CCM kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge Catherine Magige na wenzie kwa kuvamia msiba na kukosa utu

CCM kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge Catherine Magige na wenzie kwa kuvamia msiba na kukosa utu

Hivi umeona video au unakurupuka tu, unadhani CCM sawa na wajinga wengine? Haya ni masuala binafsi nakueleza wala hayahusu chama.
Kwanini walikua wanasema CCM hoyee kule msibani?? Kama ni mambo binafsi why walkua wanatumia nembo za chama???
 
kuandikwa kwenye wosia kitu gani, aliandikwa Jacqueline Ntuyabaliwe aliyekua akiaminisha hadi wajinga mitandaoni jui ya happy life yao na kujiita Mrs Mengi, ndio sembuse huyo Mh. mgawaji bureer
Mimi nimesema kwenye mirathi Catherine hana nafasi, hilo la wosia linatoka wapi? Au haukunielewa niliposema kuwa tatizo litajitokeza kama hati itakuwa kwa jina la Catherine? Au haujui mtu ana haki ya kuuza mali yake na aliyeuziwa kubadilisha hati milki baada ya kumaliza malipo?

Unawaangusha wataalam wenzako.

Amandla...
 
kuandikwa kwenye wosia kitu gani, aliandikwa Jacqueline Ntuyabaliwe aliyekua akiaminisha hadi wajinga mitandaoni jui ya happy life yao na kujiita Mrs Mengi, ndio sembuse huyo Mh. mgawaji bureer
HAHAHAAAAAAAAAAAAAAAAAA energy Jambo ntalipaa
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa umoja wa wanawake wa chama hicho Mkoa wa Arusha wakiongozwa na mbunge wa viti maalum, Catherine Magige.

Mbunge huyo jana Alhamisi Mei 27, 2021 alikwenda makaburini yalikokuwa yakifanyika mazishi ya mfanyabiashara Kuzula Madoda inayedaiwa kuwa ni mchumba wake. Madoda alifariki dunia Mei 24, 2021 na ameacha mke, Aziza Msuya na watoto.

Kitendo cha Catherine kwenda makaburini kiliibua hali ya sintofahamu kutokana na watu waliokuwa naye kuvunja geti na kuingia katika makaburi hayo ya familia.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na katibu wa itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka leo Ijumaa Mei 28,2021 inaeleza kuwa CCM inaheshimu katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na katiba ya CCM na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM," inaeleza taarifa hiyo.

PIA, SOMA=> Pole Catherine Magige, hii iwe fundisho kwa wadada maarufu nchini

=====

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige.

CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi
28 Mei 2021
Katika uhalisia marehemu alishamchagua yeye, na akamkataa huyo mwingine kwanini wanaingilia maamuzi ya marehemu, angekua hai wangemlazimisha? wanatakiwa kusimamia na kuheshimu maamuzi ya marehemu. viongozi wawe washauri ktk kulinda haki na maamuzi halisi ya watu
 
Yes. Polisi walikua watu w akwanza kudeal naye.

Pili, chama kinapaswa kumchukulia maadili kwakua kuna misingi na kanuni za kuyaishi anayopaswa kuishi kama mwanachama wa chama cha mapinduzi na mbunge anayewakilisha wanamama na watoto bungeni kwa kutunga na kutetea sheria zao. Yeye anayaishi?

Yale ni maisha yake binafsi na wala hayana mahusiano na chama chake, na wala hakwenda pale kama mwanachama wa CCM au mbunge bali kama Catherine 'hawara' wa marehemu...

CCM wanataka tu kutumia hili tukio kisiasa, baada ya kupima upepo waonekane wao ni wema sana...

Kama hao CCM wangelikuwa ni wema sana au wanafuatilia maadili ya wabunge/wanachama wao, je walikuwa qapi miaka yote huyo Cathy akijirusha na marehemu?

Na sijui wewe umeona wapi hao polisi waliyedeal naye, ila clips za video nilizoona mimi zimeonesha tu wafuasi wakibamiza bamiza geti waruhusiwe kuingia kwenye shamba/eneo la maziko, then huyo bi mdogo akaenda moja kwa moja kuweka shada, mjane analiondoa kwa kulirusha mbali na kaburi, then huyo bi mdogo akasepa zake huku wapambe wakijinadi wamefanikisha azma yao kwamba Cathy kamzika hawara yake...mwisho akagoma kutoa kauli yoyote kwa wanahabari waliokuwepo na kusepa...
 
