CCM kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge Catherine Magige na wenzie kwa kuvamia msiba na kukosa utu

Nani asiye kuwa na mitala katika CCM! Huyo ni mtoto amekurupuka, isije ikawa yeye akapewa onyo
 
Huyu mjinga analipwa 12,000,000 kwa mwezi na posho ya 340,000 ajili ya kugombea waume za watu? jinga kabisa hivi viti maalum vifutwe kutwa wanatafuta mabwana za watu.
Inaonesha wewe bado mtoto
 
Kama alihama akiwa na akili timamu Magige kosa lake nini?
Dawa ya wanawake viburi kama huyo mnayemtaja ni MATALA tu. Halafu kulia lia kinafiki si waume tukifa tutakuja kukuonana wabaya ipo siku atafufuka mtu ooooh

Magige ana Haki kuonyesha hisia zake. 2 yrs in a single bed naked mnaliona dogo.

Ngoja dawa ni kuandika mirathi hata kwa micheuko na kuirithisha tu tena naiweka kisheria zaidi
 
Huyu akivuliwa uanachama, Ndugai atachukua hatua faster na wala hatasubir kupewa barua au nyaraka yoyote kuthibitisha chama chake kimemvua uanachama.
Hivi umeona video au unakurupuka tu, unadhani CCM sawa na wajinga wengine? Haya ni masuala binafsi nakueleza wala hayahusu chama.
 

Barikiwa sana Dada kwa kuokoa Ndoa ya Mwanamke mwenzio,naamini sasa unaishi kwa furaha na Amani na Mume wako halali.Kwa busara zako umemwandalia mazingira mazuri sana mtoto wako kwa ndugu zake na Step Mom wake.
 
Unaweza kuwa sahihi lakini hata hivyo kuna shida kutoka kwa Carherine hata maelezo yako yanaonyesha hivyo (hapo uliposema wahakikishe mpendwa wao anazikwa kwa heshima bila vurugu). Kwani kuzika kwa heshima bila vurugu ni pamoja na kuhakikisha nani ashiriki na nani asishiriki.

Ndoa ni jambo la kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila. Halikadhalika, maziko ni jambo la kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila pia. Kwa msingi huo taratibu za ndoa na maziko hazina budi kutawaliwa na matakwa ya vitu hivyo. Kwa muktadha huo, wafiwa halali (wanaotambulika ima kidini, kijamii, kisheria au kiutamaduni/kimila) wana haki na wajibu wa kusimamia namna ya kumzika mtu wao ikiwa pamoja na kuamua nani awepo na nani asiwepo katika maziko. Ni wazi Catherine si mfiwa anaetambulika na kundi lolote katika hayo niliyotaja (kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila) hivyo ushiriki wake katika maziko ulipaswa uzingatie matakwa au ridhaa ya wafiwa/wahusika. Ingeonekana mke wa marehemu amekosea iwapo Catherine angekuwa anatambulika na kundi lolote miongoni mwa hayo, hapo angekuwa na haki ya moja kwa moja ya kumzika mpendwa wake. Hata kama angekuwa mke wa sirini kama ilivyo kwa jamii ya kiislam au jamii yoyote inayotambua wake wengi, madhali ana ushahidi kwamba yeye alikuwa mke (na hivyo kidini na kisheria, au kiutamaduni/kimila angetambulika) angekuwa na haki zote za kushiriki msiba huo hata kama angekatazwa. Lakini hawara aka mchepuko hana base ya kufanya hivyo. Alichofanya ni vurugu, utovu wa adabu ambapo ni dhahiri kwamba vyombo vya kinidhamu na kisheria vinapaswa kumchukulia hatua za kinidhamu na kisheria.

Kwa mfano, leo kaenda kuweka shada la maua unaona ni sawa, je ungesemaje kama angeenda kunya pale kwa hoja zozote ambazo angezitoa yeye zinazompa guts za kunya? Tujitambue! Watu na wawe michepuko, wawe mahawara au marafiki kadri wajiskiavyo ila ni vema wakijua mipaka yao.
 
