salaam katika masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabati.


Mwaka 1991/1992, alitumikia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria katika kambi za Ruvu mkoani Pwani na Maramba, Tanga.


Baada ya hapo, mwaka 1993 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya kwanza ya sayansi katika hisabati na takwimu.


Hakuishia hapo kwani baada ya kufanya kazi kwa muda katika Kituo cha Utafiti na Maendeleo ya Afya cha Ifakara, alikwenda Uholanzi kwa masomo ya shahada ya uzamili ya sayansi katika Teknolojia ya Mawasiliano na Habari katika tiba (MSc in Medical Informatics) kwenye Taasisi ya Sayansi za Afya. Alihitimu shahada hiyo mwaka 2001.
Hivi sasa ni mwanafunzi wa masomo ya shahada ya uzamivu katika teknolojia ya habari na mawasiliani kwenye fani ya afya katika chuo kikuu cha Basel, Uswisi.


Mfumo wa masomo anayosomea ni ya mazoezi ya vitendo na ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya masomo. Alisema mfumo huo unamwezesha mwanafunzi kuendelea na kazi pia na unatoa nafasi ya kuoanisha masomo ya nadharia na vitendo.


Licha ya kuwa mtaalamu aliyebobea katika fani ya TEKNOHAMA, Mukasa ni kijana mwenye uelewa mpana kutokana na bahati aliyoipata katika kutembelea sehemu mbalimbali duniani.


Baadhi ya nchi alizotembelea kutokana na masomo, warsha na ziara za kikazi ni ndani na nje ya bara la Afrika, Kenya, Uganda, Ghana, Afrika ya Kusini, Uholanzi, Scotland, Uingereza, Ethiopia, Canada, Italia, Uswisi na Vietnam.


Vile vile amekwishafanya machapisho ya kisayansi 10 na kuongoza, kusimamaia, au kuandika miradi takriban 13 ya kitaalamu iliyostahili na kupata ufadhili mkubwa wa fedha.
Mukasa hayuko mbali sana kijamii kwani ni mjumbe wa kamati ya usimamizi na tathmini ya masuala ya kitaalamu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Vile vile ni mwakilishi wa umoja wa kimataifa wa wanataaluma wa sayansi na teknolojia ya habari na mawasilino katika afya kanda ya Tanzania.

Hatua aliyoichukua Mukasa ni ya kuigwa na vijana wengine wa Tanzania waliobahatika kupata elimu. Changamoto kwa vijana na wasomi wengine nchini ni kushiriki kikamilifu katika kutatua matatizo yanayozikabili jamii kwa kuwa na wao ni sehemu ya matatizo hayo.

 
1. Mukasa, ambaye hivi karibuni anatarajia kuhitimu shahada ya uzamivu (PhD) nchini Uswisi,

2. ALIKOTOKA


3. Mukasa aliyezaliwa Julai 1970, ni mtoto wa tano kati ya 10 katika familia ya Mzee William Mukasa na Mama Apolonia Mukasa. Alizaliwa katika kijiji cha Rukaragata kilichopo takriban kilometa tatu kutoka mji Biharamulo, barabara ya kwenda wilayani Ngara.

4. Baba yake ni mtumishi wa umma mstaafu ambaye amewahi kuwa Ofisa Afya wa wilaya ya Biharamulo kati ya mwaka 1977 na mwaka 1987 kabla ya kuwa Ofisa Afya wa mkoa wa Kagera kati ya mwaka 1987 na 1992 alipostaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya hapo, aliwahi kuwa mtumishi wa umma sehemu mbalimbali nchini.

5. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Biharamulo kuanzia mwaka 1978 mpaka 1984

6. na baada ya hapo alichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Nyakato iliyopo nje kidogo ya mji wa Bukoba.


7. Mwaka 1989 alichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondari ya Pugu, Dar es Salaam katika masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabati.

8. Mwaka 1991/1992, alitumikia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria katika kambi za Ruvu mkoani Pwani na Maramba, Tanga.

9. Baada ya hapo, mwaka 1993 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya kwanza ya sayansi katika hisabati na takwimu.

