CCM: Kamati Kuu Kulikoni Tena?

CCM: Kamati Kuu Kulikoni Tena?

Toa hoja zako. Kwahiyo unakubaliana na hayo niliyoandika eeeh!! Safi, sasa mimi sipo kihivyo.

Anyway ngoja niachane na wewe watashindwa kutofautisha...

U always seek to be embedded in cotton wool....much better sepa zako wacha mjadala wenye maslahi uendelee eboo!
 
Rev. Kishoka,

Achana na huyo FMES maana atakupotezea muda tu. Umejaraibu kujenga hoja yeye anaenda kwenye mambo ya familia. Watu wengine wakienda mambo ya familia yake anakuja juu.

Hapo mamake yuko kweye hilo kundi basi atamtetea mpaka siku ya kufa. Hao hao walioitwa wahuni na Nyerere tunaambiwa ndio wanaongoza kutupigania sisi maskini, ni uwizi mtupu.

Nimepata points nyingi sana kwenye hii thread za kutumia huku vijiweni. Asante kwa somo la nguvu mkuu Kshoka.

- Mkuu kwa hoja hizi za mama una maana Mwakyembe ana something to do na mama yako ndio maana unamchukia au what?

- Kuhusu familia yangu nimekupa go ahead kama unaijua yaweke hapa, tatizo lako wewe ni low mind unachojua ni kurusha rusha majina ya watu na kuwaisngizia ID, hujawahi kuwa na hoja hata siku moja ndio maana kila wakati ninauliza mtu mwenye high IQ kama Mwakalinga, anawezaje kuwa karibu na mtu low mind kama wewe nashindwa kupata jibu,

- Yaani una maana Nyerere alimuita mama yako muhuni au what? maaana sielewi haya ya mama na uhuni ulikoyatoa vipi ukiyaweka sawa hapa mkuu ili ujibiwe ipasavyo!

Respect.

Field Mashall Es!, ni Wazee wa Sauti ya umeme!
 
- Eti ufisadi ni tatizo la system yetu ya uchumi tuliloachiwa na wakoloni? Can you define this mkuu kwanza kabla sijakujibu post yako nzima? Unasema wakoloni ndio waaliotuachia tabia za kuogopana kwenye uongozi wa juu wa taifa letu ambacho ndio hasa chanzo cha ufisadi?

- Unasema wakoloni ndio waliotufundisha kutoheshimu sheria zetu wenyewe, au the respect kwa rule of our laws? Unasema wakoloni ndio walio-create system ya vigogo kina Kahama, Rupia na Bomani ndani ya political system yetu ambao sasa na wao wamekuja kurithiwa na kina Rostam, Karamagi, na Lowassa, unasema this is wakoloni fault?

- Are you serious mkuu or you are just kidding! Mkuu ukinijbu hili basi nitaichambua post yako nzima, ila kwanza niwekee muongozo hapa!

Respect.

