CCM kwa sasa ina machaguo mawili tu. Kumtosa Rais Samia na wenzie waliotufikisha hapa ianze upya au kuikosa Ikulu 2025

CCM kwa sasa ina chaguzi mbili tu, kumtosa Rais Samia na wenzie waliotufikisha hapa ianze upya au kuikosa Ikulu 2025​

Nchi imechafuka, wananchi wamekasirika kwa kuwa wameujua ukweli kwamba CCM na Serikali yake si rafiki, ni adui yao,na haiwezi kabisa kuwafikisha Kanani, nchi ya maziwa na asali. CCM kwa sasa ina options mbili tu,au imtose Samia na wenzake waliotufikisha hapa ianze upya, au iikose Ikulu 2025.

Ni ukweli usiopingika, kwamba nchi yetu haijawahi kuwepo katika sintofahamu ya namna hii tangu tupate Uhuru wetu mwaka 1961. Ndio CCM na serikali zake mbali mbali zimetufanyia mambo mengi mabaya:Vijiji vya Ujamaa,sera ambayo iliingiza Watanzania kwenye umaskini uliotopea;kutaifisha mali za walioitwa wanyonyaji na hatimaye kuharibu uchumi wa nchi kabisa; mikataba mingi mibovu: MEREMETA, KAGODA, SYMBION, IPTL, ATCL, TRC nk., lakini nchi haijawahi kukosa amani na Wananchi wakalalamika na kuichukia serikali yao kiasi hiki.

Hii ni kwa nini? Ni kwa sababu wananchi wamekosa imani kabisa na mfumo mzima wa utawala. Hawana imani tena na utawala wowote wa CCM na Serikali zake,wanataka mabadiliko chanya. Unaweza ukauvuta mpira kwa kiasi fulani, lakini hatimaye unafikia ukomo wa kuvutika(elastic limit) na kukatika.Ndio, Watanzania wamefikia ukomo wa uvumilivu.CCM sasa ina chaguzi mbili tu ili angalau kujisafisha:au iachane na Samia na kufanya kama kile kilichofanyika Uingereza kwa kuachana na Waziri Mkuu Boris Johnson na kumuweka Waziri Mkuu wa sasa Rishi Sunak madarakani,au iparaganyike kabisa na kupotea kwenye ulingo wa siasa, huku ikisubiri uchaguzi mkuu 2025.Ndio uaminifu na heshima ya wananchi kwa CCM vimeshashuka sana, lakini angalau wananchi wataona kwamba CCM imetambua makosa yake na iko tayari kujirekebisha.

Ni nini kimeibua yote haya. Hakuna shaka yeyote kwamba mkataba mbovu wa DP World ambao kwa kipimo chochote ni mkataba mbovu,ndio uliofukua makaburi. Legal Human Rights Centre(LHRC) wamesema bila kumung'unya maneno, kwamba mkataba huu una matatizo mengi.

Katibu Mkuu wa CCM Comrade Chongolo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Comrade Kinana nao wameonyesha wasi wasi wa wazi katika mkataba huu.

Sababu zinazotolewa na mamlaka za kutafuta muwekezaji kwenye bandari zetu ni kama ifuatavyo:

1.Watanzania ni wezi.
Sababu hii si ya msingi sana,kwa kuwa kama walioajiriwa Bandarini ni wezii,wangefukuzwa na kuajiriwa wengine waadilifu.Isitoshe Watanzania tupo million sitini(60) na zaidi,naamini kusinge-kosekana Watanzania waaminifu.Naomba niseme hivi, sababu hii ambayo si ya kweli, imetudhalilisha sana Watanzania kwenye jamii ya kimataifa.Katika jamii yeyote wezi wapo,si ajabu.Sasa kusema kwamba Watanzania ni wezi,ni kutudhalilisha na kutukosea Watanzania heshima,kwa hiyo katika hili, tunaomba tuombwe radhi.

