CCM kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge Catherine Magige na wenzie kwa kuvamia msiba na kukosa utu

CCM kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge Catherine Magige na wenzie kwa kuvamia msiba na kukosa utu

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa umoja wa wanawake wa chama hicho Mkoa wa Arusha wakiongozwa na mbunge wa viti maalum, Catherine Magige.

Mbunge huyo jana Alhamisi Mei 27, 2021 alikwenda makaburini yalikokuwa yakifanyika mazishi ya mfanyabiashara Kuzula Madoda inayedaiwa kuwa ni mchumba wake. Madoda alifariki dunia Mei 24, 2021 na ameacha mke, Aziza Msuya na watoto.

Kitendo cha Catherine kwenda makaburini kiliibua hali ya sintofahamu kutokana na watu waliokuwa naye kuvunja geti na kuingia katika makaburi hayo ya familia.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na katibu wa itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka leo Ijumaa Mei 28,2021 inaeleza kuwa CCM inaheshimu katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na katiba ya CCM na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM," inaeleza taarifa hiyo.

PIA, SOMA=> Pole Catherine Magige, hii iwe fundisho kwa wadada maarufu nchini

=====

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige.

CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi
28 Mei 2021
Nani asiye kuwa na mitala katika CCM! Huyo ni mtoto amekurupuka, isije ikawa yeye akapewa onyo
 
Huyu mjinga analipwa 12,000,000 kwa mwezi na posho ya 340,000 ajili ya kugombea waume za watu? jinga kabisa hivi viti maalum vifutwe kutwa wanatafuta mabwana za watu.
Inaonesha wewe bado mtoto
 
Hujui ulisemalo. Huyo bwana kahama nyumbani mwaka Jana baada ya matokeo ya Kura. Na lilikua anakata roho alikuwa anaomba aitiwe mke wake aziza na alkua anamwonba msamaha, sijahadithiwa nilikuepo haponkwa Dr mohamed alipoingizwa kwenye chumba Cha sindano.
Lakini ni kwanini wale wapambe wa mbunge wavinje Ile gate, waingie msibani kwa nguvu, wamekuta ibada inaendelea hawakuheshimu Ile ibada mbunge akaweka shada... Halafu wakawa wanasema ccm hoyee na wapo na viongozi wa UWT? Kwanini waliingizwa mambo ya chama kwenye mambo binafsi???
Kama alihama akiwa na akili timamu Magige kosa lake nini?
Dawa ya wanawake viburi kama huyo mnayemtaja ni MATALA tu. Halafu kulia lia kinafiki si waume tukifa tutakuja kukuonana wabaya ipo siku atafufuka mtu ooooh

Magige ana Haki kuonyesha hisia zake. 2 yrs in a single bed naked mnaliona dogo.

Ngoja dawa ni kuandika mirathi hata kwa micheuko na kuirithisha tu tena naiweka kisheria zaidi
 
Huyu akivuliwa uanachama, Ndugai atachukua hatua faster na wala hatasubir kupewa barua au nyaraka yoyote kuthibitisha chama chake kimemvua uanachama.
Hivi umeona video au unakurupuka tu, unadhani CCM sawa na wajinga wengine? Haya ni masuala binafsi nakueleza wala hayahusu chama.
 
Kilchompata Catherine kinaweza mpata mwanamke yeyote yule, hata Mimi nilianzisha mahusiano na mwanaume aliniambia Hana mke walishaachana. Na akawa haishi nae. Nikiwa na mimba ya miezi Saba mke alikuja kwangu na vyeti vya ndoa,,, mke ni mkatoliki, mume mkatoliki na Mimi mkatoliki.
Haraka Sana nilivunja hayo mahusiano simply because
1. nilijua kwa Sheria ya dini yetu ni ngumu Mimi KUISHI kwa amani.
2. Nilifikiria mistakabal wa watoto na familia ya yule baba.
3. Niliona ujinga Mimi KUISHI na mwanaume ambae ndoa yake Bado haijavunjika na mkewe Bado anampenda, na nliwaza mbali hivi akifa ntakua mgeni wa Nani mimi??? Mpaka Leo yule mwanamke tunaheshimiana na anamtambua mwanangu na wanae wananiheshimu na nilimpata mwanaume wangu ambae sio mume wa MTU na maisha yanasonga.