Field Marshall Es!
Field Marshall, Jambo Afande! Jana nilikusoma Mkuu lakini nikawa sina buku ya kulipia internet cafe' nikashindwa kutoa majibu ya hoja yako.Leo nimebangaiza Kariakoo shimoni ndo mana niko jamvini.
Mkuu umehoji hoja yangu ya kuhusisha historia ya ufisadi na ukoloni. Ngoja nikukumbushe,kabla na mara baada ya uhuru kulikuwa na Kampuni kubwa sana nchi hii inaitwa Smith McKenzie,hawa ndo walikuwa biggest importers nchi hii,actually ndo predecessor wa RTC na Ugawaji(NDL),Je hii Smith McKenzie ilikuwa ina trade na nani? Kwenye mashamba ya mkonge,chai,kahawa,pamba ambayo ndo yalikuwa mainstay ya uchumi wa nchi nani walikuwa suppliers wa inputs na matumizi ya vibarua kama sukari ,mchele,viberiti,kaniki na sigara? Jibu la swali hili litakupa picha kamili ya mfumo wa uchumi aliojenga mkoloni na kuturithisha. Sasa jiulize baada ya kutaifisha Smith McKenzie na kuanzisha SU zetu badala yake, je hizi SU mpya zili trade na nani? jiulize pamoja na nia njema ya Mwalimu (RIP) kubadili mfumo wa uchumi mwaka 1967 je alifanikiwa? kama alifanikiwa kwa nini lilitokea seke seke la uhujumu uchumi early 80's?, na kama hakufanikiwa ni kwa nini? Kaja Mzee Mwinyi kafutilia mbali SU na Mzee Mkapa akamsaidia kuzishindilia lijisumari la mwisho je hii ilileta mabadiliko yoyote katika mfumo wetu wa uchumi? Kama haujabadilika na hali ya maisha ya Watanzania bado ni tia maji tia maji ili tufikie maisha bora kwa kila Mtanzania tufanye nini? FMES nasema na ninasisitiza something radical lazima kifanyike katika kubadili mfumo wetu wa uchumi,lazima tujitengenezee utaratibu utakaotuhakikishia kuwa rasilimali zetu zinatusaidia sisi na sio vinginevyo,huu ndo utaratibu wa wote walioendelea,kuanzia bara Asia,Ulaya hadi Amerika.Field Marshall,kuwatukana wazee wetu kama kina Mzee Kahama, Mzee Rupia,Mzee Bomani(RIP) hakutatupeleka popote afterall wote tunaelekea huko, we are not getting younger.Kumbuka hawa walipewa nchi wakiwa kwenye 20's, jiulize wewe at 25 ulikuwa na uwezo gani wa kuongoza, si ndo ulikuwa moto bati chini kila kukicha Disco (which is normal kwa kijana yeyote wa rika hilo)? FMES unapomsimanga Mzee Kahama kuwa ni fisadi in the same breath mbona humsifii basi Mzee Kawawa,Mzee Songambele,Mzee Nnauye na wengine ambao wamemalizia Uongozi wao katika umasikini tu? Mkuu FMES hebu jiangalie kwenye kioo huku ukijua kwamba ufisadi ni ufisadi tu hata kutazamia mtihani darasani ni ufisadi .Wasalaam.
 
Field Marshall, Jambo Afande! Jana nilikusoma Mkuu lakini nikawa sina buku ya kulipia internet cafe' nikashindwa kutoa majibu ya hoja yako.Leo nimebangaiza Kariakoo shimoni ndo mana niko jamvini.
Mkuu umehoji hoja yangu ya kuhusisha historia ya ufisadi na ukoloni. Ngoja nikukumbushe,kabla na mara baada ya uhuru kulikuwa na Kampuni kubwa sana nchi hii inaitwa Smith McKenzie,hawa ndo walikuwa biggest importers nchi hii,actually ndo predecessor wa RTC na Ugawaji(NDL),Je hii Smith McKenzie ilikuwa ina trade na nani? Kwenye mashamba ya mkonge,chai,kahawa,pamba ambayo ndo yalikuwa mainstay ya uchumi wa nchi nani walikuwa suppliers wa inputs na matumizi ya vibarua kama sukari ,mchele,viberiti,kaniki na sigara? Jibu la swali hili litakupa picha kamili ya mfumo wa uchumi aliojenga mkoloni na kuturithisha.

Mkulu Bishanga, heshima mbele sana:-

- Hii yako ni great thinking tena a very educative posts, lakini naomba kusema hivi wakoloni walikuwa wanatafuta malighafi za kurudisha kwao katika kuendeleza uchumi wao, na kuendeleza viwanda vyao kule Europe ni kweli walikuwa ni wezi wa mali zetu lakini hawakuficha nadhiri yao kwetu wananchi hata siku moja, tulikuwa watumwa wao kwa hiyo hatukuwa na sauti wala nguvu ya kuweza kubishana nao, infact walikuwa wamepewa nchi yetu legally kwa sheria za kimataifa,

- Uchumi alioujenga mkoloni ulikuwa ni kwa manufaa yake zaidi lakini sio kwa manufaa yetu, but siku zote alihakikisha kwamba na sisi tunafaidika na ule uchumi na kukidhi matakwa yetu kimaisha, hakuchukua kila kitu bila kuturudishia chochote, infact alijitahidi hata kutusomesha na kutupeleka kwao kupata elimu ya juu zaidi, as opposed na the thinking ya wanaoujenga uchumi wetu wa sasa, ambao they could careless na kuturudishia anything back, wao ni kupeleka nje tu huku wakisaidiwa na hawa mafisadi wachache wenye power kutoka kwenye kura zetu wananchi. Wanatuhadaa kwamba they care for our nation, lakiini matendo yao ni tofauti kabisa na maneno yao,