10. Hakuishia hapo kwani baada ya kufanya kazi kwa muda katika Kituo cha Utafiti na Maendeleo ya Afya cha Ifakara, alikwenda Uholanzi kwa masomo ya shahada ya uzamili ya sayansi katika Teknolojia ya Mawasiliano na Habari katika tiba (MSc in Medical Informatics) kwenye Taasisi ya Sayansi za Afya. Alihitimu shahada hiyo mwaka 2001.

11. Hivi sasa ni mwanafunzi wa masomo ya shahada ya uzamivu katika teknolojia ya habari na mawasiliani kwenye fani ya afya katika chuo kikuu cha Basel, Uswisi.

12. Mfumo wa masomo anayosomea ni ya mazoezi ya vitendo na ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya masomo. Alisema mfumo huo unamwezesha mwanafunzi kuendelea na kazi pia na unatoa nafasi ya kuoanisha masomo ya nadharia na vitendo.

13. Baadhi ya nchi alizotembelea kutokana na masomo, warsha na ziara za kikazi ni ndani na nje ya bara la Afrika, Kenya, Uganda, Ghana, Afrika ya Kusini, Uholanzi, Scotland, Uingereza, Ethiopia, Canada, Italia, Uswisi na Vietnam.

14. Vile vile amekwishafanya machapisho ya kisayansi 10 na kuongoza, kusimamaia, au kuandika miradi takriban 13 ya kitaalamu iliyostahili na kupata ufadhili mkubwa wa fedha.

15. Mukasa hayuko mbali sana kijamii kwani ni mjumbe wa kamati ya usimamizi na tathmini ya masuala ya kitaalamu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

16. Vile vile ni mwakilishi wa umoja wa kimataifa wa wanataaluma wa sayansi na teknolojia ya habari na mawasilino katika afya kanda ya Tanzania.

 
Source: Oscar Mukasa

Swimmer: Oscar Mukasa

Location: Ifakara, Tanzania
TZ.png

Date: 20 Dec 2005

I am a researcher working with the Ifakara Health Research & Development Center (IHRDC) in Tanzania. Currently a PhD student at the Swiss Tropical Institute( STI). Coming from a place known to have high malaria transmission and consequenly high mortality(Ifakara-Tanzania), I am one of those who feel obliged to be part of this initiative.

Why someone should sponsor me: I have slight imbalance of wish and what I can ,at the moment, give out at for this purpose. I feel like contributing 4 nets(Long lasting Treated) which amount to USD 40 but can contribute only CHF 25 from own pocket.As such, I have offered CHF 25 sponsorship to someone and looking for someone to sponsor me the remaining CHF 25 so as to make it CHF 50. Will feel honoured to have contributed in saving a few lives.


 
CCM yamteua Rwegasira kuwania ubunge Biharamulo | NA JOSEPH BURRA

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Oscar Rwegasira, kuwa mgombea wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa Biharamulo Magharibi, mkoani Kagera.

Rwegasira aliteuliwa katika kikao cha kamati kilichofanyika juzi mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa ameteuliwa na mkutano huo kuzindua kampeni za uchaguzi huo, zitakazofanyika Juni 13, mwaka huu. Zitafungwa Julai 4, na Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Kamati ilikutana na wagombea sita walioomba kuteuliwa na Chama kuwania uongozi katika jimbo hilo.

Alisema lengo la kukutana nao ni kuweka mshikamano ili kukipatia Chama ushindi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Julai 5, mwaka huu.

Rwegasira aliongoza katika kura ya maoni kwa kupata kura 309. Wengine walioomba kuteuliwa kuwania kiti hicho na kura zao kwenye mabano ni Magoha Agricola (120), Balagama Mwajemi (23), Rwabudongo Hassan (14), Matata Mussa (10) na Burchard Ntibihora (5).

Kupitia taarifa hiyo, Kamati Kuu imewaomba wana-CCM, wapenzi na wananchi wa Biharamulo kumuunga mkono Rwegasira ili ushindi upatikane.

Uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Phares Kabuye (TLP), aliyefariki dunia Aprili, mwaka huu kwa ajali ya gari mkoani Morogoro.

Kamati Kuu pia imempongeza Lolesia Bukwimba kwa ushindi alioupata katika uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye jimbo la Busanda, uliofanyika mwishoni mwa Mei, mwaka huu.