Sasa najiuliza kama Mimi raiya wa kawaida niliweza kufanya hivi, mbunge kwanini alishindwa kujitambua??? Na mbaya zaidi yeye ni mbunge wa Wanawake,,, yeye analo JUKUMU la KUTETEA WANAWAKE na maslahi yao,,, sasa amefanya nini??? Na sio kwamba hajijui, Kuna video inasambaa anaomba Mungu ili awe official Mrs madodo, anakua kabisa yeye sio official wife, why alete taharuki misibani??
Kibaya zaidi kinachonikera Mimi ni wale viongozi wa Wanawake wakiongozwa na mwenyekiti walishindwa kutumia busara na hekima na kufanya mambo kistaarabu?? Je waliwawaza wale watoto wadogo wa marehemu pale msibani??? JASMIN BACHU TOKA HADHARAN UTUTAKE RADHI WANAWAKE WA ARUSHA.
Vipi KUHUSU ile ibada??? Kwa nini hawakuheshimu?? Na mbunge kama anampenda marehemu na alitaka azikwe kwa heshima anafahami SHERIA za kanisa katoliki?? Hawaziki MTU MWENYE mitala, YAni they are very strict kwenye hili, sasa anajuaje waliogopa kumshirikisha Ili marehem azikwe kwa heshima???
Kamwe usiskilize blabla za mwanaume eti oo nimeachana na mke wangu kisa malaya na WEWE unashkilia Hicho unajiaminisha kwamba HUYU wangu.
CATHERINE NI MBUNGE MTUNGA SHERIA, WAKATI MWINGINE ANAWAJIBIKA KUSIMAMIA SHERIA. KUISHI NA MUME WA MTU TENA MWENYE NDOA YA KIKATOLIKI AMBAYO HAIVUNJIKA HAKUKUFANYI UWE MKE KAMILI NA UWE NA HAKI YA KUMZIKA MUME AKIFA.

Barikiwa sana Dada kwa kuokoa Ndoa ya Mwanamke mwenzio,naamini sasa unaishi kwa furaha na Amani na Mume wako halali.Kwa busara zako umemwandalia mazingira mazuri sana mtoto wako kwa ndugu zake na Step Mom wake.
 
Watakuwa wanamuonea. Kama aliishi na marehemu kwa miaka miwili alitakiwa apewe nafasi ya kuweka shada. Kwa kumfungia ndio wamelikuza jambo bila sababu. Walitakiwa kuhakikisha tu kuwa mpendwa wao anazikwa kwa heshima bila vurugu. Kitendo cha kufunga geti ndicho kilichosababisha vurugu. Na CCM hawana sababu ya kuingilia maana ni mambo ya kifamilia.

Hii ndoa inaonekana ilikuwa tayari ICU wakati umauti unamkuta jamaa. Kilichokosekana ni kijikaratasi tu.

Amandla. .
Unaweza kuwa sahihi lakini hata hivyo kuna shida kutoka kwa Carherine hata maelezo yako yanaonyesha hivyo (hapo uliposema wahakikishe mpendwa wao anazikwa kwa heshima bila vurugu). Kwani kuzika kwa heshima bila vurugu ni pamoja na kuhakikisha nani ashiriki na nani asishiriki.