- Na besides, system ya uchumi iliyojengwa na wakoloni haina anything to do na ufisadi sugu uliokithiri sasa nchini kwetu, mafisadi watatu ambao ndio hasa kichwa cha huu ufisadi bongo ninashindwa kuamini kwamba chanzo chao ni system ya uchumi tulioachiwa na wakoloni miaka 45 iliyopita, wakoloni walikuwa wanajali na kuheshimu sana sheria, sisi toka awamu ya kwanza we never respected the rule of law kwa hiyo tukasahau kwamba freedom comes with a keen sense of responsibilities na haya ndio matokeo yake tuka-create ufisadi on our own.

- Wakoloni walikuwa wanajali sana kukusanya kodi, sisi we did not tuka-politicise kila kitu na ku-set agenda that had some worthy and convincing elements, lakini very in-adequate katika kweza ku-meet our future economics challenges as the results we are stuck na ufisadi. Siamini kwamba Wahindi ambao ndio wanaomiliki uchumi wetu sasa hivi wanaweza kushamiri katika kutufisadi, kama sio kwa msaada wa viongozi wetu wachache sana ambao ndio hasa chanzo cha ufisadi nchini.

- Lakini still you have a point, ingawa kwangu it is too vague na ni too general to cover fairly the root ya ufisadi nchini.

Respect.

FMEs!
 
Bosi, embu kuwa na adabu kidogo!

Mkuu hiyo ni Lugha tu, lakini ukweli wa Mambo ndio Huo, sisi tunapenda sana KUKONGWA ROHO, akitokea mtu AKATUKONGA ROHO basi tunasahua kabisa shida zetu za jana, tunasahau hata ADUI zetu wa Jana, Ona sasa Chiligati AMEKONGA watu ROHO sasa hivi na yeye atajumuishwa katika kundi la WAPIGANAJI
 
1.
Sasa jiulize baada ya kutaifisha Smith McKenzie na kuanzisha SU zetu badala yake, je hizi SU mpya zili trade na nani? jiulize pamoja na nia njema ya Mwalimu (RIP) kubadili mfumo wa uchumi mwaka 1967 je alifanikiwa? kama alifanikiwa kwa nini lilitokea seke seke la uhujumu uchumi early 80's?, na kama hakufanikiwa ni kwa nini?

- Again, katika kutaifisha taifisha bila research wala history education behind the subject, tuliishia ku-throw away a chance ya kuruhusu the past to serve the present,

- Mwalimu asingeweza kufanikiwa kwa sababu nyingi sana moja ikiwa ni kutoheshimu sheria, na besides fundamentally his socialism theory was flawed period, sasa kwa sababu alikuwa tayari ameshavunja au kuondoa system ya cheks and balance in governing kwa kuanzisha one party state, akaishia kuwa kiongozi anaye hid behind disarmament image of himself ambayo ni a formula only good for protecting status quo, lakini not a formula for good leadership, And that is what we have today as urithi lakini nothing to do na wakoloni na jinsi walivyotutawala leave alone system ya uchumi waliyotuachia.

- Inasikitisha sana kwamba Mwalimu a great thinker na educated leader, would base his beliefs in a deeply flawed theory of socialism na he would even force us wananchi to believe on that flawed theory, huku yeye binafsi akiwa amejitayarisha ku-bail out incase it did not work, lakini never prepared us as a nation to know how to swim kama boat ikienda mrama as it did.

Sasa 45 years after uhuru, na almost 23 years after Mwalimu jumped the sinking ship, tumefanya nini kurekebisha mwendo wa our ship?

Respect.

FMEs!
 