Wakati huo huo, Angela Sebastian anaripoti kutoka Biharamulo kuwa, vijana wa wilaya ya Biharamulo wamepokea kwa furaha uteuzi wa Rwegasira.

Kutokana na uteuzi huo, vijana hao walifanya maandamano makubwa wakiimba nyimbo za kumpongeza.

Vijana hao walisema uteuzi huo ‘umewakuna' na kilichobaki ni kumuunga mkono mteuliwa huyo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, ili aweze kuwa mbunge.

Walisema wananchi wa Biharamulo wanahitaji mabadiliko, kwani wamekuwa na wabunge ambao kazi yao ni kwenda bungeni na kupokea posho bila ya kuangalia maslahi ya vijana.

Kwa upande wake, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Wilaya ya Ngara, Pantaleon Rumanyika, aliye Biharamulo kwa shughuli za Chama, alisema amepokea kwa furaha uteuzi huo na kwamba, wamejipanga kuhakikisha Chama kinaibuka na ushindi.


Mukasa/Rwegasira - One and the same ?
 
Mukasa/Rwegasira - One and the same ?


Anaitwa Oscar Rwegasira Mukasa ni mtu mmoja! CHADEMA lazima waweke mgombea makini, vinginevyo jimbo walisahau! Hawa CCM wako makini, siipendi lakini ndo hivyo! Maana naona hata hapa JF kampeni ni kali zimeisha aanza naona watu wapo kiitikadi zaidi...

Mas
 
Mukasa/Rwegasira - One and the same ?

- Mkuu Mag3, nimeuliza wanaohusika huko ndani ya CCM baada ya kuiona hii article, ukweli ni ina utata kidogo kwa sababu waliokutana na kuamua sio NEC, ila ni CC ambayo imekutana kwa niaba ya NEC kuepuka gharama za kuita kikao kizima cha NEC na kwamba hiyo inakubalika ndani ya chama cha CCM.

- Pili nimeambiwa kwamba aliyepitishwa ni Oscar ambaye ana jina la mwisho Mukasa, lakini jina la Mukasa ni moja ya sababu kubwa zilizoleta kizaa zaa ndani ya kikao cha kumpitisha huko CC, kwa hiyo ninajaribu again kuthibitisha kama either ni yeye huyo huyo ameamua kuondoa jina la Mukasa, na kutumia Rwegasira, au ni mwingine kabisaa na kama ni mwigine kabisa sitasita kuiomba radhi JF,

- Nitarudi baadaye na more info za uthibitisho.

Respect.

FMEs!
 
- Sawa sawa ni huyo huyo mtu mmoja, nimethibitisha sasa.

Respect.

FMEs!

Oscah nakumbuka kuwa nae Secondari, JKT na UDSM. Wakati huo alikuwa kijina mzuri na analytical. Tumepotezana kwa muda kiasi, nafurahi kuona CV yake imekaa vizuri sasa. Ningependa aendelee kijiimarisha katika sector ya ICT kwenye afya ambapo naamini tuna wataalam wachache sana na mwelekeo wake utatusaidia zaidi huko mbele kama taifa. Tatizo jamii yetu imeshatekwa na utaratibu wa kila mtu kukimbilia kwenye Ubunge kwa kisingizio cha kusaidia jamii. Anyway, namtakia kila la kheri katika juhudi zake ila inaniuma kuona anaenda kwenye siasa na kuacha pengo kwenye ICT na medical services ambapo anahitajika zaidi.
 
Oscah . Ningependa aendelee kijiimarisha katika sector ya ICT kwenye afya ambapo naamini tuna wataalam wachache sana na mwelekeo wake utatusaidia zaidi huko mbele kama taifa. Anyway, namtakia kila la kheri katika juhudi zake ila inaniuma kuona anaenda kwenye siasa na kuacha pengo kwenye ICT na medical services ambapo anahitajika zaidi.