2.Watanzania hawana weledi wa kuendesha bandari.
Inawezekana hii ni kweli,lakini kama ni kweli,CCM na serikali zake mbali mbali tangu Uhuru wanahusika moja kwa moja katika tatizo hili kwa kuharibu Elimu yetu.

Kulikuwa na sababu gani za msingi kwa mfano za kutumia waalimu wa Darasa la Saba.Kulikuwa na sababu gani za kuwa na Elimu ya UPE(Universal Primary Education).Kwa nini mitaala mibovu.Kuna haja gani ya kubadilisha mitaala kila wakati na hivyo kukosa consistency.Kuna sababu gani ya msingi ya kuajiri waalimu wa Division IV tena,wa course ya ualimu ya mwaka mmoja tu(Voda Fasta).Kulikuwa na ulazima gani na haraka gani ya kuanzisha Shule za Kata,huku tukijua kwamba hazina vifaa,waalimu wanaofaa na mazingira mazuri ya kufundishia na mengine mengi?Jibu ni moja tu,nia ni kuharibu elimu,ili kusiwe na watu wenye weledi wa kusimamia rasilimali zao na maendeleo ya nchi yao.

Labda katika swala la Watanzania kutokuwa na weledi unaotakiwa kuendesha bandari,niongeze jambo lingine la msingi.Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tabia ya kutoa ajira kindugu na kujuana.Sina shaka yeyote kwamba mfumo huu wa ajira ume-compromise sana weledi,na hii haijaathiri utendaji Bandarini pekee tu,lakini serikalini kwa ujumla na kwenye mashirika yote.Na hapa niseme wazi,CCM na serikali zake zote inahusika,kwa kuwa haijaisimamia serikali zake vizuri kudhibiti uovu huu.

Kumekuwa na harakati nyingi kutoka CCM na serikali yake kuutetea mkataba huu kati ya Serikali na DP World. Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mkataba huu kwa kipimo chochote haufai,kwa hiyo kimsingi hakuna sababu yeyote ya kuendelea kuutetea na kulazimisha kuutekeleza, kwa kuwa wananchi hawautaki,na sababu kwa nini hawautaki iko wazi,hauna maslahi kwa Taifa lao.Kuendelea kuutetea na kuonyesha nia ya kuutekeleza ni kuendelea kuwatia wananchi hasira na ningeishauri CCM iache.

Hapa naomba niwe muwazi,Watanzania hawakatai uwekezaji katika bandari zao,au hata bandari ya Dar es Salaam, wanachokataa ni uwekezaji usio na maslahi kwao na taifa lao.
Wananchi Hawa Hawa ndio wamechoka au unazungumzia wananchi wa taifa gani

Ccm inajiamini Sana hat wamejuwa kbsa hate tupige kelele VIP ss hatuwezi kufanyatafiti lolote pia ,,baada ya ccm kugundua kuwa cc Ni vilaza wameamua kufanya lolote juu ya Mali na rasilimali za inch hi na hakuna wa kupinga

Jana nimesikia boda dar wameandamana wanataka dp aje Mara moja
 
Thubutu. Nani wa kumweka pembeni mwenyekiti wakati ndiyo final sayer. Labda aamue kuachia mwenyewe. Au Mungu aweke mkono wake kama alivyofanya kwa wana wa Israel
Mungu ataweka mkono wake mkuu,hawezi kukubali Watanzania wateseke indefinitely.
 
Wananchi Hawa Hawa ndio wamechoka au unazungumzia wananchi wa taifa gani

Ccm inajiamini Sana hat wamejuwa kbsa hate tupige kelele VIP ss hatuwezi kufanyatafiti lolote pia ,,baada ya ccm kugundua kuwa cc Ni vilaza wameamua kufanya lolote juu ya Mali na rasilimali za inch hi na hakuna wa kupinga

Jana nimesikia boda dar wameandamana wanataka dp aje Mara moja
Yalitokea Mali,Burkina Faso na recently Niger unayajua na kwa mazingira haya haya ya kwetu?Okay,tusubiri Mungu ni mwaminifu,naamini hatakubali CCM iendelee kutesa watu wake.
 