Kaja Mzee Mwinyi kafutilia mbali SU na Mzee Mkapa akamsaidia kuzishindilia lijisumari la mwisho je hii ilileta mabadiliko yoyote katika mfumo wetu wa uchumi? Kama haujabadilika na hali ya maisha ya Watanzania bado ni tia maji tia maji ili tufikie maisha bora kwa kila Mtanzania tufanye nini?

- Hapa I agree with you kwa 100%, Ingawa ninam-recommend Mkapa for atleast creating a min middle class, ya kibongo bongo.

FMES nasema na ninasisitiza something radical lazima kifanyike katika kubadili mfumo wetu wa uchumi,lazima tujitengenezee utaratibu utakaotuhakikishia kuwa rasilimali zetu zinatusaidia sisi na sio vinginevyo,huu ndo utaratibu wa wote walioendelea,kuanzia bara Asia,Ulaya hadi Amerika.

- Again hapa nipo na wewe, lakini kumbuka kwamba imewachukua miaka 300 hao walioko mbele yetu kiuchumi huko ughaibuni, na besides hawakufanya makosa makubwa sana katika kujenga foundation yao kama sisi tulivyofanya, viongozi wetu walishindwa ku-stand behind the enforcement of their own resolutions which they claimed to be beneficial to our future development as a nation na as the results their resolutions were fruitless, did not mean anything much kwa taifa and so wakafanikiwa kujenga foundation based on illusions na matokeo yake wakajenga society ambayo ni perfect in illusinations na isiyo na hope at all and that is where we are,

- Ukiwaangalia vizuri viongozi wetu ni suiciders, unstable na wameshia kuinflict a grave damage to the credibility of our political system. Sasa tunahitaji kwanza a new more human approach ambayo ita-put a side all political considerations solutions na kuweka emphasis kwenye legal considerations kwanza.

Taifa lisiloheshimu sheria zake ni sawa na kichwa cha mwendawazimu, and we know what mwandawazimu does ni kuzunguka pale pale huku akidai ana-move forward.

Respect.

FMEs!
 
Field Marshall,kuwatukana wazee wetu kama kina Mzee Kahama, Mzee Rupia,Mzee Bomani(RIP) hakutatupeleka popote afterall wote tunaelekea huko, we are not getting younger.Kumbuka hawa walipewa nchi wakiwa kwenye 20's, jiulize wewe at 25 ulikuwa na uwezo gani wa kuongoza, si ndo ulikuwa moto bati chini kila kukicha Disco (which is normal kwa kijana yeyote wa rika hilo)?


- Whaaat! wow! wow! hold on there for aminute, unasema kuwaita mafisadi exactly what they are ni kuwatukana? Ohh yeah I am not getting younger lakini I m also not stealing from anybody,

- Yaani unasema kwamba age like 20-25 years wakiiba inapaswa kuwa legal defense kwenye mahakama zetu kwamba hawajui wanachofanya? Mkuu mbona ulianza vizuri sasa unaanza kuharibu tena, yes nikiwa na miaka 20-25 nimecheza Disco infact bado ninacheza mpaka leo, lakini sikumuibia mtu wala serikali katika kucheza Disco langu, now what that has to do na mafisadi?

- No! no! mkuu this point is out of the line, absolutely out! fisadi ni fisadi it does not come with age excuse, it is simply fisadi!

FMES unapomsimanga Mzee Kahama kuwa ni fisadi in the same breath mbona humsifii basi Mzee Kawawa,Mzee Songambele,Mzee Nnauye na wengine ambao wamemalizia Uongozi wao katika umasikini tu?

- Mkuu wrong number, tunaongelea mafisadi sio viongozi safi unaweza kuanzisha thread ya viongozi wetu saafi, lakini I am not so sorry mkuu hapa tunaongelea mafisadi, na ni wewe ndiye uliyeamua ku-cover their history, fisadi ni fisadi hatuwezi kuwaita anything else!

Mkuu FMES hebu jiangalie kwenye kioo huku ukijua kwamba ufisadi ni ufisadi tu hata kutazamia mtihani darasani ni ufisadi .Wasalaam.

