CCM kutawala karne nyingine ijayo

Siyo lazima kuondoka kwake iwepo nguvu toka nje yake, itajisambaratisha yenyewe sababu ya kugombea madaraka na maslahi
Basi tuendelee kumuomba MUNGU hili litimie. tupange strong block ndani ya CCM
 
Wasomali walikuwa Watu wa kwanza kuziunganisha Nchi zao na walikuwa ni wapole sana.

Hata Watigrai walikuwa ni watu wapole na waelewa

Watu wa Ubangishari pia walikuwa ni wapole kupita kiasi lakini leo wameingia kwenye machafuko yasioisha pamoja na vifaru na bunduki zote lakini hazikufua dafu.
 
Tumbe hili la kumwaga damu lisitokee, lkn bila katiba mpya hata mtu asipoteze muda wake kuombea Urais kupitia vyama mbadala.
 
Tumbe hili la kumwaga damu lisitokee, lkn bila katiba mpya hata mtu asipoteze muda wake kuombea Urais kupitia vyama mbadala.
Ndugu,soma historia ya Nchi za Kiafrika zilizokumbwa na machafuko

Hakuna Mtu Duniani anayeomba kumwaga Damu ila huwa wanajikuta wameingia kwa sababu kama hizi.
 
Umesahau,

DPP ambaye anashitaki watu ama kuwafutia mashitaka akitaka yeye pia anateuliwa na Mwenyekiti wa CCM. Kwa maneno mengine huyo anayeshitaki na yule anayechunguza mashitaka hayo kama yana ukweli ama laah yaani Jaji - wote ni wateule wa Mwenyekiti wa CCM taifa.
 
Hivi ni kwanini Rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu wa itikadi tofauti , wengine hawana hata chama anakuwa mwenyekiti wa Chama cha Siasa? Kwanini katiba isimkataze ili abaki kuwa wa wote kama alivychaguliwa na wote?
 
Suala la kutenganisha kofia mbili ilikuwa hoja ya moto sana ndani ya CCM kwamba Rais wa nchi asiwe mwenyekiti wa chama cha siasa.

Waligoma katu katu..waulize kwa nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…