Ndoa ni jambo la kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila. Halikadhalika, maziko ni jambo la kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila pia. Kwa msingi huo taratibu za ndoa na maziko hazina budi kutawaliwa na matakwa ya vitu hivyo. Kwa muktadha huo, wafiwa halali (wanaotambulika ima kidini, kijamii, kisheria au kiutamaduni/kimila) wana haki na wajibu wa kusimamia namna ya kumzika mtu wao ikiwa pamoja na kuamua nani awepo na nani asiwepo katika maziko. Ni wazi Catherine si mfiwa anaetambulika na kundi lolote katika hayo niliyotaja (kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila) hivyo ushiriki wake katika maziko ulipaswa uzingatie matakwa au ridhaa ya wafiwa/wahusika. Ingeonekana mke wa marehemu amekosea iwapo Catherine angekuwa anatambulika na kundi lolote miongoni mwa hayo, hapo angekuwa na haki ya moja kwa moja ya kumzika mpendwa wake. Hata kama angekuwa mke wa sirini kama ilivyo kwa jamii ya kiislam au jamii yoyote inayotambua wake wengi, madhali ana ushahidi kwamba yeye alikuwa mke (na hivyo kidini na kisheria, au kiutamaduni/kimila angetambulika) angekuwa na haki zote za kushiriki msiba huo hata kama angekatazwa. Lakini hawara aka mchepuko hana base ya kufanya hivyo. Alichofanya ni vurugu, utovu wa adabu ambapo ni dhahiri kwamba vyombo vya kinidhamu na kisheria vinapaswa kumchukulia hatua za kinidhamu na kisheria.

Kwa mfano, leo kaenda kuweka shada la maua unaona ni sawa, je ungesemaje kama angeenda kunya pale kwa hoja zozote ambazo angezitoa yeye zinazompa guts za kunya? Tujitambue! Watu na wawe michepuko, wawe mahawara au marafiki kadri wajiskiavyo ila ni vema wakijua mipaka yao.
 
Kama alihama akiwa na akili timamu Magige kosa lake nini?
Dawa ya wanawake viburi kama huyo mnayemtaja ni MATALA tu. Halafu kulia lia kinafiki si waume tukifa tutakuja kukuonana wabaya ipo siku atafufuka mtu ooooh

Magige ana Haki kuonyesha hisia zake. 2 yrs in a single bed naked mnaliona dogo.

Ngoja dawa ni kuandika mirathi hata kwa micheuko na kuirithisha tu tena naiweka kisheria zaidi
Nakuunga mkono, tuache kuwanyanyasa hao wanaotuhifadhi wake zetu wakitutesa. Magige nimemheshimu sana alikuwa na Upendo wa kweli. Kitendo cha kutupa ua kilionesha huyo mwanamke ni jeuri na hakuwa anampenda Marehemu
 
Wivu tu. Wakati akiwa hai mbona alitengana na mme.

Wanawake jueni ukisusa wenzako wanakula. Ningekuwa mi marehemu ningeinuka nimukatalie Unafiki wake wa kunipenda nikiwa marehemu

Kwa taarifa yako Marehemu alimwita mke wake wa Ndoa dakika za mwisho za uhai wake na ndiye amemfia mikononi mwake.
 
Nakuunga mkono, tuache kuwanyanyasa hao wanaotuhifadhi wake zetu wakitutesa. Magige nimemheshimu sana alikuwa na Upendo wa kweli. Kitendo cha kutupa ua kilionesha huyo mwanamke ni jeuri na hakuwa anampenda Marehemu
Huyo mtupa Ua akili iko kwenye mirathi tu. No more.
Afufuke huyo Madoda ndio mtaamini. Ni Mnafiki tu
 
HAKI ZA WANAWAKE sijui mko wapi kumtetea Magige asionewe. Kwani sheria inasemaje mwanamke akikaa na mwanaume zaidi ya miezi 6

Kwa scenario hiyo kwakuwa Mume alikuwa na Ndoa tena ya Kanisani hiyo miezi 6 hai apply hapa.
 
Unaweza kuwa sahihi lakini hata hivyo kuna shida kutoka kwa Carherine hata maelezo yako yanaonyesha hivyo (hapo uliposema wahakikishe mpendwa wao anazikwa kwa heshima bila vurugu). Kwani kuzika kwa heshima bila vurugu ni pamoja na kuhakikisha nani ashiriki na nani asishiriki.