- Unajua I am looking forward, one day to have a serious discusions kuhusu our nation, bila kuishia mimi kuingizwa personal tena bila dataz wala facts, I can't wait for that day,

- Nijiangalie kwenye kioo for what matter comparing with ufisadi ambao ndio the main subject hapa on our nation? Sasa on the same token je wewe umejiangalia tayari au unafikiri hii ID inanidanganya kuhusu who you are? Majuzi tu umesema hutaki personal na mimi lakini since umekuwa ukijizungusha zungusha kama kinyonga vipi mkuu unataka kujadili taifa au mimi as a person?

I mean chagua moja mkuu, kusuka au kunyoa! Otherwise, angalau umejitahidi na serious points na education, mpaka huku mwishoni na sikulaumu sana maana nimegundua siku nyingi sana kwamba you can't help your self kama wengine wengi humu JF, inapokuja FMES. Sasa tuendelee kukata ishus muhimu kwa masilahi ya taifa, lakini please can we stick to the ishus badala ya mimi as a person?

Respect.

Field Marshall Es, ni Wazee wa Sauti Ya Umeme!
 


- Whaaat! wow! wow! hold on there for aminute, unasema kuwaita mafisadi exactly what they are ni kuwatukana? Ohh yeah I am not getting younger lakini I m also not stealing from anybody,

- Yaani unasema kwamba age like 20-25 years wakiiba inapaswa kuwa legal defense kwenye mahakama zetu kwamba hawajui wanachofanya? Mkuu mbona ulianza vizuri sasa unaanza kuharibu tena, yes nikiwa na miaka 20-25 nimecheza Disco infact bado ninacheza mpaka leo, lakini sikumuibia mtu wala serikali katika kucheza Disco langu, now what that has to do na mafisadi?

- No! no! mkuu this point is out of the line, absolutely out! fisadi ni fisadi it does not come with age excuse, it is simply fisadi!



- Mkuu wrong number, tunaongelea mafisadi sio viongozi safi unaweza kuanzisha thread ya viongozi wetu saafi, lakini I am not so sorry mkuu hapa tunaongelea mafisadi, na ni wewe ndiye uliyeamua ku-cover their history, fisadi ni fisadi hatuwezi kuwaita anything else!



- Unajua I am looking forward, one day to have a serious discusions kuhusu our nation, bila kuishia mimi kuingizwa personal tena bila dataz wala facts, I can't wait for that day,

- Nijiangalie kwenye kioo for what matter comparing with ufisadi ambao ndio the main subject hapa on our nation? Sasa on the same token je wewe umejiangalia tayari au unafikiri hii ID inanidanganya kuhusu who you are? Majuzi tu umesema hutaki personal na mimi lakini since umekuwa ukijizungusha zungusha kama kinyonga vipi mkuu unataka kujadili taifa au mimi as a person?

I mean chagua moja mkuu, kusuka au kunyoa! Otherwise, angalau umejitahidi na serious points na education, mpaka huku mwishoni na sikulaumu sana maana nimegundua siku nyingi sana kwamba you can't help your self kama wengine wengi humu JF, inapokuja FMES. Sasa tuendelee kukata ishus muhimu kwa masilahi ya taifa, lakini please can we stick to the ishus badala ya mimi as a person?

Respect.

Field Marshall Es, ni Wazee wa Sauti Ya Umeme!
Nothing personal Kamanda,what i meant ni ile ya Bwana Yesu kwamba anayetaka kurusha jiwe na ajiangalie mwenyewe nafsi yake kwanza,and that applies kwangu,kwa yeye na yule na wanajamvi wote.Binafsi sijui identity yako Kamanda and I am not in the business of speculating identities za Wadau,it does not suit me,raha ya JF ni uhuru wa kutoa mawazo yako without checking over your shoulder.Kama nimekukwaza kunradhi Kamanda,I salute!
 
Nothing personal Kamanda,what i meant ni ile ya Bwana Yesu kwamba anayetaka kurusha jiwe na ajiangalie mwenyewe nafsi yake kwanza,and that applies kwangu,kwa yeye na yule na wanajamvi wote.Binafsi sijui identity yako Kamanda and I am not in the business of speculating identities za Wadau,it does not suit me,raha ya JF ni uhuru wa kutoa mawazo yako without checking over your shoulder.Kama nimekukwaza kunradhi Kamanda,I salute!