Wafute hivyo viti maalumu, hizo kodi zetu wanazolipwa wanazitumia kuhonga waume za watu, na kukaa nao bar hadi usiku wa manane..... maneeenah zao!!!
Hahaha kaombe na wewe upate viti maalumu uhonge hao waume za watu,acha wivu na fikra potofu.
 
Yale ni maisha yake binafsi na wala hayana mahusiano na chama chake, na wala hakwenda pale kama mwanachama wa CCM au mbunge bali kama Catherine 'hawara' wa marehemu...

CCM wanataka tu kutumia hili tukio kisiasa, baada ya kupima upepo waonekane wao ni wema sana...

Kama hao CCM wangelikuwa ni wema sana au wanafuatilia maadili ya wabunge/wanachama wao, je walikuwa qapi miaka yote huyo Cathy akijirusha na marehemu?

Na sijui wewe umeona wapi hao polisi waliyedeal naye, ila clips za video nilizoona mimi zimeonesha tu wafuasi wakibamiza bamiza geti waruhusiwe kuingia kwenye shamba/eneo la maziko, then huyo bi mdogo akaenda moja kwa moja kuweka shada, mjane analiondoa kwa kulirusha mbali na kaburi, then huyo bi mdogo akasepa zake huku wapambe wakijinadi wamefanikisha azma yao kwamba Cathy kamzika hawara yake...mwisho akagoma kutoa kauli yoyote kwa wanahabari waliokuwepo na kusepa...
Mbona unachanganya mambo? Nani kasema alivamiwa na mapolisi wakati yeue ndo aliyeongozana nao? Sijui ni wewe ama mwingine huko juu aliyesema polisi ilibidi ndo wadeal na magige kwa kuinvade yeye na genge lake kwenye mji wa watu nami nikakubaliana na hoja yake sijui yako yes polisi walipaswa kuanza kuwajibika na magige pale pale ila kwakua madaraka yanatumika vibaya basi wakawa kama ndugu wasikilizaji.

And yes, yeye magige amepewa ruhusa ya kuhudhuria msibanj kama nani wa marehemu? Mnajua jitambueni na ujinga uwatoke? Hana haki yoyote ya msingi. Yeye ni kiongozi. Na anapaswa kutaishi maadili ya uongozi tena hasa ya chama chake na kanuni zinavyomtaka kulinda na kutetea haki za wanawake wenziye na watoto. Katarina amevuruga ndoa za wangapi? Ama wewe umemjua leo? Katarina ni kahaba mzoefu. Huyuhuyu mume wa aziza mnayetetea sijui katarina ndi kipenzi chake ndo huyihuyo katarina ameenda msaliti kwa mwanaume mwingine halaf wasema nn? Katarina ana bwana mmoja? Ama tufungulie vaults hapa tukimbiane? Anapaswa kuwajibishwa. Na ikibidi hata wale walioongozana naye wale viongozi wenzake.
Kama it was personal kwaninj aliongozana na mpk mbunge na wengineo mpk wamama wa UWT. Usijitoe ufahamu asilani. Na zaidi tukasikia ccm hoyeeee.
Halafu ukishakua kiongozi maisha yako uhuru umeahanunuliwa. Kama yeye kahaba anadhulumu haki za wengine je yeye tutamuamini vipi anaweza kulinda na kutetea wanyonge waliokosa sauti. Unafahamu kwamba huyu ni mtunga sheria? Tusijadili hata elimu yake na historia yake maana ni kinyaa. Eti katarina naye mtunga sheria. Hawa UWT umalaya umewajaa tu majority.
 
Sasa munachanganyaje mambo ya Kifamilia na masuala ya siasa? Hii nchi ina mambo ya ovyo sana
 
Katika uhalisia marehemu alishamchagua yeye, na akamkataa huyo mwingine kwanini wanaingilia maamuzi ya marehemu, angekua hai wangemlazimisha? wanatakiwa kusimamia na kuheshimu maamuzi ya marehemu. viongozi wawe washauri ktk kulinda haki na maamuzi halisi ya watu
Aziza ndoa aliishindwa bwana Madoda akamchagua Cathy,kwanini Cathy anatukanwa? Mambo ya mirathi na makaratasi na dini achana nayo.Mpenzi wa bwana Mwendazake Ni Cathy period.
 
Back
Top Bottom