Nakuunga mkono, tuache kuwanyanyasa hao wanaotuhifadhi wake zetu wakitutesa. Magige nimemheshimu sana alikuwa na Upendo wa kweli. Kitendo cha kutupa ua kilionesha huyo mwanamke ni jeuri na hakuwa anampenda Marehemu
 
Wivu tu. Wakati akiwa hai mbona alitengana na mme.

Wanawake jueni ukisusa wenzako wanakula. Ningekuwa mi marehemu ningeinuka nimukatalie Unafiki wake wa kunipenda nikiwa marehemu

Kwa taarifa yako Marehemu alimwita mke wake wa Ndoa dakika za mwisho za uhai wake na ndiye amemfia mikononi mwake.
 
Nakuunga mkono, tuache kuwanyanyasa hao wanaotuhifadhi wake zetu wakitutesa. Magige nimemheshimu sana alikuwa na Upendo wa kweli. Kitendo cha kutupa ua kilionesha huyo mwanamke ni jeuri na hakuwa anampenda Marehemu
Huyo mtupa Ua akili iko kwenye mirathi tu. No more.
Afufuke huyo Madoda ndio mtaamini. Ni Mnafiki tu
 
HAKI ZA WANAWAKE sijui mko wapi kumtetea Magige asionewe. Kwani sheria inasemaje mwanamke akikaa na mwanaume zaidi ya miezi 6

Kwa scenario hiyo kwakuwa Mume alikuwa na Ndoa tena ya Kanisani hiyo miezi 6 hai apply hapa.
 
Mnakosea sana, maana mtu akifariki tunapozika tunahusisha uhusiano wa marehemu wakati akiwa hai na wafiwa. Infact kawaida kama kwenye familia ya wafiwa, Marehemu ndiye alikuwa rafiki yako; ukimaliza kuzika unarudi nyumbani. Magige alikuwa na haki zote kuweka udongo maana aliishi naye. Masuala ya ndoa ya kanisani au ya mtu binafsi (uchepukaji) hayana maana katika kuzika. Anayeguswa na kifo ni haki yake kuweka Udongo katika kaburi la Marehemu.
Huyo mtupa Ua akili iko kwenye mirathi tu. No more.
Afufuke huyo Madoda ndio mtaamini. Ni Mnafiki tu
Nadhani ni mchagga tu huyo
 
Kwa taarifa yako Marehemu alimwita mke wake wa Ndoa dakika za mwisho za uhai wake na ndiye amemfia mikononi mwake.
Kwani kumuita si kuonyesha marehemu marehemu hata kwenda akikiwa ameshikilia makosa. Nani ameanza kumtafuta mwenzake? Usikute ame mspeedisha kufa hapo hospitari. Mwanawake huwajui analia huku moyoni anacheka
 

Andika huo wosia ukidhani unawakomoa,uzuri kina Judge Mlyambina wapo,Wosia utapinduliwa kama wa Mzee Mengi. Soma kwa makini Hukumu ya Judge Mlyambina ikusaidie kuandika Wosia vizuri
 
Kivipi mkuu. Na ndio maana mimi sikutaja chochote kuhusu mirathi kwa sababu kwanza sijui kama marehemu ana nini na nini na pia sijui kama msingi wa kilichotokea ni mirathi.
Nimeongeza kasome tena tujadili.
 
Andika huo wosia ukidhani unawakomoa,uzuri kina Judge Mlyambina wapo,Wosia utapinduliwa kama wa Mzee Mengi. Soma kwa makini Hukumu ya Judge Mlyambina ikusaidie kuandika Wosia vizuri
Hahahahaa. Kama si wosia basi akaunti yake itanona .
Wanawake wanakutesa halafu wanasubiri ufe wafaidi.
Huyo aliyekutunza sheria kama hazimuelewi nitamuelewa mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…