Ndoa ni jambo la kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila. Halikadhalika, maziko ni jambo la kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila pia. Kwa msingi huo taratibu za ndoa na maziko hazina budi kutawaliwa na matakwa ya vitu hivyo. Kwa muktadha huo, wafiwa halali (wanaotambulika ima kidini, kijamii, kisheria au kiutamaduni/kimila) wana haki na wajibu wa kusimamia namna ya kumzika mtu wao ikiwa pamoja na kuamua nani awepo na nani asiwepo katika maziko. Ni wazi Catherine si mfiwa anaetambulika na kundi lolote katika hayo niliyotaja (kidini, kijamii, kisheria na kiutamaduni/kimila) hivyo ushiriki wake katika maziko ulipaswa uzingatie matakwa au ridhaa ya wafiwa/wahusika. Ingeonekana mke wa marehemu amekosea iwapo Catherine angekuwa anatambulika na kundi lolote miongoni mwa hayo, hapo angekuwa na haki ya moja kwa moja ya kumzika mpendwa wake. Hata kama angekuwa mke wa sirini kama ilivyo kwa jamii ya kiislam madhali ana ushahidi kwamba yeye alikuwa mke (na hivyo kidini na kisheria angetambulika) angekuwa na haki zote za kushiriki msiba huo hata kama angekatazwa. Lakini hawara aka mchepuko hana base ya kufanya hivyo. Alichofanya ni vurugu, utovu wa adabu ambapo ni dhahiri kwamba vyombo vya kinidhamu na kisheria vinapaswa kumchukulia hatua za kinidhamu na kisheria.

Kwa mfano, leo kaenda kuweka shada la maua unaona ni sawa, je ungesemaje kama angeenda kunya pale kwa hoja zozote ambazo angezitoa yeye zinazopa guts za kunya? Tujitambue! Watu na wawe michepuko, wawe mahawara au marafiki kadri wajiskiavyo ila ni vema wakijua mipaka yao.
Mnakosea sana, maana mtu akifariki tunapozika tunahusisha uhusiano wa marehemu wakati akiwa hai na wafiwa. Infact kawaida kama kwenye familia ya wafiwa, Marehemu ndiye alikuwa rafiki yako; ukimaliza kuzika unarudi nyumbani. Magige alikuwa na haki zote kuweka udongo maana aliishi naye. Masuala ya ndoa ya kanisani au ya mtu binafsi (uchepukaji) hayana maana katika kuzika. Anayeguswa na kifo ni haki yake kuweka Udongo katika kaburi la Marehemu.
Huyo mtupa Ua akili iko kwenye mirathi tu. No more.
Afufuke huyo Madoda ndio mtaamini. Ni Mnafiki tu
Nadhani ni mchagga tu huyo
 
Kwa taarifa yako Marehemu alimwita mke wake wa Ndoa dakika za mwisho za uhai wake na ndiye amemfia mikononi mwake.
Kwani kumuita si kuonyesha marehemu marehemu hata kwenda akikiwa ameshikilia makosa. Nani ameanza kumtafuta mwenzake? Usikute ame mspeedisha kufa hapo hospitari. Mwanawake huwajui analia huku moyoni anacheka
 
Kama alihama akiwa na akili timamu Magige kosa lake nini?
Dawa ya wanawake viburi kama huyo mnayemtaja ni MATALA tu. Halafu kulia lia kinafiki si waume tukifa tutakuja kukuonana wabaya ipo siku atafufuka mtu ooooh

Magige ana Haki kuonyesha hisia zake. 2 yrs in a single bed naked mnaliona dogo.

Ngoja dawa ni kuandika mirathi hata kwa micheuko na kuirithisha tu tena naiweka kisheria zaidi

Andika huo wosia ukidhani unawakomoa,uzuri kina Judge Mlyambina wapo,Wosia utapinduliwa kama wa Mzee Mengi. Soma kwa makini Hukumu ya Judge Mlyambina ikusaidie kuandika Wosia vizuri
 
Andika huo wosia ukidhani unawakomoa,uzuri kina Judge Mlyambina wapo,Wosia utapinduliwa kama wa Mzee Mengi. Soma kwa makini Hukumu ya Judge Mlyambina ikusaidie kuandika Wosia vizuri
Hahahahaa. Kama si wosia basi akaunti yake itanona .
Wanawake wanakutesa halafu wanasubiri ufe wafaidi.
Huyo aliyekutunza sheria kama hazimuelewi nitamuelewa mimi
 
Back
Top Bottom