CCM kumuita Lissu kibaraka wa mabeberu haitusaidii. Watanzania ni waelewa sana

CCM kumuita Lissu kibaraka wa mabeberu haitusaidii. Watanzania ni waelewa sana

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
CCM let's be matured, hii propaganda ya kumuita Tundu Lissu kibaraka wa mabeberu imebumba tutafute neno lingine zuri la kummaliza.

Kutumia hili neno hakujabadili kitu kabisa mtaani kila ninapopita sioni sehemu yeyote akiitwa Bebebru zaidi ya kuitwa Mkombozi, mimi sijui ni mkombozi wa nini.

Unamwitaje mtu kibaraka wa beberu wakati hakuna walichomtuma? Hatuna ushahidi ni vipi mabeberu wanatumia Lissu. Mbaya zaidi kila anachokiongea Lissu ni msumari kwetu maana anasema kweli tupu.

Anakotumaliza Lissu ni pale anakotuita sisi CCM mafisadi na wanyang'anyi tinamjibu vipi wakati maheka mengi ya Ardhi wastaafu wetu wanamiliki? Hakuna mahali ambapo tumewahi kusikia Lissu kaiba au kala cha mtu.
 
Tatizo walianza kumuita majina mabaya zamani, so he had all the time in this world, kujibu tuhuma na propaganda hizo.

Vilevile Tundu Lissu ana historia yake ya uanaharakati, misimamo isiyoyumba, na kutetea haki, tangu miaka ya 90.

Sasa mtu ambaye wananchi wanafahamu misimamo yake kwa miaka zaidi ya 20, huwezi kumbomoa kwa propaganda za miaka 3, tena baada ya mtu huyo kuwa ameshambuliwa kinyama kwa marisasi.
 
"..kama ni reli na madaraja hata wakoloni walijenga..." na Tundu Antipasi Lissu.

Watu wazima tunajua kuwa wakoloni walijenga miundombinu kwa ajili ya kupitisha mali ghafi kwenda kwao sio kwa maendeleo ya makoloni yao! Lissu Urais utapata tu huko Ubelgiji na sio Tanzania.
 
"..kama ni reli na madaraja hata wakoloni walijenga..." na Tundu Antipasi Lissu.

Watu wazima tunajua kuwa wakoloni walijenga miundombinu kwa ajili ya kupitisha mali ghafi kwenda kwao sio kwa maendeleo ya makoloni yao! Lissu Uraisutapata tu huko Ubelgiji na sio Tanzania

..hoja ni kwamba jengeni miundombinu lakini mjitofautishe na wakoloni.
 
"..kama ni reli na madaraja hata wakoloni walijenga..." na Tundu Antipasi Lissu.
Watu wazima tunajua kuwa wakoloni walijenga miundombinu kwa ajili ya kupitisha mali ghafi kwenda kwao sio kwa maendeleo ya makoloni yao! Lissu Uraisutapata tu huko Ubelgiji na sio Tanzania
Hujasikia Magufuli anajenga sgr kwenda Rwanda ili ipitishe mizigo ya Rwanda kwenda bandari ya Dar kisha Ulaya. CCM na Wakoloni akili zao ni sawa. Kama ccm inawajali raia ijenge sgr ya kutoka Dsrm kwenda Mtwara au Mbeya to Tabora kurahisisha movement ya watu na mizigo

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuchora mstari wa tofauti kati ya ccm na mkoloni mjerumani au Mwingereza. Tena mara elfu ya mkoloni alitupa elimu tikawa na akili tukaweza kumdai atupe uhuri wetu
 
Na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato umejengwa kwa manufaa ya nani?
Kufungua Mkoa wa Geita: utalii, dhahabu, nk. mbona hutaji viwanja vingiene vipya vinavyojengwa au kwa kuwa kasema Lissu kuhusu Chato? JPM atapita ila uwanja utatumiwa vizazi na vizazi!
 
Kufungua Mkoa wa Geita: utalii, dhahabu, nk. mbona hutaji viwanja vingiene vipya vinavyojengwa au kwa kuwa kasema Lissu kuhusu Chato? JPM atapita ila uwanja utatumiwa vizazi na vizazi!

Tungeona dalili zake sasa hivi akiwa Rais.

..uwanja huo unaweza kuwa kama ule wa kijijini kwa Mobutu Sese Seko.
 
Kufungua Mkoa wa Geita: utalii, dhahabu, nk. mbona hutaji viwanja vingiene vipya vinavyojengwa au kwa kuwa kasema Lissu kuhusu Chato? JPM atapita ila uwanja utatumiwa vizazi na vizazi!
Kwa hoja yako hiyo hiyo, kwani hao wakoloni unaosema walijenga reli ili watuibie, waliondoka na reli zao si wameziacha hadi leo ndio tunazotumia?
 
Mnamponza lisu, wabelgiji wanampulia kisogoni kila siku.
 
Hujasikia Magufuli anajenga sgr kwenda Rwanda ili ipitishe mizigo ya Rwanda kwenda bandari ya Dar kisha Ulaya. CCM na Wakoloni akili zao ni sawa. Kama ccm inawajali raia ijenge sgr ya kutoka Dsrm kwenda Mtwara au Mbeya to Tabora kurahisisha movement ya watu na mizigo

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuchora mstari wa tofauti kati ya ccm na mkoloni mjerumani au Mwingereza. Tena mara elfu ya mkoloni alitupa elimu tikawa na akili tukaweza kumdai atupe uhuri wetu
Kweli wewe nyumbu. Unalinganisha reli ya mkoloni na sgr kwa matumizi.
Reli ya mkokoni ilitumiwa na mwafrika?
 
..walisema Tundu Lissu ameongea na Deo Mwanyika, hivyo ni msaliti na anapaswa kuuwawa.

..baada ya hapo Deo Mwanyika ameteuliwa kuwa mgombea ubunge wa CCM.

..unaona jinsi CCM walivyo wapumbavu?
Ni rahisi tu. Mwanyika ameelewa kisa na kuamua kuwa mzalendo. Huyu mbu wenu bado anataka kushindana na serikali. Atakwisha si muda.
 
Back
Top Bottom