- Mkuu wangu O, heshima mbele mimi ninamfahamu sister mmoja PhD na mtaalamu wa juu sana kutoka huko Ifakara, sasa anabeba mabox majuu, pia ninamfahamu tena mshikaji aliyekua engineer wa ndege ya rais Mwalimu, naye sasa anabeba mabox huko majuu,

- Je inaweza kuwa kubeba mabox majuu ni bora kuwa huko ICT na u-ngineer wa ndege ya rais wa bongo, au?

Respect.

FMEs!
 
Mwacheni kijana aende tu huko na kama ana nia njema basi ni baraka kwa wilaya yake na taifa.

Tatizo tu la Watanzania wengi ni hii ya kusema jambo moja wanapoomba nafasi na kufanya tofauti wanapokuwa madarakani.

Kijana ajiepushe na publicity isiyo na maana, huenda hata hayo magazeti hayafiki huko Biharamulo. Aweke nguvu zote kwenye kutimiza yale anayoyaamini kuanzia kule chini vijijini (grassroot politics) na taratibu mafanikio yake yatafika hata kitaifa.

Ni msomi huyo na ana exposure ya kutosha kufanya mabadiliko kama yuko committed; namtakia kila la heri na mungu amsaidie.
 
Mwacheni kijana aende tu huko na kama ana nia njema basi ni baraka kwa wilaya yake na taifa.

Ni msomi huyo na ana exposure ya kutosha kufanya mabadiliko kama yuko committed; namtakia kila la heri na mungu amsaidie.

- Very strong point, tupo pamoja hapo mkuu.

Respect.

FMEs!
 
Kwenye fani yake ya ICT yuko vizuri lakini tukija kwenye mambo mengine kama mwanasiasa sidhani kama anafaa, siwezi kwenda personal kwa hili...ulizia jamaa alofanya nao kazi kwenye kituo chake hapo....ameisha waliza computer...malipo fake kibao...ulizia utaambiwa. CHADEMA wakiweka mgombea makini CCM wanakazi sana. Sijui kama kadi yake ya CHADEMA ameisha irudisha...ameangalia upepo...ni opportunist sana dogo huyo anawaza kuja waziri kama class mate wake wa shule ya msingi, Kamala

Siwezi sema zaidi ila nikiona uongo hapa nitakuja na kasi ya mwewe!

Wakuu; Nimeongea kwa simu na Oscar, alikuwa njiani kuelekea Bihalamulo na nimemuuliza juu ya tuhuma hizo hapo juu zilizotolewa na Masanilo. Kwa kweli amesikitika sana na amekanusha vikali kuwa hausiki na tuhuma hizo.

Sasa kama Masanilo ana data basi azilete hapa kuliko kutoa tuhuma ambazo hazina ukweli wowote.
 
Wakuu; Nimeongea kwa simu na Oscar, alikuwa njiani kuelekea Bihalamulo na nimemuuliza juu ya tuhuma hizo hapo juu zilizotolewa na Masanilo. Kwa kweli amesikitika sana na amekanusha vikali kuwa hausiki na tuhuma hizo.

Sasa kama Masanilo ana data basi azilete hapa kuliko kutoa tuhuma ambazo hazina ukweli wowote.

Mkuu Allien,

Tuwe wakweli, sasa ulitegemea jamaa aseme kweli alihusika? Umefanya vizuri kuweka upande wa pili wa shilingi ila sasa tumwachie Masanilo kumwaga data zote.

Mimi sitashangaa kama kuna ukweli maana jamii yetu karibu yote imeoza tu. Kwasasa tunashindana kwenye nani fisadi zaidi ya mwingine lakini watu clean wako wachache sana.
 
Mkuu Allien,

Tuwe wakweli, sasa ulitegemea jamaa aseme kweli alihusika? Umefanya vizuri kuweka upande wa pili wa shilingi ila sasa tumwachie Masanilo kumwaga data zote.

Mimi sitashangaa kama kuna ukweli maana jamii yetu karibu yote imeoza tu. Kwasasa tunashindana kwenye nani fisadi zaidi ya mwingine lakini watu clean wako wachache sana.


Nakubaliana na wewe si rahisi mtuhumiwa kukubali kirahisi.

Sasa tusubiri hizo dataz za Masanilo. lakini siyo tuambiwe tukawaulize staff wenzake ofisini kama alivyodai.
 
Back
Top Bottom