CCM kunawaka moto, wakubwa waanza kulaumiana issue za Musiba, Mangula

mkuu upo meatu ipi,miye nipo huku posta ya zamani
 
Mtu kashafariki siku nyingi lakini roho haitaki kuacha mwili - Hii ndiyo CCM yangu...tunaishi kwa nguvu ya Betri....alternator ishakufa kitambo sana....

sasa msishangae siku mkiamuka gari halipigi.....
 
Naona unapambia suala kulikuza hata kuliko lilivyo kihalisi. Mahali po pote palipo na wengi, kutakuwepo na mawazo mengi. Haiwezekani watu wote wakawa na wazo moja tu. La muhimu ni kwamba suala likiisha amuliwa, hata wale waliokuwa na mawazo tofauti waunge mkono huo uamuzi. Hiyo ndiyo demokrasia.

Kwa mfano, kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, wana CCM wote waliotaka kugombea urais walialikwa kujitokeza, na wengi walifanya hivyo. Madaraka husika yalichuja majina hayo yakabainisha wanachama wanane, kama sikosei, wenye sifa stahili, akiwemo Lowasa. Majina hayo yalipelekwa mbele. Pamoja na kwamba wote wanane walikuwa na sifa, lakini wengine walifaa zaidi, sawasawa na kwenye mtihani mmoja atashinda kwa kupata 50%; mwenzake akashinda kwa kupata 90%. Wote wameshinda lakini kama anatakiwa mmoja tu, yule mwenye maksi kubwa zaidi ndiye atachukuliwa.

Katika kuwachuja hao wanane, watatu walienguliwa (nadhani akiwemo Lowasa); wakabaki watano. Watano hao wakaenda mbele na wawili wakaondolewa wakabaki watatu. Uchujwaji uliofuatilia ukamchagua John Magufuli kuwa ndiye mwenye maksi za kuwapita wote, na kwa hiyo ndiye akapitishwa kuwa mgombea wa CCM. Hiyo ndiyo demokrasia yenyewe. Tatizo likaja kwamba Lowasa alitaka yeye tu ndiye apitishwe. Kwa kuwa haikuwa hivyo, akaamua kuachana na Chama. Sawa. Ana uhuru huo. Hili ndiyo tatizo pia la Membe: anajiona anafaa kuwa mgombea wa CCM. Chama kinaona kweli anafaa, lakini kuna mwanachama mwingine anayefaa zaidi. Kwa hiyo yeye ameachwa. Aidha, CCM waliamua kuwa kama Rais amekuwa madarakani kwa miaka mitano, kwenye uchaguzi ufuatao yeye tu ndiye awe mgombea wa CCM ili awe Rais kwa miaka mingine mitano, kufanya urais wake kuwa na jumla ya miaka kumi. Membe anakataa hilo. Huku ni kukiuka maadili ya chama. Yeye ni nani kwamba mawazo yake tu ndiyo yafuatwe kuacha makubaliano ya chama. Kama anaona hayo maadili ya kiutendaji yanayokuwepo si sahihi, basi afuate ngazi husika ili yabadilishwe. Siyo kuleta maneno maneno kwamba yeye tu ndiye achaguliwe. Ingekuwaje mwaka 2015 kama kila mmoja wa wale wagombea wanane angekomalia yeye tu ndiye ateuliwe kugombea? Ingekuwa fujo na demokrasia ingefutika. Demokrasia haimaanishi wewe peke yako tu ndiye upitishwe. Maana ya demokrasia ni wengi wape.
 
Ningekuwa karibu ningemwagia petrol ili kiwake zaidi
 
Ni ujinga kumcheka adui yako kisa ameshika bunduki vibaya wakati hata panga huna. Unasahau kwamba ile bunduki ipo kwa ajili yako.
 
Membe, ameonewa sana na kudhalilishwa sana.
Mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni.
Katiba ya chama ndio mahala pake kutumika ipasavyo,ili haki ipatikane.
Mangula mustakabal wake ufahamike sawia.
 
Tangu mwaka 1985 CCM kulikua kunawakaga moto ila huo moto ni kitu kinapikwa bwana mdogo kikiiva watauzima
 
Majungu tu hayo.
 
Jitahidi kutokujihusisha na umbea. Jihadhari na corona. Nawa mikono, kaa mita moja karibu na mtu mwingine na fuatilia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya.
 
Siasa za ccm kila unapokaribia uchaguzi mkuu hua kunafukuta moshi na watia nia hua wanafikia 40 lakn mwisho wa siku anaeteuliwa ni mmoja ndo huyo huyo analiongoza taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…