- It takes a lot kunikwaza, I hope hukujikwaza mwenyewe,

- Bby the way sina sababu ya kujiangalia anything inapokuja kurusha mawe kwa mafisadi, sasa can we get back to the real ishu and lets cut the chase!

Respect.

FMEs!
 
- Matokeo ya kikao hiki cha Kamati Kuu:-

- Respect wakuu kikao kimeisha tayari, agenda zilikuwa mbili tu according to the dataz, nazo ni kusimamishwa kwa zoezi la utamaduni wa wajumbe wa CC kutembelea majimbo na maeneo ya uchaguzi nationally ambayo huwa tabled as kuhamasisha wananchi kwa ajili ya uchaguzi, na pili Kikao kilitakiwa kutoa baraka zake kwa mfumo mpya utakaotumiwa na CCM kupitia mtandao, yaani online au internet.

- Briefly, the dataz za kikao ni kwamba:-

1. Rais amesitisha zoezi la wajumbe wa kamati hiyo kusafiri mikoani kuhamasisha wananchi kuelekea uchaguzi mbali mbali unaokuja, tabia ambayo imekua ni utamaduni wa CCM kwa miaka mingi.

- Sababu iliyotolewa ni kwamba chama hakina pesa kwa sasa, lakini wajumbe wengi wa kikao hicho wametoka huko ndani wakiwa na hisia mbali mbali kuhusiana na uamuzi huo wa mkulu. Kuna hisia moja nzito ambayo haijathibitishwa kwamba mafisadi wameamua kukichezea chama ili kikwame kipesa, ikiwa ni kwa kuwashawishi wafadhili wake wakubwa kutokipa pesa as usual.

2. CC ilitakiwa kutoa baraka kwa zoezi jipya la kuanza kutumia mtandao kama nyenzo muhimu ya kuwasiliana na wananchi na wanachama wake katika kutekeleza ilani za chama hasa za uchaguzi na utawala. Kikao hicho kwa kauli moja kilitoa baraka hizo ambazo ni kufuatia matayarisho makubwa ambayo yamekua yakifanywa kwa muda mrefu sana sasa, kuelekea kwenye kuhamishia shughuli nzito za chama yaani CCM, kwenye mtandao,

- Pia itakumbukwa kwamba ni majuzi tu Chadema walikuwa wa kwanza kuanzisha rasmi njia hii ya siasa kwenye mtandao.

- Hakukuwa na hoja ya ufisadi period, wala kizaa zaa cha NEC iliyopita.

Respect Wakuu.

Field Marshall Es!
 
Field Marshall Es,
Mkuu nimekusikia.. lakini haya mahitimisho yamefikiwa baada ya Wapiganaiji kuingia mikoani au? maanake nashindwa kuelewa haswa lengo la kikao hiki kuzungumzia mambo kwa ujumla wakati kuna makundi ya watu, wilaya na hata mikoa yatakayonufaika zaidi..
 
Field Marshall Es,
Mkuu nimekusikia.. lakini haya mahitimisho yamefikiwa baada ya Wapiganaiji kuingia mikoani au? maanake nashindwa kuelewa haswa lengo la kikao hiki kuzungumzia mambo kwa ujumla wakati kuna makundi ya watu, wilaya na hata mikoa yatakayonufaika zaidi..

- Mkuu kuna hisia nyingi among viongozi wa CCM, kuhusu uamuzi huu kwamba moja ya hisia hizo ni temporary kujikinga na njama za mafisadi kui-bring CCM to its knees kwa kuifungia njia za kupata hela kutoka wafadhili wake ili iwe tegemezi wake, kwa sababu sasa hivi CCM haina hela za kuwa-afford kuzunguka mikoani,

- Na besides, viongozi wapiganaji kwenye kamati kuu ni wawili tu, ninaamini waliozuiwa ni wajumbe wa CC tu, kama the idea ingekuwa ni kuwabana wapiganaji, basi ingekua ni kwa NEC nzima na viongozi wote wa CCM, huu ulikuwa ni simply uamuzi wa Mwenyekiti tu, na CC walipewa orders tu!

Respect.

Kamanda Es!
 
