CCM kuendelea kujimilikisha nchi kiharamu mwisho umefika. Hatutakubali tena

Jeshi la police liache kujifanya refa liache vyama vinyukane kwa hoja, wananchi ndio majaji
 
Kwa Upinzani huu dhaifu uliopo nchini Tanzania ni kheri CCM itawale Tanzania mpaka pale Yesu Kristo na Mtume Mohammed SAW watakapokuja Kutukomboa na kutupeleka Mbinguni kwa Mungu Baba.

Cc: Prof Koboko
Mtume hakutoa ahadi kwamba atarudi, yeye alikufa mazima.

Aliyeahidi kurudi ni Yesu tu
 
Mimi najiuliza suali moja:- Ikiwa ccm hawaitaki katiba mpya hivi kweli watakubali mpinzani ashinde?

Lunatic
ccm hawatakubali kwani chaguzi zote huwa wapinzani wanashinda tu mbona,masikini maalim seif hadi anaingia kaburini alikuwa anawagaragaza ccm zenji kila chaguzi
 
Kwa Upinzani huu dhaifu uliopo nchini Tanzania ni kheri CCM itawale Tanzania mpaka pale Yesu Kristo na Mtume Mohammed SAW watakapokuja Kutukomboa na kutupeleka Mbinguni kwa Mungu Baba.

Cc: Prof Koboko
Hivi kweli upinzani ungekuwa dhaifu, CCM wangekuwa na haja ya kutegemea nguvu kubwa ya DOLA kuhalisha uvunjaji wa katiba, kamatakamata ya Polisi na abra kadabra ya ma DED/NEC?
 
Labda ulikuwa bado kuzaliwa, Tanzania ilikuwa ndio nyumbani kwa wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika.
 
Watanzania ndio wanaamua ccm iendelee kuongoza wala kwa mapenzi yako na wenzako hamuwezi zuia. Ni kitu watanzania wanaamua kwa kura zao ingawa utasema sio kweli ni kweli. Marekani democrates na republican wanaongoza. Uingereza conservatives na kile kingine. Mbona wananchi hua hawachagui vingine wakati vipo? La msingi kuna amani uhuru na serikali inafanya kazi kuleta maendeleo. Kuna nchi kama saudia wala hakuna chama. Kuna nchi kama uchina kuna chama kimoja. Siku watanzania watataka mabadiliko hakuna atawazuia hata ccm haitaweza.
 
Katiba mpya ikipatikana itatuhakikishia yafuatayo?
-itakomesha uzembe kazini?
-itawaondoa wabadhirifu wa fedha za umma?
-itasababisha huduma za kijamii kuwafikia watanzania kwa wakati?
-
-Itazuia utovu wa nidhamu kwa baadhi viongozi wa vyama kutoheshimu mamlaka zilizopo.
Kwa msingi huo sasa, isiwe katiba ya kutumika kama daraja kwa vyama vya siasa kuingia madarakani then wananchi wanaendelea kupambana na hali zao.
 
Si upinzani huu wetu wa kuongoza harakati za ugaidi na kuwa vibaraka wa mabepari. Watanzania tutaendelea na CCM tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…