Huna huo ushahidi wa uiitayo HARAMU.....

Nje ya CCM kuna wanasiasa waigizaji tu [emoji1787]
Mimi nina ushahidi mkuu,kijana wangu alikwenda kusimamia uchaguzi.Walipewa form za uchaguzi tupu waka tick,na wakaambiwa na jamaa wa Usalama Taifa kwamba atakayetoa siri atashuhulikiwa.
 
Nchi ilichafuka baada ya Dr.Slaa na Prof.Lipumba kugundua kuwa mh.Mbowe "alilambishwa ya KAIZARI MWACHIE KAIZARI"...Lipumba akakimbilia Rwanda [emoji1787][emoji1787]

Nje ya CCM hakuna siasa......
CCM hakuna siasa mkuu,kuna uhuni.
 
Wananchi Hawa Hawa ndio wamechoka au unazungumzia wananchi wa taifa gani

Ccm inajiamini Sana hat wamejuwa kbsa hate tupige kelele VIP ss hatuwezi kufanyatafiti lolote pia ,,baada ya ccm kugundua kuwa cc Ni vilaza wameamua kufanya lolote juu ya Mali na rasilimali za inch hi na hakuna wa kupinga

Jana nimesikia boda dar wameandamana wanataka dp aje Mara moja
Wamelambishwa asali hao sio wao mkuu.
 
Mimi nina ushahidi mkuu,kijana wangu alikwenda kusimamia uchaguzi.Walipewa form za uchaguzi tupu waka tick,na wakaambiwa na jamaa wa Usalama Taifa kwamba atakayetoa siri atashuhulikiwa.
Kwa hiyo hao jamaa walijitambulisha kuwa ni usalama wa taifa ?!! [emoji15][emoji15][emoji15]

Kama ni USALAMA WA TAIFA kuna ubaya gani kwani Taifa ni lazima liwe salama ?!! [emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Yalitokea Mali,Burkina Faso na recently Niger unayajua na kwa mazingira haya haya ya kwetu?Okay,tusubiri Mungu ni mwaminifu,naamini hatakubali CCM iendelee kutesa watu wake.
Hukuna jeshi Happ la kufanya mapinduzi hakuna wote Ni vilaza tu wanajeshi wengi wanafikiria mapenz tu Sasa hv
 
Mungu ataingilia kati na kutoa ukilaza wao mkuu,kama amepanga kutumia Jeshi.Na kwani Askari wa Mali,Sierra Leone na Niger wana kitu gani zaidi ya Askari wa kwetu.
But finally remember there is nothing impossible to God.Anaweza akatumia mbinu nyingine kabisa ambayo hakuna hata mtu anayeifikiria.
 
CCM kwa sasa ina chaguzi mbili tu, kumtosa Rais Samia na wenzie waliotufikisha hapa ianze upya au kuikosa Ikulu 2025​

Nchi imechafuka, wananchi wamekasirika kwa kuwa wameujua ukweli kwamba CCM na Serikali yake si rafiki, ni adui yao,na haiwezi kabisa kuwafikisha Kanani, nchi ya maziwa na asali. CCM kwa sasa ina options mbili tu,au imtose Samia na wenzake waliotufikisha hapa ianze upya, au iikose Ikulu 2025.

Ni ukweli usiopingika, kwamba nchi yetu haijawahi kuwepo katika sintofahamu ya namna hii tangu tupate Uhuru wetu mwaka 1961. Ndio CCM na serikali zake mbali mbali zimetufanyia mambo mengi mabaya:Vijiji vya Ujamaa,sera ambayo iliingiza Watanzania kwenye umaskini uliotopea;kutaifisha mali za walioitwa wanyonyaji na hatimaye kuharibu uchumi wa nchi kabisa; mikataba mingi mibovu: MEREMETA, KAGODA, SYMBION, IPTL, ATCL, TRC nk., lakini nchi haijawahi kukosa amani na Wananchi wakalalamika na kuichukia serikali yao kiasi hiki.