Mkuu Mkandara,

Hitimisho la hicho kikao haliko wazi sana na haijulikani limewalenga watu gani haswa kwa kuwa justification ya kuzuwia hizo safari, kwamba Chama hakina fedha, haina nguvu sana kwa kuwa kuna makundi ama individuals ndani ya chama wamekuwa wazinguka kwa kutumia fedha zao wenyewe.

Je, mafisadi wakiamua kuzunguka nchi nzima ili kuhamasisha uchaguzi kwa kutumia fedha zao wenyewe, JK atawaruhusu? Je, wapiganaji wanaopewa ufadhili na Mzee Mengi wakiamua kuzunguka nchi nzima ili kumwaga sera zao, JK atawaruhusu?

Mwakyembe na wenzake wanaweza kuruhusiwa kwenda mikoani kwa kuwa wao wanakwenda kwenye majimbo yao tu ama kwenye jimbo la mpambanaji mwenzao ili kumpiga tafu. Hawana hoja inayolenga nafasi kubwa na nyeti kama ya Rais kwa kuwa uwezo wao kifedha ni mdogo na pia nafasi yao ndani ya chama ni mdogo sana. On top of that kundi la wapiganaji wala si tishio kwa JK kama mgombea wa urais hapo 2010, bali ni tishio kwa kuivua nguo serikali kwa hiyo JK anacholilia sasa ni kuwa-control ili wasipige sana kelele, maana kelele za wapiganaji zinamfanya JK aonekane kuwa ni weak president ambaye ana watendaji wabovu lakini ameshindwa kuwawajibisha.

Kundi la pili ni la mafisadi ambao tayari wana watu wao walio kwenye chama na serikali. Kuanzia kwenye vikao vya juu vya chama mpaka ngazi ya wilaya kuna watetezi wa mafisadi na wala si mtetezi mmoja mmoja bali ni kikundi. Ukija serikali kuanzia mawaziri, manaibu waziri, wakuu wa idara za serikali, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, wengi wao ni watetezi wa mafisadi maana walipewa ukuu wa mkoa/wilaya kama shukurani ya kazi waliyofanya 2005. Ukija kwenye chama ngazi ya mikoa na wilaya, makatibu wa UVCCM, makatibu wa CCM, viongozi mbali mbali wa CCM wa kuchaguliwa kwenye ngazi ya wilaya na mikoa waliowezeshwa kifedha na mafisadi kwenye kampeni za uchaguzi wa chama wa 2007, wengi wako kwenye kambi ya mafisadi. Wote hao kwa makusudi maalum wanaweza kutumika na mafisadi kwa malengo ya kuhakikisha kwamba matakwa ya mafisadi yanatekelezwa. Kwa hiyo wajumbe wa CC wakienda mikoani, kama ni fisadi lazima ahakikishe anatekeleza matakwa ya mafisadi, hilo ndilo linalomtisha JK kwa sasa. Kumbuka more than 90% ya wajumbe wa CC ambao wako active (kwamba chama kinaweza kuwatuma mikoani) wana harufu ya ufisadi. Hapa nimetoa wazee kama akina Kawawa, Msuya, Mkapa, Mwinyi na wengineo ambao wanahushuria vikao tu, lakini linapokuja swala la kutekeleza hawashirikishwi.

Je, hawa mafisadi wakitaka kuzungukia mikoa yote kwa fedha yao wao wenyewe, chama kitawaruhusu? JK anakumbuka rafu aliyocheza kipindi cha kuelekea 2005, anajua mbinu zote chafu ambazo timu yake (ikiongozwa na EL na RA) walizotumia ili kuhakikisha anashinda kwa kishindo. Anaogopa wasije wakamzunguka na ikifika wakati wa kujaza fomu ajikute yuko kikaangoni na mmoja wa hao mafisadi, na iwapo CC itasema impambanishe JK na EL, kwenye NEC JK anaweza kushindwa vibaya sana. Sijawahi kuona mwenyekiti wa CCM ambaye hana nguvu ndani ya chama chake kama JK, ambaye hana ubavu wa kukemea lugha chafu na kejeli kwenye vikao maalum vya chama, ambaye hawezi kuonyesha msimamo wake ndani ya kikao mpaka asubiri kwanza apime upepo wa wananchi ndipo aseme yuko upande gani. Kwenye kikao cha NEC cha juzi, JK hakuwa na la kusema bali kukaa kimya na kuangalia comedy iliyokuwa inaendelea.