Hii ni kwa nini? Ni kwa sababu wananchi wamekosa imani kabisa na mfumo mzima wa utawala. Hawana imani tena na utawala wowote wa CCM na Serikali zake,wanataka mabadiliko chanya. Unaweza ukauvuta mpira kwa kiasi fulani, lakini hatimaye unafikia ukomo wa kuvutika(elastic limit) na kukatika.Ndio, Watanzania wamefikia ukomo wa uvumilivu.CCM sasa ina chaguzi mbili tu ili angalau kujisafisha:au iachane na Samia na kufanya kama kile kilichofanyika Uingereza kwa kuachana na Waziri Mkuu Boris Johnson na kumuweka Waziri Mkuu wa sasa Rishi Sunak madarakani,au iparaganyike kabisa na kupotea kwenye ulingo wa siasa, huku ikisubiri uchaguzi mkuu 2025.Ndio uaminifu na heshima ya wananchi kwa CCM vimeshashuka sana, lakini angalau wananchi wataona kwamba CCM imetambua makosa yake na iko tayari kujirekebisha.

Ni nini kimeibua yote haya. Hakuna shaka yeyote kwamba mkataba mbovu wa DP World ambao kwa kipimo chochote ni mkataba mbovu,ndio uliofukua makaburi. Legal Human Rights Centre(LHRC) wamesema bila kumung'unya maneno, kwamba mkataba huu una matatizo mengi.

Katibu Mkuu wa CCM Comrade Chongolo(chini mwisho) ameeleza kwamba ipo haja ya kusikiliza wadau wengine na mawazo Yao kufanyiwa kazi.Comrade Kinana naye ametoa msimamo unaofanana na Comrade Chongolo

Sababu zinazotolewa na mamlaka za kutafuta muwekezaji kwenye bandari zetu ni kama ifuatavyo:

1.Watanzania ni wezi.
Sababu hii si ya msingi sana,kwa kuwa kama walioajiriwa Bandarini ni wezii,wangefukuzwa na kuajiriwa wengine waadilifu.Isitoshe Watanzania tupo million sitini(60) na zaidi,naamini kusinge-kosekana Watanzania waaminifu.Naomba niseme hivi, sababu hii ambayo si ya kweli, imetudhalilisha sana Watanzania kwenye jamii ya kimataifa.Katika jamii yeyote wezi wapo,si ajabu.Sasa kusema kwamba Watanzania ni wezi,ni kutudhalilisha na kutukosea Watanzania heshima,kwa hiyo katika hili, tunaomba tuombwe radhi.

2.Watanzania hawana weledi wa kuendesha bandari.
Inawezekana hii ni kweli,lakini kama ni kweli,CCM na serikali zake mbali mbali tangu Uhuru wanahusika moja kwa moja katika tatizo hili kwa kuharibu Elimu yetu.

Kulikuwa na sababu gani za msingi kwa mfano za kutumia waalimu wa Darasa la Saba.Kulikuwa na sababu gani za kuwa na Elimu ya UPE(Universal Primary Education).Kwa nini mitaala mibovu.Kuna haja gani ya kubadilisha mitaala kila wakati na hivyo kukosa consistency.Kuna sababu gani ya msingi ya kuajiri waalimu wa Division IV tena,wa course ya ualimu ya mwaka mmoja tu(Voda Fasta).Kulikuwa na ulazima gani na haraka gani ya kuanzisha Shule za Kata,huku tukijua kwamba hazina vifaa,waalimu wanaofaa na mazingira mazuri ya kufundishia na mengine mengi?Jibu ni moja tu,nia ni kuharibu elimu,ili kusiwe na watu wenye weledi wa kusimamia rasilimali zao na maendeleo ya nchi yao.