Baada ya kuona yaliyojiri kwenye NEC, ameogopa na amejua kwamba NEC siyo ya kwake, anaweza kuwa na nguvu kwenye CC lakini siyo kwenye NEC. Walio na control ya NEC ni RA na EL. Leo ukiitishwa mkutano mkuu wa CCM, JK akapambanishwa na EL, anaweza asipite kwenye mchujo wa kura. Hilo ndilo ambalo linaweza kuwa limepelekea kufikia hilo hitimisho.

JK anawaogopa zaidi mafisadi kuliko hata hao wapiganaji, maana mafisadi bado wanatumia mtandao wao ule wa zamani na kwa kuwa wana mtandao wengi walikuwa recruited na EL + RA, wengi wa wanamtandao wanaendelea kuwa watiifu kwa EL na RA na hivyo JK amebaki peke yake na wachache kama akina Membe ambao wanafikiria 2015 kwamba wanaweza kugombea urais.
 
Last edited:
- Mkuu kuna hisia nyingi among viongozi wa CCM, kuhusu uamuzi huu kwamba moja ya hisia hizo ni temporary kujikinga na njama za mafisadi kui-bring CCM to its knees kwa kuifungia njia za kupata hela kutoka wafadhili wake ili iwe tegemezi wake, kwa sababu sasa hivi CCM haina hela za kuwa-afford kuzunguka mikoani,



Kamanda Es!

Je, mafisadi wakiamua kukifadhili Chama, JK atawaruhusu wajumbe wazunguke mikoani?
 
Je, mafisadi wakiamua kukifadhili Chama, JK atawaruhusu wajumbe wazunguke mikoani?

- Mkuu Keil ligi ya nini tena, mimi toka lini nimekuwa mjumbe wa CC? Nimekupa dataz za matokeo ya kikao, sasa ni wajibu wako na wangu ku-speculate why? na Kwa nini!

- Sasa majibu ya haya maswali unataka niyatoe wapi ya kujua JK anafikiria nini na atafanya nini? Why with you ni lazima iwe ligi mkuu?

Respect.

FMEs!
 
Mkuu FMES,

Hakuna ligi hapa, nilichoweka hapo ni changamoto ya swali, not necessarily limeelekezwa kwako, bali wana jamvi pamoja na hao viongozi wa CCM na wajumbe wa CC, ambao wamesema kwamba wanahisi kuwa lengo la JK ni kujikinga na mafisadi ili chama kisije kikaishiwa fedha.

NEC ya CCM ya majuzi imeleta mambo, tuko hapa tutakuja kukumbushana. Kuna mengi yanakuja ndani ya miezi 4 ijayo.

Unadhani kwanini EL ameanza kujikinga kwamba hana mpango wa kugombea urais? Haya hayaji kwa coincidence tu, lazima kuna moto unawaka somewhere na hivyo mikakati ya kudhibitiana kichini chini inaendelea ili kuweka mambo sawa.

Siku mbili zilizopita nimesoma magazeti ya Majira na Mwananchi, walisema, Lowassa asema hajafikiria kugombea, [kwa hiyo anaweza kufikiria na akaamua kugombea, tusije tukashangaa tukisikia anagombea]. Leo nimesoma gazeti la HabariLeo, anasema wanaoandika kuwa Lowassa anataka kugombea urais wanataka kumgombanisha na JK, yeye bado anamuunga mkono Rais wake. Hizo sentensi zote zimekaa kimtego mtego tu. Kwani hizo tetesi za EL kugombea zimeanza leo ama zimeanza kuandikwa leo kwenye magazeti? Kwanini aanze kuropoka baada ya kikao cha CC cha juzi jumamosi?

Kazi kwenu wana CCM, sisi wengine tunatazama tu na kutoa changamoto.
 
Hivi wapiganaji ni akina nani? Na wanapigana na nani au wanapigania nini? Nimedandia mjadala?
 
Back
Top Bottom