Labda katika swala la Watanzania kutokuwa na weledi unaotakiwa kuendesha bandari,niongeze jambo lingine la msingi.Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tabia ya kutoa ajira kindugu na kujuana.Sina shaka yeyote kwamba mfumo huu wa ajira ume-compromise sana weledi,na hii haijaathiri utendaji Bandarini pekee tu,lakini serikalini kwa ujumla na kwenye mashirika yote.Na hapa niseme wazi,CCM na serikali zake zote inahusika,kwa kuwa haijaisimamia serikali zake vizuri kudhibiti uovu huu.

Kumekuwa na harakati nyingi kutoka CCM na serikali yake kuutetea mkataba huu kati ya Serikali na DP World. Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mkataba huu kwa kipimo chochote haufai,kwa hiyo kimsingi hakuna sababu yeyote ya kuendelea kuutetea na kulazimisha kuutekeleza, kwa kuwa wananchi hawautaki,na sababu kwa nini hawautaki iko wazi,hauna maslahi kwa Taifa lao.Kuendelea kuutetea na kuonyesha nia ya kuutekeleza ni kuendelea kuwatia wananchi hasira na ningeishauri CCM iache.

Hapa naomba niwe muwazi,Watanzania hawakatai uwekezaji katika bandari zao,au hata bandari ya Dar es Salaam, wanachokataa ni uwekezaji usio na maslahi kwao na taifa lao.

CCM inaongozwa na Rais wa machawa 🤣🤣🤣 aibu ya Dunia
 
Hukuna jeshi Happ la kufanya mapinduzi hakuna wote Ni vilaza tu wanajeshi wengi wanafikiria mapenz tu Sasa hv
Wanakata mauno na kuwa na michepuko lukuki, Kila bar wao Kila demu wanamtaka wao tu 🤣🤣🤣🤣
 
Ccm ilishafeli zamani mno, Ila raia bado wana imani nayo.
Unajua kwa nini "raia bado wana imani nayo"?
Binafsi nisingeandika kama ulivyofanya hapo, ningesema "raia walikuwa bado wana imani nayo."

Nadhani kuna umuhimu wa siku moja kuliandikia swala hili na "raia kuwa na imani na CCM" kwa muda mrefu kiasi hiki, hata baada ya chama hicho kuonekana kuwa kilishaharibika siku nyingi sana.
Kuna sababu muhimu ya kulieleza hili jambo.

Lakini sasa ni dhahiri kabisa, hawa raia sasa wametambua kuwa CCM siyo chama cha siasa tena bali ni genge tu la walaji. Ninaamini raia watatoa hukumu yao safari hii.
 
CCM inaongozwa na Rais wa machawa 🤣🤣🤣 aibu ya Dunia
Eti Rais anaita loyalists wake Chawa na wenyewe wanafurahi,ajabu sana.Hivi wanajua kweli kwamba Chawa ni mdudu ambaye kadharaulika site.Sidhani, maana wangejua wasingechekelea kuitwa Chawa.
 
Ndo mnavyojidanganya sio? Mtasubiri sana

Samia hadi 2030 kwa Jina la Yesu
Yesu yupi wewe unayemwamini mkuu.Mtu anayemwamini Mungu hawezi kuchukuliana na waovu.Watawala ni watu waovu sana mkuu na hao wa kwetu sio exception.Tumeshuhudia wakifanya na kutufanyia uovu mwingi sana tangu Uhuru.Hili la DP World ni marudio tu.
 
Bila kujali ni Samia au mwingine, CCM itashinda tena na kelele zitaendelea. Na hata siku Upinzani ukipewa nchi kelele zitakuwepo.
 
Kwa hiyo unahalalisha tyranny mkuu.Swala sio "kutawala" at any cost,swala ni "kuongoza" nchi vizuri.
 
Back
Top Bottom